Iran na Israeli zajibizana kuhusu Tel Aviv

Kama tu israel ingeweza kuwa na aircraftcarrier moja au strategic bomber kama B-52 au B-2,dunia ingekoma,na iran angekuwa anashambuliwa mno,
marekani japo wako karibu mno na israel lakini haina maana kuwa wamepagawa kiasi cha kumpa israel,silaha za long range power projection
 
Ni kweli wanaushawishi duniani lkn ......kama vile wa kubumba maana huyu jamaa mwenye Facebook kabla hajaigundua fb alikuwa ni mmarekani lkn baada ya ugunduzi akawa muisrael same to
Huyu jamaa anaeunda rocket za usa
IN FACT THEY CONTROL THE WORLD.

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Israel maana yake ni MSHINDI sio lazima imaanishe lile taifa la wana wa yakobo

Hoseah 11:1
1 Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri

Na hapa alikuwa anatabiri kuwa mtoto wake yaani Israel/Yesu ataenda misri na baadae kurudi Judea sababu ya kumuepusha na hasira za Herodius.

Unabii unatimia hapa

Mathayo 2:15
15 akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii (Hoseah), akisema,''Kutoka Misri nalimwita mwanangu''

Sasa huoni connection kati ya huo mstari wa Hosea wa kuhusu Israel kuwa alimaanisha Yesu na sio Israel?? Au Mathayo amepotosha mkuu

Zunguka kote duniani kwa vyuo vyote vya theologia na wachungaji.... Ni hivi unabii wa Agano la kale unahusu kuja kwa Yesu sio kitu kingine chochote. So zakaria hapo alikuwa anatabiri kwamba Yesu ambaye of course atazaliwa Israel ndio atakuwa hilo JIWE so huo ni unabii wa kiroho kuwa Yesu atakuwa TOP wa wote ila haimaanishi Israel eti ya kina Netanyahu ndio ilitabiriwa hapo hapana.... Ni Israel chini ya YESU

I hope tumeelewana
Ukipata muda fanya google search ya Duality of prophecy fulfillment au Double fulfillment of biblical prophecies utajifunza jambo.

Unabii wa biblia hutimia mara moja, mbili au zaidi.
Hosea 11:1 inahusu Israeli kama taifa na inamhusu Yesu.
Sio ila neno humo linamhusu Yesu.

Hosea 11 anasema:
1 Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri.
2 Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia
uvumba sanamu za kuchonga.

Aya ya 1 inamhusu Israeli kama taifa na inamhusu Yesu.

Aya ya 2 inamhusu Israeli lakini si Yesu. Mungu anasema, kadiri huyo mtoto alivyoitwa na Mungu, ndivyo alivyozidisha uasi kwa kuwatolea dhambihu miungu mingine.

Je, Yesu aliwahi kumtolea dhabihu mungu gani wa uongo?
Jibu ni hakuwahi hata mara moja.
Israeli kama taifa je?
Jibu ni mara kibao.
 
Mkuu hili swala nmeshalijadili sana humu JF kuwa Israel ya kimwili haina nafasi tena kibiblia hivyo unabii wote wa kuhusu Israel ya kale unahusianisha na Israel ya kiroho yaani wafuasi wote wa Yesu ningeomba utenge muda upitie huu uzi wangu nategemea utapata vitu viwili vitatu.

Je, Israel ya sasa ni Taifa teule la Mungu au ni propaganda tu za kanisa? - JamiiForums
 
Nini kinaifanya Israeli ya kimwili idumu hadi leo wakati imezungukwa na rundo la wanaoichukia pande zote. Mabilioni ya watu wameshimdwa kuitokemeza nchi yenye watu milioni chache. Why?
 
MAREKANI na UINGEREZA..... Zaidi ya hapo Israel haina lolote ndio maana kabla ya 1948 walikuwa kila vita wanatandikwa huko Ulaya.... Kumbuka Jeshi lao la ZZW la kule warszaw Poland lililokuwa linalinda wayahudi wa ulaya ya mashariki lilichakazwa vikali na wayahudi zaidi ya elfu 80 wakateketezwa na Jeshi la ujerumiani mwaka 1940s.

Tokea pale nkajua kumbe wayahudi sio invicibles wanakufa tu kama mimi na wewe.... Kujua hilo wakaokolewa na wamarekani so ndio wanawapa kiburi hadi leo, zaidi ya hapo hawana lolote la ziada kuliko sisi wengine. Siku marekani akimuacha utakuja niambia mkuu kipigo atakachopata sidhani kama atarudi kusimulia ni zaidi ya walichopewa na Hitler.

Muda utaongea
 
Maana ya hayo uliyoeleza ni hii hapa ambayo Mungu alisema kupitia nabii Yeremia miaka mingi kabla Wayahudi hawajafika Ulaya na kwingineko:

(Jer 9:15-16) Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe. Nami NITAWATAWANYA KATI YA MATAIFA, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, NAMI NITATUMA UPANGA NYUMA YAO, hata nitakapowaangamiza kabisa.

Lakini pamoja na hiyo hukumu, ilikuwapo ahadi ambayo ilitimia na inaendelea kutimia hadi leo:
(Isa 43:5-6) USIOGOPE; maana mimi ni pamoja nawe; NITALETA WAZAO WAKO TOKA MASHARIKI, nitakukusanya toka MAGHARIBI; nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.
 
Jeremiah alikuwa anaongea after the fact,wayahudi hawajaanza kuwa uhamishoni leo,ni kabla jeremiah hajazaliwa,huo sio unabii ni inspiration za ukombozi kama wanazokuwa nazo akina che guevelar,mandela etc
 
Zamani zama za kale kila jamii ilikuwa na mungu wake,na ili ionekane mungu wa jamii fulani ana nguvu,jamii husika ilikuwa na nguvu za kijeshi na mara kwa mara walishinda vita,
mungu alihusisha na ushindi wa jamii fulani dhidi ya jamii zingine,
kama vile wayahudi walivyokuwa na mungu wao yhwh,pia jamii kama babel,asyria etc nao walikuwa na miungu yao waliyoimba katika vita na waliposhinda,imani ilikuwa kwamba ni kwa nguvu ya mungu wao
 
Inashangaza mno pale mungu anaesemwa anahusishwa na mambo ya vita na mauaji,sidhani kama kazi ya mungu ni kupigaanisha vita,hii ni imani za kale ambazo wayahudi walifanikiwa kuzipandikiza mpaka leo,
ama kuhusu sijui kutawanywa kwa mataifa,ukweli ni kuwa kila jamii pale middle east zama zile imetawanywa kwa mataifa,sasa huwa sielewi what is so speacial about wayahudi kutawanywa kwa mataifa,
mfano,Aram kingdom,iliungana na israel kingdom kuipiga Judea kingdom baada ya yudah kukataa kuungana nao kuasi dhidi ya asyrian empire ilikuwa ikiwatoza kodi,yudah wakaomba msaada asyrian empire,ambapo walikuja na kuiangusha Aram kingdom na kuwachukua utumwani asyrian,kisha walirudi na kuuangusha israel kingdom nao pia kupelekwa uhamishoni,
sasa hapa kwanini issue ya israel kwenda uhmishoni ikawa special case kuzidi Aram kingdom?
 
Ukichukua case ya israel kingdom kuchukuliwa utumwani ambapo ilikuwa ni pure geopolitical za wakati huo,
wenzetu hawa wayahudi wakaijengea spritual concept,
eti makabila 10 ya israel,yalimwasi jehova,sasa kwa hasira jehova akaamua makabila kumi ya wana wa israel yapotee na waka yasipatikane tena,
ukweli ni kuwa wayahudi walikuwa na uadui na israel kingdom,na hii ni baada ya Daudi kuasi na kupora utawala kutoka kwa king Saul,
uhasama wa the house of saul na the house of David,ndo ulipelekea baadae israel imeguke mapande mawili,Israel kingdom na Yuda kingdom,na hizi kingdom zilikuwa ni maaadui,
watu wa israel kingdom hawakupata kumuabudu jehova
 
Maana ya hayo uliyoeleza ni hii hapa ambayo Mungu alisema kupitia nabii Yeremia miaka mingi kabla Wayahudi hawajafika Ulaya na kwingineko:

(Jer 9:15-16) Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe. Nami NITAWATAWANYA KATI YA MATAIFA, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, NAMI NITATUMA UPANGA NYUMA YAO, hata nitakapowaangamiza kabisa.

Lakini pamoja na hiyo hukumu, ilikuwapo ahadi ambayo ilitimia na inaendelea kutimia hadi leo:
(Isa 43:5-6) USIOGOPE; maana mimi ni pamoja nawe; NITALETA WAZAO WAKO TOKA MASHARIKI, nitakukusanya toka MAGHARIBI; nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.
Mkuu shida ya unabii ni kwenye utafsiri..... Mna uhakika gani kwamba israel hii ya sasa ndio imerudishwa pale na Mungu?? Je mnawezaje kutofautisha kati ya unabii wa kimungu na maigizo ya shetani!!

Mfano kuna dini miaka ya 1940 zilidai Hitler ndio mpinga kristo na WW 2 ndio vita ya Armageddon n.k na zikapata wafuasi wengi ila je dunia iliisha?? Sasa kwanini tushawishike kuwa unabii umetimia wakati wa Israel ya sasa imewekwa hapo na wapagani bila hata nabii wa Mungu kuhusika!! How can we differentiate?

Mimi pamoja na kusoma Biblia ila siamini kama Israel hii ya sasa ndio inaongelewa kwenye Biblia maana imeasisiwa kwa ulaghai,ujanja ujanja,kihuni na kidhalimu kuihusisha na Mungu ni kumchafua.
 
Huku İran ikitishia kuifuta Tel Aviv na Haifa katika ramani, Netanyahu awaonya wasijaribu kufanya makosa hayo
Vita kali ya Maneno baina ya İran na İzrael
Waziri mkuu wa İzrael Benjamin Netanyahu ameijibu kauli ya İran isemayo kama Marekani ikiishambulia İran basi İran watalipiza kisasi kwa Kuifuta Tel Aviv na Haifa katika uso wa dunia.

Netanyahu amesema kama İran itajaribu kufanya makosa ya kuifuta Tel Aviv na Haifa katika uso wa dunia huo ndio utakuwa mwaka mpya wao wa mwisho kuusherekea.

Netanyahu alisema hawajavipuuzia vitisho vinavyotolewa na İran lakini pia hawajatishika kwa vitisho hivyo.

Netanyahu alisema kama uongozi wa sasa wa İran ulıopo madarakanı utajarıbu kufanya makosa ya kuifuta Tel Aviv na Haifa, kıtu ambacho hawatafanikiwa lakini huo ndio unaweza kuwa mwaka mpya wao wa mwisho kuusherekea.

Mmoja wa makamanda wa jeshi la İran Yadullah Javani aliliambia shirika la habari la İran İRNA hapo jana kwamba kama Marekani itaishambulia İran basi na wao (Iran) wataifuta Tel Aviv na Haifa katika ramani.

Trt
Waarabu wanaijua vizuri Israeli, kilichowapata miaka zaidi ya 30 iloyopita tena Nchi za kiarabu zenye nguvu zikiwa zaidi ya 7 walikula kichapo cha mbwa koko
 
Aiseee, lakini kwanini wanamkana YESU/MUNGU MTU, na hawautambui UKRISTO. Mkuu, wewe ni yahudi black unaweza kunijuza kidogo
 
Mkuu shida ya unabii ni kwenye utafsiri..... Mna uhakika gani kwamba israel hii ya sasa ndio imerudishwa pale na Mungu?? Je mnawezaje kutofautisha kati ya unabii wa kimungu na maigizo ya shetani!!

Mfano kuna dini miaka ya 1940 zilidai Hitler ndio mpinga kristo na WW 2 ndio vita ya Armageddon n.k na zikapata wafuasi wengi ila je dunia iliisha?? Sasa kwanini tushawishike kuwa unabii umetimia wakati wa Israel ya sasa imewekwa hapo na wapagani bila hata nabii wa Mungu kuhusika!! How can we differentiate?

Mimi pamoja na kusoma Biblia ila siamini kama Israel hii ya sasa ndio inaongelewa kwenye Biblia maana imeasisiwa kwa ulaghai,ujanja ujanja,kihuni na kidhalimu kuihusisha na Mungu ni kumchafua.
Uhakika uko wazi tu. Mungu alisema "Nitawatawanya" na akawatawanya. Kisha akasema, "Nitawarudisha" na akawarudisha baada ya kuwa nje ya Israeli baada ya miaka takribani 2000. Kuhusu Armagedon itakuwaje Hitla wakati Biblia inataja ni wapi vita hiyo itapiganwa?

(Yoeli 3:2) NITAKUSANYA MATAIFA YOTE, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafau, na huko NITAWAHUKUMU kwa ajili ya watu wangu, na KWA AJILI YA URITHI WANGU, ISRAELI, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.

Kinachofanyika sasa ni maadui wote wa Israel wanazidi kujawa na chuki na hasira. Kuna siku watashindwa kujizuia. Kisha wataenda kuizunguka Israeli ili kuifuta kwenye ramani ya dunia kama walivyotaka miaka yote. Lakini hapo ndipo mtego utawanasa kama ndege. Wataangukia kwenye maangamizi makuu. Na ndipo wataelewa somo.
 
Yalishapimwa na yakaonekana hayana madhara yoyote; why should you waste resources kwa kitu ambacho hakina madhara?

Kwa case ya Iran, projectile yoyote itakayokuwa intercepted ikitokea upande wa Iran au base yoyote ya Iran kuelekea Israel; nawahurumia wote waishio Tehran na miji mingine ya Iran. Mungu apishe mbali maana kichapo chake nashindwa kupata picha kitakavyokuwa hata ikibidi Sabato itavunjwa siku hiyo.
Utakua ndio mwaka wao mpya wa mwisho.

Hapa nahisi Israel atashusha nukes tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhakika uko wazi tu. Mungu alisema "Nitawatawanya" na akawatawanya. Kisha akasema, "Nitawarudisha" na akawarudisha baada ya kuwa nje ya Israeli baada ya miaka takribani 2000. Kuhusu Armagedon itakuwaje Hitla wakati Biblia inataja ni wapi vita hiyo itapiganwa?

(Yoeli 3:2) NITAKUSANYA MATAIFA YOTE, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafau, na huko NITAWAHUKUMU kwa ajili ya watu wangu, na KWA AJILI YA URITHI WANGU, ISRAELI, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.

Kinachofanyika sasa ni maadui wote wa Israel wanazidi kujawa na chuki na hasira. Kuna siku watashindwa kujizuia. Kisha wataenda kuizunguka Israeli ili kuifuta kwenye ramani ya dunia kama walivyotaka miaka yote. Lakini hapo ndipo mtego utawanasa kama ndege. Wataangukia kwenye maangamizi makuu. Na ndipo wataelewa somo.
Mkuu Kibiblia mara zote Israel walikuwa wakirudishwa na manabii wa Mungu je kuna nabii gani kawarudisha waisrael??

Israel ilikuwa na makabila 12 na makabila 10 mpaka sasa yamepotea yalibaki mawili tu Yuda + Benjamin je pale Tel aviv mbona yale makabila 10 hayapo?? Je Israel gani hiyo ambayo 70% ni jamii ya Ashkenazi pekee ilihali original israel ilikuwa na makabila 12??

Pia swali la msingi je kwanini Israel ya sasa muihusishe na unabii..... Ina maana hata leo hii nikibeba wasukuma nikawapeleka pale Israel nikasema hawa ndio wayahudi basi mtasema MUNGU ndio kawarudisha Israel?? Yaani how do you tell kama ni unabii wa Mungu na sio mpango wa wapagani wachache?? Yaani kwanni mseme Mungu ilihali ni wapagani walioshiriki kuwarudisha kwa maslahi yao wanayolinda hadi leo??

Mie naamini Israel ya kweli kama itarudi basi itarudishwa na Mungu sio wahuni wachache alafu tunaingizwa kwenye mtego wa kuaminishwa ni Mungu ndio kawarudisha....
 
Waarabu wanaijua vizuri Israeli, kilichowapata miaka zaidi ya 30 iloyopita tena Nchi za kiarabu zenye nguvu zikiwa zaidi ya 7 walikula kichapo cha mbwa koko
Iran sio waarabu mkuu muwe mnasoma kwanza kabla ya kuchangia..... Kingine Mbona husemi waisrael pia wanamjua HITLER alivyowachinja kama wanavyodai Million 6 miaka 60 iliyopita??

Alafu msipende kuwatofautisha Israel na "waarab" maana wote ni jamii moja yaani Semites na hata Yakobo alioa "waarab" wa Syria ndio akazaa hao watoto 12 walioasisi taifa la Israel sasa kusema "waarab" sijui wanawajua Israel ni kushindwa fahamu historia zaidi ungesema waarab wanawajua watoto wa ''Ma mdogo'" zao!!

Nachoona wafia dini wengi tunafuata mkumbo tu bila kujua chanzo na historia wa huu mgogoro wa Israel mashariki ya kati
 
Mkuu Kibiblia mara zote Israel walikuwa wakirudishwa na manabii wa Mungu je kuna nabii gani kawarudisha waisrael??

Israel ilikuwa na makabila 12 na makabila 10 mpaka sasa yamepotea yalibaki mawili tu Yuda + Benjamin je pale Tel aviv mbona yale makabila 10 hayapo?? Je Israel gani hiyo ambayo 70% ni jamii ya Ashkenazi pekee ilihali original israel ilikuwa na makabila 12??

Pia swali la msingi je kwanini Israel ya sasa muihusishe na unabii..... Ina maana hata leo hii nikibeba wasukuma nikawapeleka pale Israel nikasema hawa ndio wayahudi basi mtasema MUNGU ndio kawarudisha Israel?? Yaani how do you tell kama ni unabii wa Mungu na sio mpango wa wapagani wachache?? Yaani kwanni mseme Mungu ilihali ni wapagani walioshiriki kuwarudisha kwa maslahi yao wanayolinda hadi leo??

Mie naamini Israel ya kweli kama itarudi basi itarudishwa na Mungu sio wahuni wachache alafu tunaingizwa kwenye mtego wa kuaminishwa ni Mungu ndio kawarudisha....
- //Israeli walirudishwa na manabii// ---- hakuna andiko la hivyo. Aliyewarudisha ni Mungu.
- Israeli ilikuwa makabila 12, sawa. Bado wanaendelea kurudi. Fanya google search ya "Jews aaliyah" utapata mengi zaidi.
- Tunaihusisha Israeli na unabii kwa mujibu wa maandiko. Ukibeba wasukuma ukatupa andiko linalojustify kitendo hicho, hatuna shida. Suala ni maandiko tu.
 
Sasa wasukuma si sawa na hao Ashkenazi mkuu ambao kihistoria ni jamii ya Japhet na sio shem ambaye ndiye mzizi wa kina Abraham na wayahudi wengine?? Ashkenazi wanatajwa wapi kwenye Biblia kama waisrael halisi?? Nasubiri andiko unisaidie.

2. Hao wanaorudi wanakuwa traced vipi kuwa ni Original israelites ilihali hayo makabila 10 yalishakuwa contaminated toka enzi za Yesu na yakatengwa na Ufalme wa Yuda?? Watakuwaje tena waisrael halisi hadi leo mseme wanarudi taratibu?? Mind you 70% ya waisrael wote duniani ni Ashkenazi sasa hao makabila 10 ndio yanamake 30%???

3.Mungu aliwarudisha ndio lakini kupitia manabii sio wahuni wapagani wa kiingereza na marekani ambao ndio wanawapa silaha kila mwaka ili kuwalinda alafu leo mnahusianisha na Mungu!! Hivi kweli Mungu anategemea nguvu za marekani ili israel i-survive?? Hamuoni mnamdhalilisha Mungu wenu??
 
Back
Top Bottom