Ipo haja ya mitaala yetu ya elimu kuwa na somo la uzalendo

With this definition, even the head of the state is not patriotic enough.
Kwa maelezo hayo hata mtawala wetu anajikuta si mzalendo halisi.

Kabisa kabisa ndugu umeliona hilo, many people have narrow view of patriotism.
 
nimejifunza kitu apa__hatuna budi kuwakubali viongozi teule kwa haki hata kama hawakuwa chaguo letu
Kama wamechaguliwa kwa kura ya haki, Tanzania sasa hivi polisi na ccm wanaamua nani awe kiongozi hata kama wananchi hawamtaki. Uzalendo utatoka wapi bila haki kutendeka?
 
Hata ufundishe vipi, kama hakuna haki, watawala wakiendekeza upendeleo, ubinafsi na wakaishi na kutenda nje ya viapo vyao, Taifa haliwezi kuwa na wazalendo wa kweli. Zaidi utawapata wanafiki na waovu watakaojitambulisha kuwa ni wazalendo.

Mzalendo wa kweli kwa Taifa (siyo kwa serikali) ni yule anayepinga uovu katika Taifa lake, anayepinga upendeleo, anayepinga uvunjwaji wa katiba na sheria, anayepinga utawala wa kidikteta au utawala usio na maono. Je, mfumo wetu wa utawala, utaruhusu mambo hayo yafundishwe kwa watoto wetu?
 
Tz hakuna mzalendo hata mmoja
Mzalendo alikuwa nyerere tu....sahvi waliyobaki ni boshen tu

Ova
 
Tz hakuna mzalendo hata mmoja
Mzalendo alikuwa nyerere tu....sahvi waliyobaki ni boshen tu

Ova
Wazalendo wapo mkuu, ila utandawazi nao umechangia sana kuua uzalendo, ingawa wenzetu wameshaona mbali na kuanza kujihami, sio vibaya na sisi tukafanya hivyo mapema kabisa mkuu.
 
Wazalendo wapo mkuu, ila utandawazi nao umechangia sana kuua uzalendo, ingawa wenzetu wameshaona mbali na kuanza kujihami, sio vibaya na sisi tukafanya hivyo mapema kabisa mkuu.
Mzalendo pekee labda mtu kama rais wa Uruguay,mzalendo utamuona namna anavyoishi hadi hatua anazochukua
Kwa tz suala la uzalendo ni ngumu kupatikana

Ova
 
Mzalendo pekee labda mtu kama rais wa Uruguay,mzalendo utamuona namna anavyoishi hadi hatua anazochukua
Kwa tz suala la uzalendo ni ngumu kupatikana

Ova
sio sahihi sana kuhusianisha umaskini na uzalendo. nadhani kuwa active tu katika kujali maslahi ya nchi ni uzalendo tosha, regardless ya financial status.
 
Uzalendo haufundishwi, uzalendo ni jumla ya yale mambo serikali inayowafanyia wananchi wake.
Serikali ikiwa ya kibabaishaji usitegee wananchi watakua wazalendo.
 
Uzalendo haufundishwi, uzalendo ni jumla ya yale mambo serikali inayowafanyia wananchi wake.
Serikali ikiwa ya kibabaishaji usitegee wananchi watakua wazalendo.
Jumla ya mambo ambayo wananchi wanaifanyia serikali ni nini??
 
sio sahihi sana kuhusianisha umaskini na uzalendo. nadhani kuwa active tu katika kujali maslahi ya nchi ni uzalendo tosha, regardless ya financial status.
Viongozi wa tz hawajali mambo muhimu ya jamii we jiulize wanashindwaje kuweka CT scan machine wakati kila leo wananunua mashangingi tena kwa garama kubwa kuliko hizo machine....Ukienda hospital huzikuti hizo machine....hapo huoni kama kuna shida mahali

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mpaka umetoa hiyo hoja, nafikiri umeona kuna mahitaji ya watu kuwa wazalaendo au kifupi watanzania walio wengi sio wazalendo.
.
Ni nini maana ya Uzalendo?
Ili uwe mzalendo kwa nchi yako unatakiwa ufanye nini?
Kwanini Uzalendo haupo Tanzania kwa watanzania wenyewe?
Nani chanzo cha Watanzania kutokuwa wazalendo?
Unaweza kuwa mzalendo pale unapoona uzalendo haukunufaishi na familia yako bali unanufaisha kundi fulani na familia zao?.
Ni haki kuwa mzalendo kwa manufaa ya watu fulani huku wewe ukiumia?

Ushauri wangu na nionavyo.
Uzalendo ni suala ambalo huja automatically baada ya kujikuta moyoni unaipenda nchi yako.
Kuipenda nchi hakuji hivihivi kama nchi husika kupitia mifumo yake haitendi yale yatakayofanya watu wake wawe na furaha, Taifa lolote ambalo furaha ipo watu wake automacally huwa wazalendo maana mifumo hutenda yale yaliyo mema na furaha huja kama matokeo ya mema ambayo mifumo inatenda.
Uzalendo hauwezi kuja kama Zaidi ya nusu ya watu wa Taifa husika watakuwa wanahangaika kutafuta hela ya kula, kulipia ada, kulipia matibabu huku wakiona wenzao kwenye mifumo na familia zao wanamudu hivyo vitu kwa kutumia kodi za wanyonge, HAPO UZALENDO HAUWEZI KUWEPO.

UNAFIKI HAUWEZI KUWA NDIO UZALENDO.
 
Back
Top Bottom