IPTL running at maximum capacity, a relief to power shedding?

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Kuna taarifa kuwa kituo cha kuzalisha umeme cha IPTL ambacho kinatumia nishati ya mafuta mazito (HFO) sasa kinatembea katika full capacity (100MW) baada ya shehena ya mafuta hayo kuwasili hapa nchini mwishoni mwa juma lililopita.
Je tutarajie kuwa hii ni habari njema kwa watumiaji umeme hapa nchini...? kwamba makali ya mgawo wa umeme yatapungua au kilio cha makali ya giza kitaendelea?
 
naona umepungua kidogo, lkn wameshaagiza mara kibao, yanaisha then gizani tutarudi kama kawa. Is this sustanable? Halafu nasikia this dude is very expensive to run. lets c
 
Mtalia mkisikia aliyepewa TENDA ya kuyaleta hayo mafuta.......kijana mdogo tu....mwanasheria
 
Yap nimeona malori ya mafuta ya mmoja wa mapacha matatu yakiende huko na shehena ya mafuta ,kwanza nilifikiri huko Salasala kumegunduliwa mgodi mwingine kwani kampuni yake ya mafuta ndio imeshika tenda ya kupeleka mafuta kwenye migodi huko kanda ya ziwa ,kufa kufaana bana
 
naona umepungua kidogo, lkn wameshaagiza mara kibao, yanaisha then gizani tutarudi kama kawa. Is this sustanable? Halafu nasikia this dude is very expensive to run. lets c

Tatizo kubwa hapa ni lile lile..zimamoto. Wameagiza shehena ambayo ndio imeingia..ili kuwe na sustainability inabidi ku-forecast matumizi against shehena iliyopo then una-establish gap na muda unaotumika kufikisha shehena husika site halafu ndo unafanyia kazi. Sidhani kama wanafanya kitu cha namna hiyo.
Kwa mfano, kwa jinsi mashine zile zinavyokula mafuta na kwamba mafuta hayo hayapatikani hapa nchini nilitarajia wakati shehena hii inafika basi nyingine iwe njiani kuweza kufika hapa nchini ndani ya wiki mbili hivi, nina mashaka kwa kitu kama hiki kuwa kinafanyika.
Subirini tu mtasikia: "Makali ya mgawo yameongezeka tena kwa sababu tulipata mafuta na sasa yamekwisha, Tanzania haichimbi mafuta ni lazima tuagize nje...."

Ni kweli kuwa mafuta hayo ni gharama sana lakini kwa hali ilivyo nchini kwa sasa nadhani hakuna njia mbadala...lazima njia hiyo itumike kama dharula wakati wahusika wakiangalia njia za kudumu za kutatua tatizo hili.
Wasiwasi wangu ni kuwa dharula hii itaendelea bila wahusika kutafuta suluhu ya kudumu..huku waki-buy time kusubiri mvua zinyeshe. Zisiponyesha utasikia: "Chanzo cha mgawo wa umeme ni ukame. Serikali haina uwezo wa kufanya mvua inyeshe".
 
Mtalia mkisikia aliyepewa TENDA ya kuyaleta hayo mafuta.......kijana mdogo tu....mwanasheria

"Ndivyo nilivyolelewa, naishi kimjini mjini.., ukiniona naendesha gari la thamani si lazima liwe langu, huwa naazima"
Hahaaaaahaa...kufa kufaana nini mkuu!
Halafu ukiuliza na hiyo gharama utakuta EXAGRATION.
kufa kufaana nini mkuu!
 
Kuna taarifa kuwa kituo cha kuzalisha umeme cha IPTL ambacho kinatumia nishati ya mafuta mazito (HFO) sasa kinatembea katika full capacity (100MW) baada ya shehena ya mafuta hayo kuwasili hapa nchini mwishoni mwa juma lililopita.
Je tutarajie kuwa hii ni habari njema kwa watumiaji umeme hapa nchini...? kwamba makali ya mgawo wa umeme yatapungua au kilio cha makali ya giza kitaendelea?

tushazoea tiamaji-tiamaji.

subiri hayo majuta yakwishe.
 
Giza linatafuna uchumi wa taifa na IPTL inatafuna uchumi na uhai wa taifa. Hatuna ahueni ndivyo walivyopanga wakubwa wa nji hii.
 
Giza linatafuna uchumi wa taifa na IPTL inatafuna uchumi na uhai wa taifa. Hatuna ahueni ndivyo walivyopanga wakubwa wa nji hii.

Na bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini safari hii wanakuja na "Songosongo gas expansion project" ambapo mtarajie kupata gesi ya kutosha kuzalisha umeme wa kutosha mwishoni mwa mwaka 2013.

Wakati Pan Africa Energy wamesamehewa kodi ambayo kuanzia mwaka 2004 hadi sasa inafikia kiasi cha dola milioni 10, na wataendelea kusamehewa kwa kipindi cha miaka 25 ya uhai wa mkataba wao wa kuiuzia Tanesco gesi ya Songosongo; wao Songas wanatarajia kufanya expansion na kisha kutoza TARRIFS kubwa ikiambatana na kusamehewa kodi kwa kipindi hicho cha takriban miaka 15 kutoka sasa ambapo makadirio yanaonesha kuwa gesi itakuwa imekwisha kibiashara.

Na hapa ndipo watanzania tutalia kwa mara nyingine tena kilio cha samaki.
Subirini muone!
 
Too litle too late; danganya toto kwa ajili ya kampeni hizo!!

Back
Top Bottom