Baada yakurejea ios vitu pekee ninavi miss sana kwenye Android ni kuforce simu ishike 2g au 3g
Kwenye ios hata uselect nini simu itakamata penye signal kubwa
Ukiwa mbali kidogo tu na mnara iphone inasoma edge na hakuna namna unaweza fanya
Lakini kwenye Adroid ukiselect 3g only itakamata hata kama signal ipo chini
Kingine ni ku clear app data bila kui unstall app husika
Kwenye Android unaweza kuclear data ya za app bila shida
Kwenye ios kuna kui delete app na data zake au kudelete app na kuacha data zake
Telegram ina kama gb 10 na sijui nnitaclear vipi
Sms report nayo hakuna kwenye ios kujua kama muhusika amepokea sms yako
So inawezekana mimi ndio sijajua namna ya kufanya, mwenye uzoefu toa maoni yako
Iphone 8 mini, ios 14.3