Investors Reach .Serikali inajua Kampuni hii inawaibia wananchi wake Maskini?

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,505
Moja ya sehemu ambayo kumekuwa kukifanyika sana ufisadi kwa watanzania ni sehemu za Kazi. Kupitia Makampuni haya ya Recruitment na Pia Makampuni kadhaa ambayo yamekuwa yakitumia umaskini wa Watanzania kuwanyonya na kuwakandamiza. Kuna Makampuni Ya Recruitment ambayo yamekuwa yakiwanyonya wafanyakazi na kuwakamua mpaka tone la mwisho la damu. Nakumbuka Kampuni moja iliyokuwa inawa recruit wafanyakazi wa Tigo siku za nyuma hi ilikuwa inachukua pesa nyingi sana toka kwa wafanyakazi hawa na kuwalipa kidogo sana. Ikichukua pesa zao za likizo na Overtime pia. ilikuwa imeaajiri wafanyakazi wengi toka Kenya.

Sasa Kuna Kampuni inaitwa INVESTORS REACH. hii imekuja na utaratibu mwingine wa pekee kuwa watu wanaambiwa wamekuwa shortlisted then wanaambia maneno mengi kadhaa wa kadhaa na baadaye wanaambiwa kuwa wachangie tsh 9,500/= kwenda kwenye namba hii ya tigo 0653883618 . wanadai pesa hii ni ya
1.ada ya consultation
2. kifungua kinywa kwa watahiniwa wote
3. allowances kwa Watahini wataoenda Mikoa yote Nchini. hivyo wametangaza mikoa yote mikubwa nchini kuwa na vituo vya kuwafanyia watu interviews.

swali najiuliza hivi kama wameomba kazi watu 10,000. kutokana na nafasi nyingi kutangazwa na ukosefu wa ajira uliolikumba Taifa. je watakuwa na tsh ngapi? Tsh 95,000,000 au nusu yake tu. Je ni Tsh ngapi? Huu ni wizi Serikali ifatilie jambo hili kama ni halali basi tutangaziwe.
 

Attachments

  • Screenshot_2016-07-19-09-20-28.png
    Screenshot_2016-07-19-09-20-28.png
    56.3 KB · Views: 37
Back
Top Bottom