Ipi kampuni nzuri ya kuagiza gari kutoka nje kati ya SBT na Befoward?

Je, na hao wanotapiliwa inakuwaje? Hebu toeni somo na hapo. Ili mtu asije akatapeliwa tena hela zake za mafao. Unaweza ukatapeliwa kupitia makampuni hayo mliyoytaja au wanaotumia online auction ndio mara nyingi huwa wanatapeliwa?
 
Je nahao wanotapiliwa inakuwaje? Hebu toeni somo na hapo. Ili mtu asije akatapeliwa tena hela zake za mafao. Unaweza ukatapeliwa kupitia makampuni hayo mliyoytaja au wanaotumia online auction ndio mara nyingi huwa wanatapeliwa?
Hayo makampuni, Beforward, SBT, Autocom, yana ofisi zao DSM. Ukiogopa kutapeliwa, basi unaenda kwenye ofisi zao kwa msaada wa karibu. Hata ukiamua ku order online, bado kuna maelekezo ya kutosha kung'amua mbinu za kitapeli, kuna documents wanakuonesha.
 
Sikuhizi be forward wamefungua Duka la spare parts pale Kariakoo yaani Kwa spare ya gari yeyote Ile utaweza kuagizia kupitia ofisini kwao na utaipata baada ya siku 30.

Hawa jamaa wapo mpaka Kwenye simu, TV,radio, computer na mashine mbalimbali sidhani Kwa Tanzania kuna kampuni ambayo most trusted kama be forward
Kariakoo sehemu gani?
 
Hapo inategemea na wewe mwenyewe unachangamka kiasi gani...

Meli ikishaondoka Japan, wanakujuza...zikiisha wiki mbili beforward wanakutumia documents zote za gari kutoka huko Japan kwa kupia DHL au shirika lingine watakalopenda wao.

Ukishapokea hizo docs inakuwa zimebaki wiki mbili meli ifike Dar...hizo wiki mbili ndiyo unazitumia kuchakarika kulipia kodi zote stahiki huko TRA ili meli ikifika unakuwa umeshakamilisha malipo yako karibu yote..

Meli ikifika inatakiwa utoe gari ndani ya siku saba, zaidi ya hapo utakuwa unatozwa gharama ya gari kukaa bandarini kila siku...(penalty after grace period).

Mara nyingi ukiwa umeshakamilisha malipo ndani ya zile wiki mbili kabla ya meli kuwasili, Meli ikifika tu unaweza kulipata gari lako ndani ya siku mbli mpaka nne at most.

Kuhusu bima, ukishafanya registration ya gari TRA na kupewa plate number na kadi, hapo unaweza kwenda na kadi ya gari kulipia bima...coz gari likishakubaliwa kutoka bandarini ina maana limekamilika usajili wake....na polisi wana haki ya kukupiga faini kama huna bima..

Sent using Jamii Forums mobile app
Iko vizuri
 
Befoward ni mapaka pori niliagiza nao gari ikawa bomu wakakataa kuwa liable na wanajinasibu kuwa wanafanya ukaguzi (inspection) ya nguvu hukohuko kiufupi wale ni mbwa mwitu kabisa , Tumia Tradecarview sikuhizi wanajiita TCV hao jamaa hutajutia
 
Achana na mahangaiko, ingia trade car view... ambao sahiv wanaitwa TCV..
Hawa jamaa gari zao vinanda, na unapata nafas ya kulia kupunguziwa beii kama upo mtaa wa congo unanunua madela.
 
Befoward ni mapaka pori niliagiza nao gari ikawa bomu wakakataa kuwa liable na wanajinasibu kuwa wanafanya ukaguzi (inspection) ya nguvu hukohuko kiufupi wale ni mbwa mwitu kabisa , Tumia Tradecarview sikuhizi wanajiita TCV hao jamaa hutajutia
Declare ur interest.
 
TCV na Bei zao za kubumba'
 
Back
Top Bottom