Iran na Israeli zajibizana kuhusu Tel Aviv

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,924
2,000
Huku İran ikitishia kuifuta Tel Aviv na Haifa katika ramani, Netanyahu awaonya wasijaribu kufanya makosa hayo
Vita kali ya Maneno baina ya İran na İzrael
Waziri mkuu wa İzrael Benjamin Netanyahu ameijibu kauli ya İran isemayo kama Marekani ikiishambulia İran basi İran watalipiza kisasi kwa Kuifuta Tel Aviv na Haifa katika uso wa dunia.

Netanyahu amesema kama İran itajaribu kufanya makosa ya kuifuta Tel Aviv na Haifa katika uso wa dunia huo ndio utakuwa mwaka mpya wao wa mwisho kuusherekea.

Netanyahu alisema hawajavipuuzia vitisho vinavyotolewa na İran lakini pia hawajatishika kwa vitisho hivyo.

Netanyahu alisema kama uongozi wa sasa wa İran ulıopo madarakanı utajarıbu kufanya makosa ya kuifuta Tel Aviv na Haifa, kıtu ambacho hawatafanikiwa lakini huo ndio unaweza kuwa mwaka mpya wao wa mwisho kuusherekea.

Mmoja wa makamanda wa jeshi la İran Yadullah Javani aliliambia shirika la habari la İran İRNA hapo jana kwamba kama Marekani itaishambulia İran basi na wao (Iran) wataifuta Tel Aviv na Haifa katika ramani.

Trt
 

popbwinyo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,845
2,000
Hii hadithi inanikumbusha mwanzoni mwa miaka ya 2000(s) wakati Taliban wanasimama juu milimani kule Afghanistan wakinyanyua AK 47 zao na kujinadi kuwa ;Iwapo USA angengia kwao wangemtia adabu.Mwishowe sikumbuki ilikuwaje.
Kilichofuata ni mayowe ya NCHI ZA KIISLAMU ZINAONEWA SANA,
ALLAH ATATUNUSURU WAJA WAKE

Sent using Jamii Forums mobile app
 

RTI

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
1,221
2,000
Hawa wote wanaogopana hawatapigana moja kwa moja wataendelea kupigania kwenye mataifa mengine.kwahiyo mnao subiri vita kati ya Iran na Israel mtasubiri sana.
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,675
2,000
Ayatollah ni kelele tu Mkuu ila anaujua vizuri moto wake endapo atafanya kosa la kujaribu kurusha bomu Israel; Iran itakula kichapo ambacho hakijawahi kufikiriwa!
Iran ameanza kuzungumza haya Maneno muda mrefu Sana, Hana uwezo wa kufanya huo ujinga, Kwanza amezungukwa na kambi za marekani nyingi sana, ambazo zina mashine zinazochunguza kila mradi unaofanyika hapo Irani. Kwy Google ukiangalia tuuu military base zilizopo karibia na Iran, zinaonyesha kwamba pale mashariki ya kati hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumsumbua Israel
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
5,675
2,000
Iran ameanza kuzungumza haya Maneno muda mrefu Sana, Hana uwezo wa kufanya huo ujinga, Kwanza amezungukwa na kambi za marekani nyingi sana, ambazo zina mashine zinazochunguza kila mradi unaofanyika hapo Irani. Kwy Google ukiangalia tuuu military base zilizopo karibia na Iran, zinaonyesha kwamba pale mashariki ya kati hakuna yeyote mwenye uwezo wa kumsumbua Israel
Angalieni izo Military Base zilizopo karibia na Irani
Ni shida
Screenshot_20190212-114727.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,559
2,000
Iraq chini ya sadam alirusha scud inside Israel zaidi ya Mara mbili lakini hakukuwa response yoyote ya haraka..

Sent using Jamii Forums mobile app
Yalishapimwa na yakaonekana hayana madhara yoyote; why should you waste resources kwa kitu ambacho hakina madhara?

Kwa case ya Iran, projectile yoyote itakayokuwa intercepted ikitokea upande wa Iran au base yoyote ya Iran kuelekea Israel; nawahurumia wote waishio Tehran na miji mingine ya Iran. Mungu apishe mbali maana kichapo chake nashindwa kupata picha kitakavyokuwa hata ikibidi Sabato itavunjwa siku hiyo.
 

Kanye2016

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
2,077
2,000
Hii hadithi inanikumbusha mwanzoni mwa miaka ya 2000(s) wakati Taliban wanasimama juu milimani kule Afghanistan wakinyanyua AK 47 zao na kujinadi kuwa ;Iwapo USA angengia kwao wangemtia adabu.Mwishowe sikumbuki ilikuwaje.
Jaribu kuangalia VICE utaona jamaa wanavyozidi kugain controll, Usisome na kusikiliza sana vyombo vya habari kutoka west wanaficha mambomengi sana
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
26,677
2,000
Jana nimeona BBC wakijadili ukuaji wa Influence ya Iran huko duniani,nikajua kumekucha sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom