Mkuu naona unashindwa kutuletea taarifa za uhakika. Lakini taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mdau mmoja aliyepo huko IPP ni kwamba Capt Komba aliingia kwenye ofisi za Gazeti la Sema Usikike akiwa amefura kwa hasira kutokana na habari zilizoandikwa kwenye toleo la leo lenye kichwa cha habari "MAHANGA, JOHN KOMBA WAPATA PIGO MAJIMBONI
* Wananchi wawashangaa kumtetea Edward Lowassa
*Wadai kumkingia kifua kashfa ya Richmond si sawa
*Wasema safari hii watewaengua majimbo yao.
* Wadai kuwa na wabunge wa aina hiyo ni fedheha kwao
Ila nimeambiwa Capt Komba keshaondoka sasa na hali ni shwari. Hakuna taarifa zaidi iwapo walifanikiwa kuonana na huyo mhariri au la.