Klabu ya CR Belouizdad wafyekwa mishahara kisa Yanga

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,773
24,209
KISA YANGA BENCHI LA UFUNDI NA WACHEZAJI WAKATWA MISHAHARA YAO.

Baada ya kipigo kizito kutoka katika klabu ya Yanga sc, klabu ya CR Belouizdad wamekaa kikao Cha dharura kujadili juu ya matokeo mabovu ya kuchapwa mabao 4-0 na Yanga SC.

Kikao hicho kimeamua nyota wote waliohusika kwenye mchezo huo kukatwa mishahara kwa asilimia 80 pamoja na benchi la ufundi.

Pia kocha mkuu Paquetta ameamriwa kupeleka ripoti ya kila mchezaji kabla na wakati wa mchezo huo kwenye kamati ya nidhamu ya timu.

Uongozi wa timu hiyo umechukizwa sana na matokeoa hayo na kuwa na hasira na kikosi kwa kuwa waliwakodia ndege binafsi .

#FutbalPlanetUpdates

Nb: ni Yanga hiii hii ilisababisha makolo kutimuana ...Baada ya mnara

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Tusingemkosa Diara kwenye mchezo ule Yanga ingemaliza kwenye nafasi bora sana hii ligi maana timu zote ni vibonde tuu
 
Ni Yanga hii hii ndiyo inayo wasababishia mashabiki wa mbumbumbu fc, kuishi huku wakiwa hawana furaha kwa miaka minne sasa.

Ni Yanga hii hii ndiyo inayosababisha mashabiki wa mbumbumbu fc kumkataa Mwenyekiti wao Chifu Mangungu, kila timu timu inapotoa sare au kufungwa na wapinzani wao.
Kiukweli Yanga siyo watu wazuri kabisa.
 
Ukiona hivyo waliwadharau mnooo...yani hawakuamini timu ya utopolo itawafunga..hii ni dharau kubwa...
Ni kama tu na nyinyi mlivyogongwa 🖐️

Sidhani kama mlitarajia. Ila mwisho wa siku mkaingia kwenye historia iliyo tukuka.
 
Ni Yanga hii hii ndiyo inayo wasababishia mashabiki wa mbumbumbu fc, kuishi huku wakiwa hawana furaha kwa miaka minne sasa.

Ni Yanga hii hii ndiyo inayosababisha mashabiki wa mbumbumbu fc kumkataa Mwenyekiti wao Chifu Mangungu, kila timu timu inapotoa sare au kufungwa na wapinzani wao.
Kiukweli Yanga siyo watu wazuri kabisa.
Kabisa mkuu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom