introvert
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,372
- 2,423
Huu utulivu ndio tunautaka kwenye mjadala.
Nakuomba utuwekee hivyo vipande iwe cha kizungu au kiswahili tuvijadili.
Tunachojadiliana ni hiki, "The Controller and Auditor-General shall hold office for the fixed term of five years and shall be eligible for renewal for one term only".
Kwa lugha ya sheria unapotumia neno shall inamaana huna uhuru zaidi ya kufanya unalotakiwa na kifungu husika iwapo vifungu vingine vyote vimezingatiwa.
Na ikiwa pana ulazima wa kuchaguliwa tena (reappointment) kulikua na haja ya kuweka muhula wa miaka mitano badala ya kumi kabisa?
Ni sawa na kusema CAG atadumu ofisini kwa miaka kumi kama vifungu vingine vitazingatiwa (mfano umri wa kustaafu haujafika).
Hakuna CAG Tanzania ambaye kipindi cha kwanza kilipoisha akachaguliwa mwingine. Hii ndiyo mara ya kwanza. Ni historia. Lakini haina maana kwa sababu kitu kimefanyika mara ya kwanza basi ni kosa ila inatuma ujumbe mkubwa juu ya uhuru wa CAG huyu wa sasa na wote wanaofuatia kama hili litakubalika.
Kwa hapa "kinachomfunga" Rais ni neno moja tu, shall. Hii inaweza kuwa sababu watangulizi wake hawakufanya kama alivyofanya yeye.
Ndiyo maana nimeuliza, kwa tafsiri yenu, ingetumika "may" au "shall" kwenu kusingekuwa na tofauti yoyote?