Sasa wasukuma si sawa na hao Ashkenazi mkuu ambao kihistoria ni jamii ya Japhet na sio shem ambaye ndiye mzizi wa kina Abraham na wayahudi wengine?? Ashkenazi wanatajwa wapi kwenye Biblia kama waisrael halisi?? Nasubiri andiko unisaidie.
2. Hao wanaorudi wanakuwa traced vipi kuwa ni Original israelites ilihali hayo makabila 10 yalishakuwa contaminated toka enzi za Yesu na yakatengwa na Ufalme wa Yuda?? Watakuwaje tena waisrael halisi hadi leo mseme wanarudi taratibu?? Mind you 70% ya waisrael wote duniani ni Ashkenazi sasa hao makabila 10 ndio yanamake 30%???
3.Mungu aliwarudisha ndio lakini kupitia manabii sio wahuni wapagani wa kiingereza na marekani ambao ndio wanawapa silaha kila mwaka ili kuwalinda alafu leo mnahusianisha na Mungu!! Hivi kweli Mungu anategemea nguvu za marekani ili israel i-survive?? Hamuoni mnamdhalilisha Mungu wenu??
Ashkenazi jamii ya Yafeti inatajwa kwenye Mwa 10:2-3
2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, .....
3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, .......
Huyu hana uhusiano na Ashkenaz Jews.
//Wanaorudi watakuwa traced vipi?// ------- anayewa-trace ni nani? Mungu alisema Yeye ndiye atawaleta kutoka pande nne za dunia. Yeye ndiye anayejua amlete nani na amuache nani. Ndugu, maandiko hayajasema mwanadamu yeyote afanye tracing na kuwaleta.
//Mungu aliwarudisha ndio lakini kupitia manabii sio wahuni// -------- sio kweli. Mungu anatumia yeyote amtakaye ili kutekeleza ahadi zake. Alimtumia Koresh (Cyrus) mfalme mpagani wa Irani (Uajemi) kuwahimiza Wayahudi warudi Ireali na kwenda kujenga nyumba ya Mungu wao.
Ezra 1:
1 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema
kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi,
hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi;
3 Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee
mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu),
iliyoko Yerusalemu.