TANZIA Kahama: Watu 19 wafariki dunia kwenye ajali inayohusisha trekta, hiace na lorry!

Mama Debora

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
1,482
2,582
Ni usiku (saa nne) wa kuamkia leo Agosti 9, 2022.

Gari ndogo IST inatokea Kahama, inaelekea Tinde. ikaparamia trekta lililokua mbele limejaza kuni halafu halina taa za nyuma wala reflector. Watu watatu wakafa kwenye IST!

Dereva wa Trekta akakimbia!

Wakati uokoaji unaendelea, ikaja Hiace iko full nyomi full speed, kutoka Kahama kuelekea Tinde.

Kufumba kufumbua mbele (kwenye ajali ya Trekta na IST) wametandaza majani, uokoaji unaendelea. It was too late!

Dereva wa Hiace akapoteza control, akakwepa lile Trekta akaparamia Lori lililokua limepunguza mwendo kupisha uokoaji upande wa pili wa barabara. Paaaaaahh!!

Watu 16 wakafa papo hapo (na dereva akiwemo)!

Jumla watu 3 + 16 = 19!

Majeruhi 15 wamekimbizwa Hospital ya manispaa ya Kahama (mmoja amekata moto, wamebaki 14)

Kwenye IST imekutwa chupa ya Konyagi (Kvant)

RPC na RC Shinyanga wamefika eneo la tukio Alfajiri.

ee.jpg
 
Ni usiku wa kuamkia leo Agosti 9, 2022.

Lori linatokea Kahama fresh, linaelekea Tinde. Likaparamia trekta lilokua mbele limejaza kuni halafu halina taa za nyuma wala reflector. Watu watatu wakafa!

Wakati uokoaji unaendelea, ikaja Hiace iko full nyomi full speed, kutoka Kahama kuelekea Tinde.

Kufumba kufumbua mbele (kwenye ajali ya Trekta na Lori) wametandaza majani, uokoaji unaendelea. It was too late!

Dereva wa Hiace akapoteza control, akakwepa lile Trekta akaparamia Lori lingine upande wa pili wa barabara.

Watu 16 wakafa papo hapo (na dereva mmojawapo)!

Jumla watu 19!

Majeruhi wamekimbizwa Hospital ya manispaa ya Kahama.

Dereva wa Trekta amekimbia usiku huohuo (anajua makosa yake)!

RPC na RC Shinyanga wamefika eneo la tukio Alfajiri.

View attachment 2318712
Jamani jamani jamani

Damu ya Watanzania inamwagika kama tupo vitani vile.

Wenye Imani tusiache kuiombea nchi

Moyo wangu umeumia sana
 
Hizi ajali pasipo madereva wenyewe kuacha kuendesha kwa mwendo kasi haziwezi kwisha, hatuwezi kutegemea askari wa usalama barabarani kila siku waokoe maisha yetu kama abiria ndani ya mabasi hatuwaambii madereva ukweli wapunguze mwendo.
 
Daah haya magar makubwa na taa za nyuma ni tatizo sana.

Unaweza kuta linakunja kona bila indicator yoyote kuwashwa(hazina).
Duuh ndugu umeelewa kweli kilichoelezwa na chanzo cha ajali ni nini umeelewa?

Hazina ndio harzad?

Kosa la trekta kutokuwa na taa wala reflector na haya ni makosa yanajirudia rudia sana juu ya hii mitambo haisimamiwi kabisaa
.mwenye hiace hakuwa na tahadhari moto mchibuyu umewawahisha ndugu zetu mbele ya haki na hiyo njia huwa hakuna matuta basi ni kufuta kisahani tena usiku hakuna "watoto yatima wale".

Mwendokasi ni hatari sana ndugu zangu madereva na ajali inazuilika palipo na subira na kuepuka mashindano tuache papara barabarani tu wapi barabarani na pia tahadhari ni muda wote vicheche ni vingi usiku tuwe makini sana.

Poleni ndugu na jamaa zetu huko kahama.
 
Nakala aipate kinana
Ni lini ajali hazikuwepo kwasababu ya traffic kujazana barabarani? Too pathetic!

Kuwapunguza askari wa barabarani kumeanza juzi tu ila kabla ya hapo ajali zilikuwa kila siku.

Traffic hawapo barabarani kwa ajili ya kukagua magari mzee unless kama huna gari, pikipiki ama chombo chochote cha moto.

Wale ni wakusanya rushwa tu wanadai buku mbili kwa nguvu uondoke hata ukiwa na skrepa barabarani hawajali utajua mwenyewe mbele ya safari.
 
Nakala aipate kinana
Uganda walitimua askari barabarani wakabaki wa kuhesabu mmoja mmoja tu lakini suala la ajali ni kitendawili.

Zambia unaweza kutembea kilometers 500 usikutane na askari barabarani zaidi ya watu wa uhamiaji tu na hakuna ajali za kizembe kama hapa kwetu wanapolundikana traffic kila baada ya kilomita 3.

Elimu kwa madereva na wasafiri kwa ujumla ndiyo inaweza kupunguza ajali.

Ama itumike njia ya artificial intelligence ambayo itawaondoa traffic wote barabarani kwakuwa mfumo haudai rushwa kama hawa viumbe.
 
Ni usiku wa kuamkia leo Agosti 9, 2022.

Lori linatokea Kahama fresh, linaelekea Tinde. Likaparamia trekta lilokua mbele limejaza kuni halafu halina taa za nyuma wala reflector. Watu watatu wakafa!

Wakati uokoaji unaendelea, ikaja Hiace iko full nyomi full speed, kutoka Kahama kuelekea Tinde.

Hivi Hiace ina capacity ya kubeba watu wangapi? Assume watu wazima.

Kufumba kufumbua mbele (kwenye ajali ya Trekta na Lori) wametandaza majani, uokoaji unaendelea. It was too late!

Dereva wa Hiace akapoteza control, akakwepa lile Trekta akaparamia Lori lingine upande wa pili wa barabara.

Watu 16 wakafa papo hapo (na dereva mmojawapo)!

Jumla watu 19!

Majeruhi wamekimbizwa Hospital ya manispaa ya Kahama.

Dereva wa Trekta amekimbia usiku huohuo (anajua makosa yake)!

RPC na RC Shinyanga wamefika eneo la tukio Alfajiri.

View attachment 2318712
So sad huu mwaka sio poa
 
Habari ngumu sana asubuhi tunaipokea!
Mungu awajalie pumziko la amani waliofariki, walio jeruhiwa wapate wepesi wa kupona , pole kwa ndugu jamaa na wanaohusika wote.

Tuendelee kuwa na tahadhari tuwapo barabarani kwani ni heri kukawia ufike.
 
Uganda walitimua askari barabarani wakabaki wa kuhesabu mmoja mmoja tu lakini suala la ajali ni kitendawili.

Zambia unaweza kutembea kilometers 500 usikutane na askari barabarani zaidi ya watu wa uhamiaji tu na hakuna ajali za kizembe kama hapa kwetu wanapolundikana traffic kila baada ya kilomita 3.

Elimu kwa madereva na wasafiri kwa ujumla ndiyo inaweza kupunguza ajali.

Ama itumike njia ya artificial intelligence ambayo itawaondoa traffic wote barabarani kwakuwa mfumo haudai rushwa kama hawa viumbe.
Watanzania tunakaririshwa tunaridhika, hatuna tabia ya kujitafutia vitu/maarifa mapya ili kuyapima tunayo karirishwa kama ni ya kweli au la.
Waganda wamewezaje bila askari barabarani kuzuia ajali? Mahakama zao ni masaa 24 kwa madereva wazembe.
Maafisa wao wengi kozi zao wanasoma Tanzania,hawapati muda wa kubadilishana mbinu za uongozi?
Waswahili tuna safari ndefu kufikia suluhisho...
 
Nakumbuka kuna siku moja nilipanda gari kutoka dodoma kwenda mbeya. Ilikuwa usiku kwenye barabara ya mafinga makambako dereva anapitisha gari kwenye matuta kwa spidi abiria tunaruka juu ila tumepiga kimya tu. Nakumbuka wakati huo nilikuwa katika hali ya kutapika nilikuwa nimejikunja kwenye siti ili nijizuie so kwa upande wangu nilishindwa kufanya chochote ila ningekuwa comfortable ningefanya kitu aisee.
 
Back
Top Bottom