Hivi ni nani alotudanganya kuwa wasiwasi ndio akili? Sio kweli, udadisi ndio akili

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,071
Unataka kuwa na akili?

Tena kimsingi sio kutaka kuwa na akili, bali ni je? Unataka kuzitumia akili ambazo tayari unazo?

Na je Unataka mwanao aweze kutumia akili alizojaaliwa kwa kuzaliwa tu akiwa Homo sapiens a wise humanoid?

Je unataka awe mwenye uwezo wa kujifunza?

boy-311392_1280.png

Ni kweli matumizi akili ya mtu hutegemea baiolojia na mazingira anayokulia. Lakini chukulia kwamba kibaiolojia wooote tumezaliwa na Homo sapiens hivyo akili tayari tunazo kwa urithi wa ubinadamu wetu.

Kinachobaki kututofautisha ni kiwango cha matumizi kitakachotegemea saana mazingira ya mtoto na mtoto, mtu na mtu.

Kuna vitu unaweza kuviandaa ili kumfanya mwanao atumie akili yake zaidi ikisaidiwa na hisia, machale sijui bahati. Vyote atatumia lakini akili ndio itawale maisha yake.

Can you inspire your childs inner genius?
exam-2410373_1280.png

Katika kupima ukweli wa jambo na ushikamanifu wake tunaweza kutumia vijiukweli vilivyokwisha kuaminika tayari (well established facts)

Kanuni ni moja tu visipingane. Na hata visipopingana sio lazima vikubaliane, bali yatosha tu hata vioane.

Kuna kauli mbili au tatu ninazozifahamu kuhusiana na akili; moja inasema 'wasiwasi ndo akili'; na kuna kauli ya pili inasema 'kuuliza si ujinga'. Ya tatu yenyewe ni ya kisukuma inasema 'masala kulangwa'

Tukizichambua zaidi kauli hizi kwa upande wa wasiwasi. Wasiwasi imekaribiana zaidi na hofu kuliko akili. Imekaribiana zaidi na hisia na silika kuliko hekima. Hivyo basi kama utamlea mtoto katika misingi ya awe na wasiwasi (aogope) vitu fulani basi jua unamtengeneza mwanadamu wa chini zaidi (kama mu Homo erectus tu) atakayetumia silika na hofu kuyakimbia mambo mabaya ili asipotezwe maisha (survival). Hii ni kwa wazazi wenye imani ya wasiwasi ndio akili. Huwezi pata jiniazi hapo, hawapo 'smart' hata wao wenyewe.

Kauli ya pili ambayo nayo sijaipenda sana, hapana nimeipenda nusu ( kikamilifu baada ya kuiweka sawa) ni hii; KUULIZA SI UJINGA.

Sijataka kuifafanua kabla sijairekebisha maana ipo hasi sana. Basi tuweke kisawe na kinyume cha neno moja ili tupate kauli ilonyooka zaidi:
Udadisi ni kisawe cha kuuliza na akili ni kinyume cha huo ujinga. Hivyo badala ya kusema 'kuuliza si ujinga' tutasema 'udadisi ndo akili'

Katika kuishi kwangu nimegundua kuwa 'vitu' hivi vitatu mtu huwa havimiliki kama tunavyomiliki nyumba au kompyuta. Maana kiukweli hizi ni hali na sio vitu 'per se';
Utajiri
Akili na
Afya

Tunasema mtu mwenye afya, lakini kumbe kiukweli ni yule mtu ambaye kila siku anafanya mambo ya kuitafuta afya. Atafanya mazoezi, atakula vizuri, usafi na atapumzisha mwili wake. Kila siku anaijenga afya yake na ndio anakuwa mwenye afya🤔. Siku anapoacha kujijenga kiafya ndipo anapogonjeka.

Tunasema mtu mwenye utajiri na kumbe utajiri ni ile hali endelevu ya kutafuta na kuwekeza kwenye mali. Siku anapoacha kutafuta (hata 'passively') ndipo anapofilisika!!

Basi ndugu zangu hata akili nayo ni hivyohivyo. Mtu anayeitwa ni mwenye akili kiulweli sio kwamba tu basi kiajabu amekuwa na vitu/'materials' vingi kichwani. La. Ukweli ni kwamba ni tabia yake ya kila siku kujifunza vitu mbalimbali. Karibu kila uzoefu anaopitia maishani anautumia kujifunza. Muda mwingine anajifunza hadi vitu vya ziada kabisa. Na mwishowe anaweza kuunganisha funzo la hapa na la pale na akapata kitu kipya kabisa!. Udadisi, huo utafutaji wa maarifa ndio akili yenyewe. Mmeelewa sasa?

Huu ndio uzoefu wangu mimi na haya ni majibu ya swali linaloulizwa. Kwamba mtu anafanyeje hadi anakuwa na akili? Jibu ni sawa katika kipengele cha afya na hata kile cha utajiri.

Kwa wazazi wenye watoto angalizo;
Udadisi unapatikana penye utulivu
Udadisi unapatikana penye amani
Udadisi unasisimuliwa na vitu asili vya kuvutia na kushangaza.

Peleka mtoto kwenye shule yenye mazingira mazuri. Watoto wa mashuleni wafanye tour zitakazosisimua udadisi iwe ni kwa wanyama, au viwandani huko. Viwandani iwe ni kwa ajili ya kukata kiu ya udadisi wa 'hivi gari zinaundwaje?', mabati na nondo au karatasi zinaundwaje? Sio tu za twende kiwanda cha soda na mikate kunywa soda. Ujinga huu ukome. Mtoto aende kujibu swali la hivi soda na mikate vinatengenezwaje. Waalimu mnaweza kuileverage hii penda tamtamu ya watoto ili kuwaongeza udadisi. Mfano unanunua vifaa wanaenda kiwandani kujifunza recipe halafu mnakuja darasani mnatengeneza keki, mikate na soda mnakunywa wote.

Tengeneza mazingira ya mtoto kuona maua na wadudu mbalimbali, wanyama eeh! Kiufupi tengeneza ka 'Edeni' nyumbani kwako.

Badili 'approach' ya ukali na mafokeo kuwa uthabiti na maelekezo. Ukali unasisimua uoga tu unazalisha li Homo erectus. Lakini pia maelekezo yanazalisha skilled workers tu unazalisha li Homo habils. Ili uzalishe ka jiniazi kenye hekima hebu karuhusu kajaribu, kabebe majukumu na katatue matatizo madogomadogo ukisaidia knowledge za hapa na pale. Kakiweza kuharmonize knowledge unayokapatia hapo umepata a leader, a thinking man a Homo sapiens indeed.

Kiufupi mazingira yawe ni yanayomruhusu mtoto mwenyewe kujifunza maana msemo wa tatu unaojazia na kufunga ni 'Masala Kulangwa' yaani akili ni kufundishwa/kujifunza zaidi na zaidi.

Nb: mniwie radhi nimeandikaa mwisho nikachoka sikuwa na muda tena wa kuiperfect lugha. Pambaneni tumieni akili zenu maana mnazo tele
 
Wasiwasi ndio akili yenyewe. Kama huna akili huwezi kuwa na wasiwasi
Sawa ni akili japo ya kiwango cha kuanzia (chini)

Ng'ombe akisikia sauti ya simba au risasi hutahayari na taharuki kwa wasiwasi kibao.

Wasiwasi ni akili ya kiwango cha chini, kiwango cha silika tu za wanyama. Nani anapenda kuishia hapo. Hapa kiumbe atasavaivu.🤕

Udadisi ndio huleta hekima ya kibinadamu, kwa kujiuliza maswali ya nimesikia sauti hii je nifanyeje?. Utashi huhusika hapa. Hapa kiumbe ataishi.😊

Kiufupi tu, ng'ombe akitumia wasiwasi atakimbia au kuzimia tu lakini akiweza kutumia udadisi ataweza hata kutengeneza 'bulletproof zizi la ngombee🤯😂😂.' Ili mambo ya marisasi na ma simba yasimsumbue tena
 
Je wewe ni nani aliokuambia akili ipo ya aina moja TU?
Kwa kifupi hoja isemayo:-
-Wasiwasi ndio akili ni sahihi,pia hoja Yako ya udadisi ndio akili nayo ni sawa.
Sasa akili haiishii hapo kwa vitu viwili TU vinawndelea kulingana na uhitaji wa mtu.
Mfano wa hoja nyingine za akili ni kama:-

Mashaka ndio akili,
Kufikiria kwa kina ndio akili,
Kuchunguza kwa undani ndio akili,
Kufuatilia kwa kina ndio akili,
Nakdhalikanakadhalika.

Maana yake,
Wasiwasi ni kutokuamini jambo Fulani,inapelekea kufanya upelelezi.

Udadisi ni kutaka kujua zaidi inapelekea ugunduzi.

Mashaka inapelekea kufanya uchunguzi zaidi,

Kuchunguza kitu Kwa undani hii ni akili ya ugunduzi na vumbuzi.

Kwa kifupi hapa Kuna ujasusi,utafiti,ugunduzi na uvumbuzi.
Kama mtu hafanyi hayo huyo huna akili.
Ingawa Kuna mengine yanaendelea.

Nimeandika hivyo kwa ajili ya kukukosoa kwenye wasiwasi, na kukuunga mkono kwenye udadisi.
Lakini NAMI nimeongeza hoja zangu kua matendo ya akili hayaishii hapo TU kwenye udadisi na wasiwasi.
 
Aiseeee
Yaani nilipo maliza tu kusoma bandiko la mtoa mada hichi ulicho andika ndio kilinijia akili mwangu pia

Umedadafua vizuri
 
Katika akili kuna hili suala pia la attention span, yaani muda ambao mtu anaweza kutilia mkazo jambo moja lililo mezani.

Mfano mtu anawaza kuhusu mpira;

- Mwenye attention span ndogo atawaza ni wa duara na una rangi ya madoa ova.

-Anayefuata atawazia: ni wa duara, una rangi ya madoa na ndani una upepo ova!

- Anayefuatia kwa attention span kubwa atawazia: ni wa duara, una rangi za madoa, una upepo ndani lakini wamewekaje upepo kwenye plastiki? Anagundua ndani ni mpira/rubber elastic na nje ni plastiki ili kuruhusu kutanuka na kusinyaa ndani na kuruhusu kuoakwa rangi na madoa nje. Huyu ndiye ana attention span kubwa zaidi.

Utaona kwamba mwenye attention span kubwa ndiye anayeweza kufikia hatua ya kuleta mbadala wa mpira labda, hata akaboresha rangi. Kiufupi huyu ndiye mdadisi kuliko wote na ndiye tunayeweza kumuita jiniazi (wa masuala ya mpira)

Unaweza kupima akili ya watu hata kwa kuangalia namna wanavyochambua taarifa. Je anatulia anaupata ukweli kamili au anarukaruka tu na vipande vya ukweli kila mahala. A jargon of everything master of none😕!?

Japo kuwa makini maana kupitiliza kwa uoande wowote ni tatizo, maana huko utakutana na matatizo ya Autism na ADHD. Kiufupi wajengee watoto mazingira ya kutumia uwezo wote: uwezo wa kukazia (focus) na uwezo wa kupuuziapuuzia kunyapianyapia.

By the way Udadisi ndo Akili✌
 
Katika akili kuna hili suala pia la attention span, yaani muda ambao mtu anaweza kutilia mkazo jambo moja lililo mezani.

Mfano mtu anawaza kuhusu mpira;

- Mwenye attention span ndogo atawaza ni wa duara na una rangi ya madoa ova.

-Anayefuata atawazia: ni wa duara, una rangi ya madoa na ndani una upepo ova!

- Anayefuatia kwa attention span kubwa atawazia: ni wa duara, una rangi za madoa, una upepo ndani lakini wamewekaje upepo kwenye plastiki? Anagundua ndani ni mpira/rubber elastic na nje ni plastiki ili kuruhusu kutanuka na kusinyaa ndani na kuruhusu kuoakwa rangi na madoa nje. Huyu ndiye ana attention span kubwa zaidi.

Utaona kwamba mwenye attention span kubwa ndiye anayeweza kufikia hatua ya kuleta mbadala wa mpira labda, hata akaboresha rangi. Kiufupi huyu ndiye mdadisi kuliko wote na ndiye tunayeweza kumuita jiniazi (wa masuala ya mpira)

Unaweza kupima akili ya watu hata kwa kuangalia namna wanavyochambua taarifa. Je anatulia anaupata ukweli kamili au anarukaruka tu na vipande vya ukweli kila mahala. A jargon of everything master of none!?

Japo kuwa makini maana kupitiliza kwa uoande wowote ni tatizo, maana huko utakutana na matatizo ya Autism na ADHD. Kiufupi wajengee watoto mazingira ya kutumia uwezo wote: uwezo wa kukazia (focus) na uwezo wa kupuuziapuuzia kunyapianyapia.

By the way Udadisi ndo Akili
Mimi ni mdadisi kupitiliza, nafocus na jambo moja kwa kina,, utata huja kwenye imagination huwa ni kubwa kiasi kwamba nachimba jambo kwa undani sanaa,, inanisaidia kwenye mambo mbali mbali lakini inanitesa kwenye angle nyingi vile vile.
 
Hakika, kuna mambo inafaa na kuna mambo inakukata.

Hapo kizuri ni kuhakikisha unafanya kazi yenye kutumia zaidi huo uwezo wako.

Na kwa mambo mengine unadelegate unatumia akili ya watu wengine inapobidi.
 
Unataka kuwa na akili?

Tena kimsingi sio kutaka kuwa na akili, bali ni je? Unataka kuzitumia akili ambazo tayari unazo?

Na je Unataka mwanao aweze kutumia akili alizojaaliwa kwa kuzaliwa tu akiwa Homo sapiens a wise humanoid?

Je unataka awe mwenye uwezo wa kujifunza?

View attachment 2798696

Ni kweli matumizi akili ya mtu hutegemea baiolojia na mazingira anayokulia. Lakini chukulia kwamba kibaiolojia wooote tumezaliwa na Homo sapiens hivyo akili tayari tunazo kwa urithi wa ubinadamu wetu.

Kinachobaki kututofautisha ni kiwango cha matumizi kitakachotegemea saana mazingira ya mtoto na mtoto, mtu na mtu.

Kuna vitu unaweza kuviandaa ili kumfanya mwanao atumie akili yake zaidi ikisaidiwa na hisia, machale sijui bahati. Vyote atatumia lakini akili ndio itawale maisha yake.

Can you inspire your childs inner genius?
View attachment 2798698
Katika kupima ukweli wa jambo na ushikamanifu wake tunaweza kutumia vijiukweli vilivyokwisha kuaminika tayari (well established facts)

Kanuni ni moja tu visipingane. Na hata visipopingana sio lazima vikubaliane, bali yatosha tu hata vioane.

Kuna kauli mbili au tatu ninazozifahamu kuhusiana na akili; moja inasema 'wasiwasi ndo akili'; na kuna kauli ya pili inasema 'kuuliza si ujinga'. Ya tatu yenyewe ni ya kisukuma inasema 'masala kulangwa'

Tukizichambua zaidi kauli hizi kwa upande wa wasiwasi. Wasiwasi imekaribiana zaidi na hofu kuliko akili. Imekaribiana zaidi na hisia na silika kuliko hekima. Hivyo basi kama utamlea mtoto katika misingi ya awe na wasiwasi (aogope) vitu fulani basi jua unamtengeneza mwanadamu wa chini zaidi (kama mu Homo erectus tu) atakayetumia silika na hofu kuyakimbia mambo mabaya ili asipotezwe maisha (survival). Hii ni kwa wazazi wenye imani ya wasiwasi ndio akili. Huwezi pata jiniazi hapo, hawapo 'smart' hata wao wenyewe.

Kauli ya pili ambayo nayo sijaipenda sana, hapana nimeipenda nusu ( kikamilifu baada ya kuiweka sawa) ni hii; KUULIZA SI UJINGA.

Sijataka kuifafanua kabla sijairekebisha maana ipo hasi sana. Basi tuweke kisawe na kinyume cha neno moja ili tupate kauli ilonyooka zaidi:
Udadisi ni kisawe cha kuuliza na akili ni kinyume cha huo ujinga. Hivyo badala ya kusema 'kuuliza si ujinga' tutasema 'udadisi ndo akili'

Katika kuishi kwangu nimegundua kuwa 'vitu' hivi vitatu mtu huwa havimiliki kama tunavyomiliki nyumba au kompyuta. Maana kiukweli hizi ni hali na sio vitu 'per se';
Utajiri
Akili na
Afya

Tunasema mtu mwenye afya, lakini kumbe kiukweli ni yule mtu ambaye kila siku anafanya mambo ya kuitafuta afya. Atafanya mazoezi, atakula vizuri, usafi na atapumzisha mwili wake. Kila siku anaijenga afya yake na ndio anakuwa mwenye afya🤔. Siku anapoacha kujijenga kiafya ndipo anapogonjeka.

Tunasema mtu mwenye utajiri na kumbe utajiri ni ile hali endelevu ya kutafuta na kuwekeza kwenye mali. Siku anapoacha kutafuta (hata 'passively') ndipo anapofilisika!!

Basi ndugu zangu hata akili nayo ni hivyohivyo. Mtu anayeitwa ni mwenye akili kiulweli sio kwamba tu basi kiajabu amekuwa na vitu/'materials' vingi kichwani. La. Ukweli ni kwamba ni tabia yake ya kila siku kujifunza vitu mbalimbali. Karibu kila uzoefu anaopitia maishani anautumia kujifunza. Muda mwingine anajifunza hadi vitu vya ziada kabisa. Na mwishowe anaweza kuunganisha funzo la hapa na la pale na akapata kitu kipya kabisa!. Udadisi, huo utafutaji wa maarifa ndio akili yenyewe. Mmeelewa sasa?

Huu ndio uzoefu wangu mimi na haya ni majibu ya swali linaloulizwa. Kwamba mtu anafanyeje hadi anakuwa na akili? Jibu ni sawa katika kipengele cha afya na hata kile cha utajiri.

Kwa wazazi wenye watoto angalizo;
Udadisi unapatikana penye utulivu
Udadisi unapatikana penye amani
Udadisi unasisimuliwa na vitu asili vya kuvutia na kushangaza.

Peleka mtoto kwenye shule yenye mazingira mazuri. Watoto wa mashuleni wafanye tour zitakazosisimua udadisi iwe ni kwa wanyama, au viwandani huko. Viwandani iwe ni kwa ajili ya kukata kiu ya udadisi wa 'hivi gari zinaundwaje?', mabati na nondo au karatasi zinaundwaje? Sio tu za twende kiwanda cha soda na mikate kunywa soda. Ujinga huu ukome. Mtoto aende kujibu swali la hivi soda na mikate vinatengenezwaje. Waalimu mnaweza kuileverage hii penda tamtamu ya watoto ili kuwaongeza udadisi. Mfano unanunua vifaa wanaenda kiwandani kujifunza recipe halafu mnakuja darasani mnatengeneza keki, mikate na soda mnakunywa wote.

Tengeneza mazingira ya mtoto kuona maua na wadudu mbalimbali, wanyama eeh! Kiufupi tengeneza ka 'Edeni' nyumbani kwako.

Badili 'approach' ya ukali na mafokeo kuwa uthabiti na maelekezo. Ukali unasisimua uoga tu unazalisha li Homo erectus. Lakini pia maelekezo yanazalisha skilled workers tu unazalisha li Homo habils. Ili uzalishe ka jiniazi kenye hekima hebu karuhusu kajaribu, kabebe majukumu na katatue matatizo madogomadogo ukisaidia knowledge za hapa na pale. Kakiweza kuharmonize knowledge unayokapatia hapo umepata a leader, a thinking man a Homo sapiens indeed.

Kiufupi mazingira yawe ni yanayomruhusu mtoto mwenyewe kujifunza maana msemo wa tatu unaojazia na kufunga ni 'Masala Kulangwa' yaani akili ni kufundishwa/kujifunza zaidi na zaidi.

Nb: mniwie radhi nimeandikaa mwisho nikachoka sikuwa na muda tena wa kuiperfect lugha. Pambaneni tumieni akili zenu maana mnazo tele
Akili is just one's training, kept in a long term memory, inayopelekea uweze kuwa na kumbukumbu sahihi pamoja na rational decisions zinachongiwa na past experience ambayo pia inakuwa imetunzwa kwenye memory

Capacity ya mtu kutunza details kwenye memory ndiyo kile tunachoita akili. Kwa mfano mtu mwenye akili darasani ni yule mwenye capavity nzuri ya kutunza vizuri kile ambacho mwalimu amefundisha. Mtu kufundishwa kitu ni mojawapo tu ya aina mbali mbali za training
 
Hii akili ya darasani mimi nimeichunguza na ninaendelea kuitafiti.

Mie nilikuwabna akili darasani. Na sikuwa na memory kubwa hata. In fact nina kumbukumbu karibia ya chini ya kawaida.

Kumbukumbu ni sehemu tu ya akili, ila akili sio kumbukumbu tu. Ni moja kati ya 'misconceptions' watu wanazo kwamba eti kufaulu ni kukumbuka, matokeo uake wanawekeza kwenye kukariri ili wakumbuke badala ya kuelewa ili wajue.
 
Hujanielewa kabisa!
Akili siyo kumbukumbu; isipokuwa akili huwa inatunzwa kwenye kumbukumbu. Kumbukumbu ni ghala, halafu akili ni bidhaa
 
Uwezo wa kuchakata jambo na kulipatia ufumbuzi kwa haraka zaidi naamini ndio akili ilipo.

Kumbukumbu sidhani kama ndio akili.
 
Wewe mtoto una akili ngumu sana kuelewa kitu. Soma tena nilichoandika. Unasoma darasa la ngapi?
 
Even when people are shouting lies, the truth is undamaged.
Exactly....

Truth doesn'nt suffer when subjected to speculation. In such circumstances, truth shines even brighter.

Lies ndo huwa zinavunjikavunjika zikichunguzwa ndio maana waliozileta huanza kuhangaika kuzitetea kwa nguvu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom