... Nilikuwa nao mwanzoni mwa wiki hii. Bei ni sh Laki 3. unatoa Alfu 60 unapewa solar panel ndogo, radio 1 ndogo ya solar, taa 2 na tochi vya solar na charger inayoweza kuchaji simu 4 kwa wakati mmoja. unatumi kwa siku 14 kisha baada ya hapo unaanza kulipia sh Alfu 1 kila siku kupitia mpesa hadi utakapomaliza deni la laki 240. ukiacha kulipia siku 2 jamaa wana uwezo wa kufunga acc yako kutoka ofsini kwao usipate huduma yoyote. guarantee ya vifaa hivi ni miaka 2. haya ndio maelezo niliyoyapata kutoka kwa wakala wa kampuni hiyo hapa mbezi mwisho. cha kuzingatia hapa ni kuwa mashine hii ya solar ina ukubwa wa laptop tu na sio ya kuweka juu bati bali unaiweka tu nje kwenye jua, unachaji simu zako na kusikiliza redio na giza likiingia unaingia nayo ndani.