Kipigo kile alichokipata Iran mwakajana, lazima kilimpa funzo kubwa. Sidhani kama Iran itakuwa imeyahifadhi makombora yake eneo moja. Hivyo USA na Israel wanaweza kushambulia store ya makombora moja, kumbe kuna nyingine 500 hazijaguswa kabisa. Hivi ni vita vya muda mrefu, haviwezi kuwa vya wiki chache kama ilivyotarajiwa.
Advantage aliyo nayo USA, hakuna kinachoguswa kule Marekani. Inaendelea na shughuli za kiuchumi kama kawaida, inaendelea kutengeneza silaha kama kawaida, wakati Iran na Israel hazina nafasi hiyo. Israel in advantage kwa sababu mshirika wake USA anaweza kumletea silaha nyingine kukiwa na upungufu, na pia ina uhakika wa kuusimamisha uchumi wake kwa haraka kuliko Iran. Kwa Iran, hata kama vita ikiidha, madhara ya kiuchumi na kidiplomadia ni makubwa sana. Vita hii itaifanya Iran kuwa adui wa majirani zake wote, na italeta ukaribu wa Israel na mataifa jirani ya kiarabu.