Watu 14 wafariki katika ajali mbaya ya barabarani Kenya

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Watu 14 wamethibitishwa kufariki huku wengine kumi na watatu wakijeruhiwa katika ajali mbaya eneo la Kakwamunyen kando ya barabara ya Lodwar-Kakuma Jumamosi usiku .

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, waliofariki ni wanawake wanane watu wazima watatu wa kiume na watoto watatu wa kiume.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Turkana, Lemmy Njiru alisema kuwa dereva wa lori lililokuwa limepakia kupita kiasi alikumbana na ngamia eneo la Kakwamunyen ambaye aliamua kuepuka kumgonga.

Bw Njiru alisema ngamia huyo alikuwa akivuka barabara kutoka kushoto kwenda kulia na dereva aliyetambulika kwa jina la Bw David Ekitela alikwepa kulia ili kukwepa kumgonga na kutokana na uzito wa gari hilo alishindwa kulidhibiti.

"Baadaye gari hilo lilipinduka na kutua kwenye mtaro upande wa kulia wa barabara na kusababisha vifo, majeraha na uharibifu mkubwa kwa lori," mkuu wa polisi alisema.

Manusura wote walikimbizwa katika Kaunti ya Lodwar na Hospitali ya Rufaa kwa matibabu. Miili ya walioaga dunia ilihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo hicho ili kusubiri kufanyiwa uchunguzi.

BBC Swahili
 
Back
Top Bottom