Ipi flat screen bora kati ya matoleo haya?

Ushauri wa bure ...
Msipende kununua Tv za kampuni zenye majina makubwa kama SONY, SAMSUNG au LG kwani asilimia kubwa ni copy na sio ORIGINAL .
Ni bora kununua tv ya kichina halisi kutoka kwenye kampuni husika kuliko kununua copy ya Kampuni kubwa . Mfano huwez kukuta copy ya Star-X au arboder au TCL.
Kwa ushauri pia ukitaka tv imara na hutojutia nunua TCL hizi ni tv imara sana na ninayangu inatumika 24 hrs mwaka wa pili sasa haimjui fundi licha ya misukosuko ya short ya umeme lakini bado ipo safi. Picha clear kabisa 1080 au 720 resolution safi kabisa . Nunua TCL mkuu
Huu ushauri sio sahihi,ushauri sahihi ungesema watu waende kwa dealers au uwaelekeze jinsi ya kujua tv fake na original lakin sio waache kununua brand kubwa kisa watapigwa copy
 
LG,SAMSUNG,SONY BRAVIA, HISENSE na TCL , nje ya hapo mkuu mimi sinunui yaani bora hata ninunue 24 inches ya brands hizo kuliko hayo majina inch 50
Dah nihisi TV zilikuwa zile za kichogo tu. Kichogo ukiamka tu unaiwasha unakumbuka kuizima usiku wakati wa kulala, lakini nikatumbukia kwenye flat Screen (Sony Bravia) ndani ya miezi 3 tu haiwezi kukaa on masaa matatu manne mfululizo, lazima ijizime. Lol!
 
Na mimi nimegundua kitu cha namna hiyo ingawa yangu sio Sony. Nilijaribu kugoogle imeelezwa kuwa ni kitu cha kawaida ni kama inajiregulate umeme wake. Labda kuna namna ya kubadili hilo kwenye settings ila TV haina ubovu.
 
Habarini, naomba kujuzwa katika hizi flat screen za wananchi wa kipato cha kawaida, ni ipi bora kuliko zingine?

-Star-X tv
-Aborder tv
-Sundar tv

Hapa siongelei zile za kibosile kama Sony, LG na Samsung.
startimes wana flat nzuri sana
 
Nilinunua mwaka 2015 32" nimekuja kuiuza mwaka huu mwanzoni ikiwa haina tatizo lolote.
Nampango nikachukue brand hiyo hiyo. Kwanza napenda muundo wao wa kuweka base (stand) katikati. Sipendi tv zenye miguu huku na huku kama masikio ya popo.
Hah ha,Kama popo kweli
 
Kiukweli inategemea hizo brand kubwa unanunua sehem gan na umakini wako pia.....me ni mpenzi sana wa sony kuanzia tv had mziki.......nna sony bravia tv ni mwaka wa saba sasa haijawahi kuzingua zaid ya kubadili remote tu madogo wakipasua.......nikitaka kununua huwa naenda kwa agent kabisa wa sony garantee 2years
Na Sony sija wahi ona fake zote ni ngangali
 
Mkuu mm naishi mwanza. Iyo biashara ya kupitia tunduma imekaaje. Nieleze kidogo nipate ufahamu, maana sipo vizuri kwenye huu uwanda wa kuagiza vitu kwa cost benefit analysis
Hamna Samsung 43" OG Kwa laki 450! Labda iwe ya wizi..Ukitaka kujua ni OG angalia model namba yake alafu goole
 
startimes wana flat nzuri sana
Nilinunuaga tv ya startimes 32 inch ile yenye king'amuzi ndani mwaka 2011. Nilikaa na ile tv jamani mpaka nikachoka. 2015 nikafungua bar nikaihamishia huko, imesota huko mpaka nimekuja kufunga ile bar. Kwenye 2018 hivi nikampa mdogo wangu alikua anaanza maisha nae kakaa nayo mpaka kakata tamaa, mwisho nae kaipeleka kijijini baada ya kununua tv kubwa. Huko kijijini nako inaendelea kupasua anga mpaka waleo.
 
Tv ni utuzaji wako tu. Ukiifunga ukutani na ikatulia vizuri bila kubuguziwa itakaa muda mrefu tu. Mimi nilikaa na star X 24’ miaka mitano hadi nilipoiuza na kununua 43.
 
Una budget gani na unataka sifa gani? Man jipinde 500k uchukue LG au Samsung HD 32" mkataba izo.

Ulizotaja hapo dah.
Mimi nilinunua LG tena kwa bei kubwa. Ilikufa baada ya mwaka mmoja. Yaani waranty iliisha wiki hii yenyewe ikafa next Week. Iliniuma sana maana niliweka pesa nyingi pale.

Nikajiapia next time sitanunua TV ya bei ghali. Nitanunua ya bei ya kawaida ili hata ikifa nisipate hasara.

Baada ya hapo nikanunua Aborder. Nashukuru mpaka leo haijasumbua. Hata ikiharibika asubuhi tu jioni nanunua nyingine coz it is cheap.
 
Back
Top Bottom