mkuu ufahamu kitu kimoja megapixel ni ukubwa wa picha na sio quality ya picha. halafu hizi camera unazoziona zina mp 48, 64 mpaka 108 hio ni technology inaitwa quad bayer, kupata mp halisi unagawanya kwa 4, hivyo hio 64mp ni sawa na 16mp.
hebu angalia proffesional camera mfano hizi Canon mark 3/4/5 nyingi zinarange 12mp mpaka 30mp na zinauzwa mamilioni ya hela, camera tupu inaenda milioni 5 na zaidi, hivyo unafikiri kisimu cha laki 3 ama 4 sababu kina mp64 kitaishinda camera ya milioni kadhaa yenye mp 12? ukishaielewa hii logic tuangalie specification za hizi camera tutumie tu GSMArena, hakuna review ya m31 ila 64mp imetumika pia kwenye A71 tutatumia hio.
galaxy s8+
A71
angalia kwenye mlango wa hilo jengo palipoandikwa Vitosha Hall halafu utaona utofauti wa details uliopo baina ya hio 12mp na 64mp