Japo sipingani na wewe kuhusu kichapo ilichotoa Iran kwa Israel, lakini napingana na wewe katika hili swala la tetesi za Israel kuishambulia Iran.
Kiufupi hilo shambulio haliwezi kufanyika kwa sasa, unless kama ule msemo wa sikio la kufa halisikii dawa uwe unataka kujidhihirisha kupitia kwa Israel.
Netanyahu na Trump wake wanafahamu madhara makubwa waliyoyapata mwezi mmoja tu uliyopita ambapo mpaka sasa hasara yake haihesabiki. Hivyo hawatokuwa tayari kuingia katika hasara nyingine ambayo pengine safari hii inaweza kugharimu maisha ya Shetaninyahu (Netanyahu) mwenyewe.
Hapo alipo anatembea na sumu mwilini inayosemekana aliwekewa kwenye chakula na watu wenye akili kumshinda yeye na genge lake. Sasa hilo halijaisha unafikiri ataanzisha kingine?
Kinachofanyika kwa sasa ni kuanzisha taarifa hizi za taharuki, ili kujaribu kuhamisha upepo wa maandamano yanayofanyika nchini kwake, ambapo waisrael wenyewe wameshamchoka kutokana na kupenda kutumia vita kama kichaka cha kuficha ufisadi wake, na ushetani wake.
Lakini kwa Israel hii ya sasa kuishambulia Iran tena, sahau mkuu. Hakuna mtu alietegemea kile kilichotokea kwanza kingetokea. Hivyo washajifunza.