Ipi ni njia sahihi ya kugawa mali/vitu vyako vya zamani kwa ndugu, jamaa au rafiki?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

UTANGULIZI
=====
Ndugu zangu, umasikini ni kitu kibaya sana. Umasikini unakatisha uhai wa watu wengi wangali wadogo sana kwa sababu tu wameshindwa kumudu gharama za matibabu.

Umasikini ndio chanzo cha matukio mengi sana ya uhalifu kama vile udokoaji, ulevi wa kupindukia wa pombe haramu kama vile gongo pamoja na ubakaji.

Ikitokea umejikuta umezaliwa katika familia ya kimasikini, ridhika kwa hali hiyo uliyonayo kwa wakati huo kisha pambana kujikwamua. Kama wewe ni mfanyakazi, basi fanya kazi zako kwa moyo mmoja, akili pamoja na nguvu zote.

Fanya kazi usiku na mchana kama inawezekana huku ukijua fika kwamba maamuzi yako ya leo ndio matokeo ya kesho. Kama ni mwanafunzi soma sana kwa maana elimu ndio mkombozi wako. Mimi huwa ninapenda kuwaambia watoto wa mama yangu mdogo kwamba "Elimu ndio mumeo wa kwanza"

MADA KUU
=====
Ipi ni njia sahihi ya kugawa mali/vitu vyako vya zamani kwa ndugu, jamaa au rafiki? Unasubiri akuombe kwanza au wewe ndiye unayeanza kumpa?

Jenga picha mimi nilikuwa mwembamba mwaka jana 2019 ila mwaka huu kutokana na mapishi moto moto ya wifi/shemeji yenu Bushmamy (I am joking) basi kitambi kikaja. Zile nguo zangu zote zilizokuwa zinapwaya mwaka jana, mwaka huu zote zinanibana kuanzia Jersey zangu za chama la wana MAN UTD pamoja na YANGA.

TATIZO LINAANZIA HAPA
===
Ukiwa na kitu chako cha zamani kisha ukataka kumpa ndugu, jamaa au rafiki utakutana na maneno haya: "Umeniona mimi ndio masikini sana wa kunipa vitu vilivyochakaa?

Ukiwa na vitu vyako vya zamani na ukaamua kiviweka ndani kwa kuogopa kuwapa watu vitu vilivyokwisha utakutana na kadhia hii: "Mbona unarundika sana vitu vya zamani, kwani hauna ndugu uwape?"

SWALI LA MSINGI: Ipi ni njia sahihi ya kugawa mali/vitu vyako vya zamani kwa ndugu, jamaa au rafiki? Unasubiri akuombe kwanza au wewe ndiye unayeanza kumpa?

Hii story sasa imekamilika na ipo kule JAMII INTELLIGENCE: Kulikuwa na dada mmoja mrembo sana "Female Assassin" wa idara ya ujasusi ya Soviet Union almaarufu kama KGB aliwahi kuficha risasi mbili ndani ya uuke wake alipoenda kumuua mfanyabiashara mmoja maarufu sana katika hotelini huko jijini Minsk mji mkuu wa nchi ya Belarus. Mfanyabiashara huyo alikuwa amepishana kauli na serikali ya USSR mwaka 1979.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mi binafsi nimekuwa nikipewa vitu na kaka zangu bila hata kuomba! We toa tu atakaye hisi ni umaskini unaachana naye.
 
Sijui njia sahihi ila umenipa wazo la kufungua ka NGO ka kukusanya vitu ambavyo havitumiki na kugawia kaya maskini. Si ntapiga tuchenji ndugu zangu?

Mi vitu vyangu ambavyo nimegawa karibuni nimewapa marafiki. Tena wanafurahi sana. Undugu lawama.
 
Vihifadhi vizuri kwenye mfuko halafu kaviweke pembezoni mwa sehemu ya kutupia taka. Wenye kuhitaji wataokota.
 
Sijui njia sahihi ila umenipa wazo la kufungua ka NGO ka kukusanya vitu ambavyo havitumiki na kugawia kaya maskini. Si ntapiga tuchenji ndugu zangu?
Mi vitu vyangu ambavyo nimegawa karibuni nimewapa marafiki. Tena wanafurahi san. Undugu lawama
Kama unagawia masikini, hutapiga pesa, ila thawabu.
 
Kama unagawia masikini, hutapiga pesa, ila thawabu.
Nakuwa na NGO, natafuta kirikuuu. Ukiwa na nguo mbovumbovu au vitu hutumii unatupigia tunakuja kuchukua. Tutakuwa tunapita maofisi kuwamotivate mtuandalie. Sasa inabidi twende kwenye ofisi za 'mabeberu' tuwambie huu mpango watusaidie hela ya kirikuu na ya mafuta na ya ofisi na ya chai.
 
Peleka kwa watu wenye uhitaji mfano Yatima, nyumba za wazee, ukienda kijijini kusalimia etc. Nakumbuka tulipokuwa wadogo wazazi wangu walifanya hivi na kwa kweli waliopewa walishukuru sana.
 
Mimi ninachokifanyaga..huwa naziweka kwenye mfuko, naandika kakaratasi kuwa wapewe wasiojiweza nadumbukiza ndani ya mfuko, kisha naenda nauweka kwenye mlango wa kanisa.

Naamini huwa zinawafikia walengwa. Hawa ndugu zetu wa kiafrika unaweza kuwapa kitu kwa moyo mmoja wengine wakaenda hata kukurogea hizo hizo nguo zako.
 
Njia na bora na nzuri isiyokuwa na lawama ni Kanisani (nyumban za ibada pekee).

Kwa uzoefu nilionao, kwa sisi Waroman Katoliki kuna ile wakati wa kupeleka Vipaji na matoleo pale madhabauni ndio wakati mzuri wa wewe kupeleka matoleo yako.

Funga vizuri kwenye box, kisha wanapopeleka na jiunge nao.

Jana Kanisani imetangazwa pia hili jambo, kuwa sio lazima wanaotoa matoleo na vipaji wawe wahusika (Jumuiya) zilizopangiwa kufanya usafi, mtu yoyote mwenye mapenzi mema beba kipaji chako peleka.

Kanisani lina wahitaji wengi sana.
 
Kwa ndugu inafaa kuuliza, kwamba nina hiki na hiki ambavyo ningependa kuvitoa, je utahitaji?

Pia namna nyingine ni kuwatumia viongozi wa kanisa, viongozi wa mtaa au watu wanaojihusisha na masuala ya kusaidia jamii. Hawa huwafahamu watu wenye hitaji mbalimbali.

Tukumbuke kuwa asilimia kubwa ya vitu tusivyovihitaji kuna wengine wanavihitaji, tusitupe, kuchoma moto au kuviacha viharibike. Tutafute wenye uhitaji na kuwapa.
 
Mimi sio mvaa suti ila kuna kipindi nikaona ngoja nijaribu kuanza kuzivaa.So nikampata fundi mahiri kwa kipindi hicho tukashona suti 3 kwa vitambaa vizuri tofauti, fundi akafanya kazi yake na kunikabidhi.

Basi nilivozitest nikaona hazijanikaa vizuri yaani hazijanipendeza,ila kulikuwa na bro kijijini, kwa umbo lake niliamini zitamkaa vizuri,so kwenye likizo yangu nikambebea bro zile suti na nguo nyingine nyingi kadhaa ambazo zilianza kunibana.

Aisee bro alifurahi sana ila cha ajabu mke wake akamchana bro na mimi kuwa nina dharau kwa nini nimletee mume wake nguo nilizotumia mimi? Kweli iliniuma sana. Toka hapo sijawahi kurudia tena,nikiwa nazo uwa nawatafuta masela mtaani nawambia kwanza kuwa nina mzigo nawapa na wanashukuru kinoma. Kuna siku nilijisikia amani nilienda church nikakutana na msella wangu kapiga shati nililompa church nilijihisi kubarikiwa.

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Peleka kwa wahitaji na wasiojiweza hasa kanisani au masjid.
Ndugu wana lawama mno boss.

Ilishawahi nitokea nilikusanya nguo zangu kwa huruma nikampa binti fulani hg maana alikuwa na tujinguo tuchache. Nguo zilikuwa nzuri kabisa na nilimpa kwa upendo tu na si kama Nilikuwa nimezichoka au zimechakaa.

Alipoondoka maneno aliyoenda kusema sina hamu.

Tangu hapo nguo zangu zote napeleka kanisani. Hasahasa maeneo ya vyuo, huwa wana mikutano yao ya injili kila mwisho wa semester wanaenda vijinini huko, huwa wanakusanya vitu mbalimbali zikiwemo nguo na wanawapelekea wahitaji. Wale watu huwa wanashukuru mno.
 
Aise kweli kabisa, nakumbuka nilimpa dada yangu mdogo vitu vilivyotumika vya Mrs basi kuna siku alinitoa show kufa, sijarudia tena wala tena. Binadamu kwa kutoa shukrani ni majanga aise.
 
Back
Top Bottom