Nimekuja na mrejesho wa Samsung A series

tiku

JF-Expert Member
Oct 31, 2015
441
244
Habari wadau niliomba ushauri hapa simu ipi bora kati ya samsung galax a 33 au a345g. Nimenunua a345g nimegundua hizi simu za a series ni infinix iliyochangamka. Sijazoea samsung za hivi jamani, sijapenda kabisa. Na ni simu original nimeipima vya vipimo vyote vya bimei, ma sensor sijui. Mliowahi kutumia S na note series afu mkatumia a series mtanielewa.
 
Habari wadau niliomba ushauri hapa simu ipi bora kati ya samsung galax a 33 au a345g . nimenunua a345g nimegundua hizi simu za a series ni infinix iliyo changamka. Sijazoea samsung za ivi jaman sijapenda kabisa. Na ni simu original nimeipima vya vipimo vyote vyabimei,ma sensor sijui. Mliowahi kutumia s na note series afu mkatumia a series mtanielewa.

Inanekana hukuwa na ufahamu wa samsung. Kama simu zingine ina madaraja.
F series, J series, A series, NOte na S series

J series (wanyonge series) hii ni kwa wale ambao uwezo wa ku afford A series ni mgumu kwao

A series ni mid range phones. So hapa hutopata quality 100%
Hapa walilenga unafuu wa bei lakini unatapa vitu vichache mno ambavyo vinapatikana kwenye flagship

S series ndio flagship edition. Hapa ndio unapata top quality
 
Inanekana hukuwa na ufahamu wa samsung. Kama simu zingine ina madaraja.
F series, J series, A series, NOte na S series

J series (wanyonge series) hii ni kwa wale ambao uwezo wa ku afford a series ni mgumu kwao

A series ni mid range phones. So hapa hutopata quality 100%
Hapa walilenga unafuu wa bei lakin unatapa vitu vichache mno ambavyo vinapatikana kwenye flagship

S series ndio flagship edition. Hapa ndio unapata top quality
Ingawa J series na Note series hazipo kwa sasa
A series sio tu midrange, zipo hadi low end kama Samsung Galaxy A03, A04e nk

Samsung Galaxy S series pia wanazo midrange mfano Samsung Galaxy S21 FE, S22 FE nk
 
Habari wadau niliomba ushauri hapa simu ipi bora kati ya samsung galax a 33 au a345g. Nimenunua a345g nimegundua hizi simu za a series ni infinix iliyochangamka. Sijazoea samsung za hivi jamani, sijapenda kabisa. Na ni simu original nimeipima vya vipimo vyote vya bimei, ma sensor sijui. Mliowahi kutumia S na note series afu mkatumia a series mtanielewa.

Sio a series zote kuna number za a series ambazo ubora wake wa kawaida
Kwa kuwa tupo 2024 nakupa a series za kiwango cha juu mfano Samsung A54 sio za pole pole katika kila series wana toa ya kiwango na ya kawaida jitahidi kufatia mambo

Habari wadau niliomba ushauri hapa simu ipi bora kati ya samsung galax a 33 au a345g. Nimenunua a345g nimegundua hizi simu za a series ni infinix iliyochangamka. Sijazoea samsung za hivi jamani, sijapenda kabisa. Na ni simu original nimeipima vya vipimo vyote vya bimei, ma sensor sijui. Mliowahi kutumia S na note series afu mkatumia a series mtanielewa.
Yani A series ulingamishe na S au Note series?
 
Zile features zote za samsung hamna iko tu kama infinix afu batton ya kuzima simu haina ukizima inakuletea vitu vingine vingi. Au nimepigwa nimeinunua 700,000. Na omba mwenye njia nyingine jinsi ya kuangalia simu original anisaidie
Matajiri mna hela za kuchezea aisee. Laki 7 nzima ukatoa hata bila kujiridhisha kama unapata kitu orijino ama la! 😳
 
Matajiri mna hela za kuchezea aisee. Laki 7 nzima ukatoa hata bila kujiridhisha kama unapata kitu orijino ama la!
Sio matajiri nimejiunga sana kununua hii simu kwanza nilikuwa nalipankwa installment. Naomba tu msaada kujua simu og na fake kwakuwa nimenunua sio mbali na ninapo ishi nairudisha tu nabadilisha maana anazo simu aina zote hizi flagship kama note 10 plus ,ana hiz aseries . naomba jinsi ya kujua simu fake na og
 
Napenda kwanza nijiridhishe kama ni fake ndo nirudishe
Na ninaendelea kugundua maajabu wala hai screen short. Afu ukiwasha haiandiki samsung galax a34 . inaandika samsung galax basi. Yele uwiiiiiiiiii!!! Nimepigwa. Japo sijadhibitisha sana. Kuna jamaa mmoja humu huwa anajua simu sana mkwawa jamaa angenisaidia ningepona .kuna kipindi pia alisha wahi kunisaidia nikagundua simu ni oj ilikuwa j7 prime
 
Back
Top Bottom