Iringa: DC Kasesela aokoa roho za watu kwenye ajali ya Mlowa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,634
Points
2,000

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,634 2,000
Mkuu Wa Wilaya ya Iringa akitoka kwenye kusikiliza mgogoro wa wakulima na wafugaji Idodi, alikuta ajali ndio imetokea ikabidi asimame na kuanza kuokoa majeruhi ambapo dereva alikimbizwa hospital ya mkoa na amelazwa wodi 5 katika hospital hiyo hali yake inaendelea vizuri

Dereva aliyetambulika kwa jina moja tu Michael Mkoroma akiwa na abiria Deogras Luoga na Miraji Mohamed wote watumishi Wa chuo cha DUCE walikuwa kwenye gari

Gari ya chuo kikuu kishiriki DUCE ilikuwa ikitokea kwenye ziara ya utafiti Ruaha National Park ilipinduka kwenye kona ya Mlowa kutokana na barabara kuwa na tuta pamoja na viinuko vidogo vidogo maarufu kwa jina la rasta

Mkuu Wa wilaya mhe kasesela mwenye shati jeupe la maua akiongoza kunyanyua gari
 

Kasongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2007
Messages
2,836
Points
2,000

Kasongo

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2007
2,836 2,000
aiseee sasa huyu driver anaitupaje mahali kama hapo ? angeingia ngorongoro crater ingekuwaje / rasta ya serengeti
Pole majeruhi wote.Daah umenikumbusha barabara ya Ngorongoro-Mar(l?)anja,Naabi,Seronera,Ikoma/Ndabaka.Hiyo ndiyo barabara hatari ya rough road kwa Tanzania kama sijakosea.Ina mbavu za mbwa,mawe(loose rocks) na kona kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,391,509
Members 528,420
Posts 34,083,183
Top