Mkuu ni watu wachache sana wenye iphone na wakajua unayojua wewe, wengi tunajua kuchomeka line na kuitumia kama ilivyo, na wenye nazo wapo wachache sio kama wenye sumsung
Sumsung kila mtu ni mtaalamu maana asipoikuta android kwenye sumsung ataikuta kwenye simu nyingine kibao hadi za wachina
Nimekuta na watu wengi hata kuweka tu mp3 kwenye iphone hadi anunue itune maana apple wameweka discouragement kibao kwenye device zao ili mtumiaji anunue badala ya kuingiza kwa njia zingine
Mimi ninacho kimeo changu 3gs ilinichukua muda kweli kuja kugundua kuwa naweza kupata apps zaidi ya kununua app store, sipati picha sista duu au washkaji wasiokuwa interested na tech kama anamuda wa kutafuta sijui atapata wapi cracked app zaidi ya kukimbilia apps store
Kwa sumsung hali ni tofauti kabisa,
Na ndio maana tz watu wengi sana wanaona bidhaa za apple ni kama anasa kuanzia simu pad na kopyuta zao
watu wamekomaa na windows na android tu, simple to get, easy to use, freedom