Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,457
- 34,477
Tuliangalie hili kwa makini sana. Jana wakati Waziri Mkuu akiwa anatembelea kukagua Kurasini Oil Jet (KOJ) aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo (WMA) pamoja na wakubwa wengine. Swali alilomuuliza huku akitaka maelezo yake yatolewe ni ......KWA NINI ULIAMUA KUWASHA METER JANA BAADA YA KUTUMIWA UJUMBE WA SMS?......
Kiintelejensia hili limekaaje?
Inanipa mashaka hata ulinzi wa viongozi hawa ambapo inawezekana Watanzania wasio wema wakaamua kuwauza ili waondoke mbele ya macho ya Watanzania wenye kuhitaji huduma zao.....
Kwa jicho la weledi ni kwamba katika timu ya watakatifu waliowazunguka Majaliwa na JPM wapo wanaouza taarifa kwa watuhumiwa watarajiwa......“Nataka unieleze ni kwa nini ulitoa maelekezo ya kufunga mita hizo, na kwa nini jana uliamua kubadili uamuzi huo? Ni kwa nini umeamua kuchukua maamuzi haya baada ya kupokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) wakati mita zimekaa bila kufanya kazi kwa miaka mitano? Ni kwa nini umeamua kufanyia kazi ujumbe wa sms wakati unajua Serikali inafanya kazi kwa maandishi rasmi?” alisema Waziri Mkuu.....
Kiintelejensia hili limekaaje?
Inanipa mashaka hata ulinzi wa viongozi hawa ambapo inawezekana Watanzania wasio wema wakaamua kuwauza ili waondoke mbele ya macho ya Watanzania wenye kuhitaji huduma zao.....