🧠 Intuition vs Reasoning: Ipi Inapaswa Kuongoza?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
19,408
Reaction score
45,799
Hello wana great thinkers 🧠

Blue Monday ✍️

Je, tunapaswa kuamini intuition yetu ya ndani bila kutumia reasoning?

Yaani ile umekaa tu pap... ukapata sauti au msukumo wa ndani unaokuambia usifanye jambo fulani halafu ukaamua kuitii bila kwanza kufikiria kwa kina na kuchambua sababu?

Umewahi kukutwa na hali kama hiyo?

Hebu tuzogoe tunapaswa kuitii kila sauti ya ndani bila kufanya reasoning?

Ni mara ngapi umeipuuza sauti yako ya ndani halafu baadaye ukajikuta kwenye matatizo?

Na ni mara ngapi umeisikiliza intuition yako, ukaacha kutumia reasoning, lakini baadaye ukajikuta kwenye matatizo makubwa zaidi?

Hebu tujiulize pamoja 👇

Kipi kina nguvu zaidi kati ya intuition na reasoning?

Je, hivi vitu viwili vinaweza kufanya kazi kwa wakati mmoja?

Au vinafanya kazi pamoja
Ila hatutambui?

Na kama vinaweza, unawezaje kutumia intuition na reasoning kwa pamoja ili kufanya uamuzi bora zaidi?

Pia mtu mwenye uelewa
Atuambie nini maana ya intuition kwa kina
Na nini maana ya reasoning kwa kina

Maoni yangu kidogo kuhusu mada :

Mimi binafsi ni mara kadhaa nimepuuza sauti ya ndani na kuanza kutumia reasoning pekee ambayo sasa sielewi nakua nashindwa kufanya uchambuzi kwa kina au kwa usahihi na kujikuta nimefanya makosa then baadae nagundua huenda ningetumia vyote the same time lakini inakua too late

So mimi naamini kutumia reasoning ni bora sana bila kupuuza intuition yako

Karibu kwenye Chemsha Bongo



ShesRise_1. 🧠 ✋️
 
Hivi vitu viwili vinafanya kazi kiutofauti kidogo kutokana na experience yako kwenye maisha (huwa nasema mara nyingi i do believe life is collection of an experience).

Hivyo basi Intuition recognition from past experiences.

Reasoning uses the opening logics, rules and facts as my name(past and future).
 
Watu wengi hapa watakwambia reasoning but trust me, reasons zinatokana na experience yako katika maisha haya tangu umezaliwa hadi leo so always inabase kwenye uzoefu ila sauti ya ndani ni sauti halisi coz ni kitu ambacho kimekuja bila hata kukiplan na wala huwezi elezea ila unajikuta tu nafsi or whatever inakua nzito kwenye kutenda jambo au inakushawishi utende jambo fulani ambalo hata hukuwa unaliwaza.

So sauti ya ndani ndio sauti halisi na ndio sauti ambayo kimsingi unatakiwa uizingatie sana coz ndio pekee inayokuunganisha na nature.
 
Asante kwa maoni mkuu
Umesema vinafanya kazi kiutofauti

Lakini je vinaweza kutumika kwa pamoja ili kuleta matokeo bora zaidi?
 
Sawa je unapaswa kuamini kila kitu sauti yako ya ndani inachokuambia bila kutumia reasoning?
 
Wataalamu wa neuroscience wanathibitisha kuwa hisia na akili vinapaswa kutumika kwa pamoja kwenye kufanya maamuzi.

Asilimia kubwa watu wengi huishia kwenye intuition bila kufanya reasoning. Binafsi nadhani logic inapaswa kutumika kuverify intuition.

Hatuwezi kuziseparate lakini reasoning inapaswa kuwa the main approver
 
Binafsi kwa % kubwa intuition yangu inakuja na confirmation ya nilichokuwa nakiwaza

Ningekuwa mtu wa dini sana ningekuwa nasema naongozwa na roho mtakatifu
Nje ya mada au tufungue kanisa tupige hela bro 😅

Ndani ya mada
Sauti ya ndani mimi nimeupuuza mara kadhaa na kuishia kukosea

Ndio maana nauliza wadau
Je intuition na reasoning ni kipi kitangulie au vinafanya kazi kwa pamoja
 
Ni kweli reasoning inatokan na experiences and prior memories zilizopo kwenye akili ya mtu tiyari.

Lakini reasoning ndio engine ya maamuzi kwa mwanadamu, mtu anayeishia kufanya maamuzi based on intuition bila kushirikisha reasoning an nafasi kubwa kufanya maamuzi kutokana na huruka, hasira, au mawazo potoshi nk
 
Asante sana mkuu
Na ndio maana na mimi nikasema
Intuition pekee haiwezi kua sahihi kwa sababu sio kila sauti inakua nzuri zingine ni negative so bila kutumia reasoning unajikuta umekosea

Kwahiyo naunga mkono reasoning sawa lakini bila kupuuza intuition

Hivi vitu vikiwa pamoja ndio mtu hupata matokeo bora zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…