kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,045
- 18,014
Jenerali Jaafari: Quds Tukufu Itakuwa kaburi la utawala bandia wa Kizayuni
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, lengo kuu la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds. Ameongeza kuwa: Mji wa Quds utakuwa kaburi la utawala bandia wa Kizayuni.
Meja Jenerali Mohammad Ali Jaafari ameyasema hayo Jumamosi wakati akizungumza na maafisa katika Kamandi Kuu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Akiashiria uamuzi wa hivi karibuni wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua rasmi mji wa Quds kama mji mkuu wa utawala bandia wa Israel, ameongeza kuwa: "Hayo yote ni utangulizi wa kuangamiza Msikiti wa Al Aqsa na Waislamu wanapaswa kufahamu kuwa, iwapo hawatachukua hatua za haraka kukabiliana na njama hii chafu, basi watapoteza wakati kwa kasi."
Meja Jenerali Jaafari amesema Marekani na utawala wa Kizayuni zimetenda ujinga mkubwa zaidi wa kihistoria dhidi ya Quds Tukufu na kuongeza kuwa: "Uamuzi huu ni matokeo ya mazungumzo na maafikiano yaliyofikiwa na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa Saudia Arabia." Amefichua Marekani ilizifahamisha nchi hizo za Kiarbau kuhusu uamuzi huo dhidi ya Quds miezi kadhaa iliyopita.
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema kuwa: "Utawala wa Saudi Arabia inataka Waislamu walaani tu kwa maneneo jinai ya hivi karibuni ya Marekani na waridhike tu na kutoa taarifa za kulaani." Amesema Saudia imefikia mapatano na Markeani pamoja na Israel kutochukua hatua zozote za kutetea na kuulinda mji wa Quds na kuhakikisha kuwa kadhia ya Palestina inaondlewa katika duara la masuala muhimu ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Meja Jenerali Jaafari ameashiria kusambaratika njama za maadui wa Umma wa Kiislamu na kusema: "Umma wa Kiislamu mara hii pia, sawa na kadhia za Kuristan ya Iraq, Lebanon na Yemen, itasambrataisha mehsabi ya maadui na kuwaadhibi wasaliti.
Source;parstoday