Iringa: DC Kasesela aokoa roho za watu kwenye ajali ya Mlowa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Mkuu Wa Wilaya ya Iringa akitoka kwenye kusikiliza mgogoro wa wakulima na wafugaji Idodi, alikuta ajali ndio imetokea ikabidi asimame na kuanza kuokoa majeruhi ambapo dereva alikimbizwa hospital ya mkoa na amelazwa wodi 5 katika hospital hiyo hali yake inaendelea vizuri

Dereva aliyetambulika kwa jina moja tu Michael Mkoroma akiwa na abiria Deogras Luoga na Miraji Mohamed wote watumishi Wa chuo cha DUCE walikuwa kwenye gari

Gari ya chuo kikuu kishiriki DUCE ilikuwa ikitokea kwenye ziara ya utafiti Ruaha National Park ilipinduka kwenye kona ya Mlowa kutokana na barabara kuwa na tuta pamoja na viinuko vidogo vidogo maarufu kwa jina la rasta

Mkuu Wa wilaya mhe kasesela mwenye shati jeupe la maua akiongoza kunyanyua gari
 
Hio barabara kama sio mzoefu ni mbaya sana..utafikiri haiendi ruaha national park
 
Ila Kasesera kwa kiki yupo juu. Yeye kuokoa tu. Mara utasikia "... kaokoa watu kwenye mafuriko Idodi, kabeba waathirika kwenye janga. Na hii amenyanyua gari kwa mikono yake mwenyewe..."! Safi lakini.
 
aiseee sasa huyu driver anaitupaje mahali kama hapo ? angeingia ngorongoro crater ingekuwaje / rasta ya serengeti
Pole majeruhi wote.Daah umenikumbusha barabara ya Ngorongoro-Mar(l?)anja,Naabi,Seronera,Ikoma/Ndabaka.Hiyo ndiyo barabara hatari ya rough road kwa Tanzania kama sijakosea.Ina mbavu za mbwa,mawe(loose rocks) na kona kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…