Ipi ni mbinu nzuri ya utatuzi wa mgogoro wa Burundi?

Uhakiki

JF-Expert Member
May 18, 2017
6,934
7,182
Leo nimefikiria sana kuhusu hali ya kisiasa nchini Burundi ambapo mgogoro umeendelea kudumu bila kupatiwa utatuzi wowote, ijapokuwa Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin William Mkapa anajitahidi kupatanisha pande zinazo pingana (chama tawala na wapinzani).Licha ya jitihada zinazofanywa na mpatanishi huyo lakini upande wa upinzani unaonekana kutokua na imani naye kwa wanacho dai kuwa anapendelea upande wa serikali (chama tawala) katika utatuzi wa mgogoro huo.Kitu ambacho ni sumu katika utatuzi wa mgogoro kama huo ambao upande dhaifu unaonekana kugandamizwa.
 
Shida moja kila chama wanataka madaraka ndio maana, mazungumzo yamekuwepo tangu siku nyingi lakini bado migogoro inafukuta...Suluhisho la kudumu sijui ni nini kwa maana kwa mfano chama tawala kikiachia madaraka inamaanisha kinakuwa pinzani na kile pinzani kinakuwa Tawala tunarudi kulekule.... Uadui na uasi huanzia hapo.. Na si unajua Sera za vyama zinakinzana?

Mimi yangu hayo, ngoja wadau wengine watoe maoni
 
Ukitaka kuujua uhondo wa ngoma ingia ucheze, tembelea Burundi kisha upata bahati ya kufika maeneneo haya Ngozi, kayanza, bubanza ( Kama sikosei) kitongoji cha cibitoke, rumonge, huko kikinuka unaweza sema ni vita ya tatu ya dunia kumbe ni ndugu wanachapana kisha wanaenda kwenye media wanatamba kisha wanaendeleza mambo yao,
 
Mkuu suala la Burundi ni zito sana na haliwezi kutatulika bila kufuata Katiba na sheria za nchi.
Jins Kulizinza alivyobadili katiba ndivyo itakavyokuwa ngumu kulitatua hili tatizo.
SULUHISHO LA HILI
Katiba ilirudishwe kama ilivyokuwa mwanzo na Kuluzinza atoke madarakani sbb muda wa kuwepo madarakani uliisha.
Vinginevyo hakuna suluhu mpaka muda wa kuwepo Kulizinza madarakani uishe.
 
Shida moja kila chama wanataka madaraka ndio maana, mazungumzo yamekuwepo tangu siku nyingi lakini bado migogoro inafukuta...Suluhisho la kudumu sijui ni nini kwa maana kwa mfano chama tawala kikiachia madaraka inamaanisha kinakuwa pinzani na kile pinzani kinakuwa Tawala tunarudi kulekule.... Uadui na uasi huanzia hapo.. Na si unajua Sera za vyama zinakinzana?

Mimi yangu hayo, ngoja wadau wengine watoe maoni
Kosa kubwa alilolifanya ni kubadili katiba na kujiongezea muda. Wanachokifanya wapinzani wapo sawa.
Watu wasianze kuwalaumu wapinzani au wananchi. Muda wa Kuluzinza uliisha kitambo sana na alichokifanya ni unyama na uroho wa madaraka.
Kuluzinza ni sawa na kipande cha mti kilicho mguuni mwa mtu. Bila kukiondoa hakuna tiba
Kuluzinza ndiyo tatizo.
Hebu fikiria, mm nilikuwa mpangaji kwenye nyumba yako, muda umeisha unataka nyumba yako, mm nagushi nyaraka za mkabata ili nikae miaka 5 bila kulipa, mahakamani na sehemu zingine nimehonga pesa. Hivi ww mwenye nyumba unaweza kunielewa mm na tukaishi kwa amani?
 
Hapana hapo amani haipo..viongozi wetu wa Afrika ni walevi wa madaraka
 
Viongozi wetu wanajisahau sana na kufananisha nchi ni kama familia yake.
Ukishajua na kuelewa kuwa nchi ni ya watu wote hapo hakuna mgogoro wala vita.
Ghadafi alisahau kuwa nchi ni wanalibya na yy akiwemo na hakuna mtu mwenye dhamana ya kuongoza milele lbd kwako tu yaan nyumbani kwako.
 
true mkuu
 
Mkuu suala la Burundi ni zito sana na haliwezi kutatulika bila kufuata Katiba na sheria za nchi.
Jins Kulizinza alivyobadili katiba ndivyo itakavyokuwa ngumu kulitatua hili tatizo.
SULUHISHO LA HILI
Katiba ilirudishwe kama ilivyokuwa mwanzo na Kuluzinza atoke madarakani sbb muda wa kuwepo madarakani uliisha.
Vinginevyo hakuna suluhu mpaka muda wa kuwepo Kulizinza madarakani uishe.
Katiba ile inayoruhusu kuongoza mihula miwili?
 
Kosa kubwa alilolifanya ni kubadili katiba na kujiongezea muda. Wanachokifanya wapinzani wapo sawa.
Watu wasianze kuwalaumu wapinzani au wananchi. Muda wa Kuluzinza uliisha kitambo sana na alichokifanya ni unyama na uroho wa madaraka.
Kuluzinza ni sawa na kipande cha mti kilicho mguuni mwa mtu. Bila kukiondoa hakuna tiba
Kuluzinza ndiyo tatizo.
Hebu fikiria, mm nilikuwa mpangaji kwenye nyumba yako, muda umeisha unataka nyumba yako, mm nagushi nyaraka za mkabata ili nikae miaka 5 bila kulipa, mahakamani na sehemu zingine nimehonga pesa. Hivi ww mwenye nyumba unaweza kunielewa mm na tukaishi kwa amani?
Kwahiyo unashauri Nkuluzinza afanyiwe umafia?
 
Viongozi wetu wanajisahau sana na kufananisha nchi ni kama familia yake.
Ukishajua na kuelewa kuwa nchi ni ya watu wote hapo hakuna mgogoro wala vita.
Ghadafi alisahau kuwa nchi ni wanalibya na yy akiwemo na hakuna mtu mwenye dhamana ya kuongoza milele lbd kwako tu yaan nyumbani kwako.
Libya wemekipata walicho kitafuta
 
Ukabila Nchi Nzima Makabila Matatu Tu Wengine Wanajiona Bora Zaidi Ya Wengine Na Huu Mgogoro Ni Wa Muda Mrefu Sana Tumezaliwa Tumeukuta Mpaka Tunazeeka Wenyewe Ni Kupinduana Tu Na Kuchapana Risasi Wakati Ni Ndugu Dawa Ni Kuwahamisha Tu Na Kuwapeleka Sehemu Nyingine Wakajichanganye Na Jamii Zingine
 
Hapana. Mihula miwili ilikuwa zamani Sasa hivi imeshachakachuliwa siyo tena mihula miwili ni zaidi.
Nikafikiri kwamba ni mgogoro wa kushindwa kutafsiri vizuri katiba. Wapinzani wanadai ameongoza mihula miwili tayari lakini chama tawala wanadai muhula wakwanza aliongoza miaka pungufu halafu muhula wapili ndio akaongoza kamilifu.Hivyo chama chake wa nataka aongeze mwingine wa tatu ili kufidia muhula wa kwanza.
 
Ameshaongezewa tayari. Na huu ndiyo muhula wake wa 3.
 
Back
Top Bottom