Meja Jenerali Salami: Gaza ni kaburi la Marekani na utawala wa Kizayuni

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,936
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo Gaza imekuwa uwanja wa kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni, na utawala naoikalii kwa mabavu Quds hauwezi kurejesha nguvu zake zilizopotea.

Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), amesema hayo leo katika hafla ya kufungaKongamano la Kitaifa la Fursa Zinazoibuka na Vitisho vya Baharini na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni unakabiliwa na kushindwa vibaya kusikowezekana kufidika.

Kamanda Salami ameashiria Operesheni ya Kimbunga cha Aqsa, na kusema: "Gaza leo kaburi la kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Utawala wa Kizayuni na nchi nyingine za magharibi zimefikia mahali ambapo zinadhania kwamba, kwa kuua watoto huko Gaza watapata amani na nguvu, lakini wanajua kwamba hawawezi kufikia malengo yao.

Meja Jenerali Salami ameongeza kusema kuwa, Iran iko katika ufuo wa bahari muhimu zaidi duniani na kwamba, asilimia 90 ya biashara ya dunia yakiwemo mafuta na gesi inafanywa kupitia bahari hiyo na kusema: Marekani inatumia fursa ya kuwa katika pwani ya bahari ili kuwa na satwa na na udhibiti kwa nchi zingine, na viongozi wao wanaamini kuwa hawawezi kufikiwa, lakini hii ni sera bandia na ya uwongo.

Akigusia uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kumfanya adui asijaribu kuishambulia katika uga wa bahari na kusema kuwa, mabeberu wa dunia lazima wajue kwamba Iran inaweza kutetea haki na maslahi popote pale dunian
 
Kuna lidada le-usi tiii linapo kwenye maandamano uko Uingereza. Mtangazaji akaliuza" ni vipi uli-react wakati hamas walipovamia Israel? "

Linajibu" Mimi sijui na sijasikia taarifa yoyote ya hamasi kuivamia Israel".

Wengi pro hamas/palestina ni tick tockers, vichwani mweupe.
 
Kuna lidada le-usi tiii linapo kwenye maandamano uko Uingereza.
Mtangazaji akaliuza" ni vipi uli-react wakati hamas walipovamia Israel?...
Screenshot_20230908-180902.png
 
Back
Top Bottom