Ingekuwa vipi kama mkeo naye akakugeuzia kibao

Fidel tusichukue uamuzi wa harakaharaka bali tuangalie kwa undani.
Na je ikiwa wewe ndiyo wa kuondoka na rambo mkononi kwa maana ya kuwa yeye ndiye mwenye uwezo?

Kwa undani kivipi?
Mwanamke akitoka nje ya ndoa ni dharau kubwa sana kwa mwanaume anastahili kufukuzwa kabisa...
Mwanamke kama umetoka nje unamdhalilisha mmeo na ni dharau kwa mmeo.
 
TENA UMESEMA VEMA KABISAAA!
Wanaume nao wajue kuwa wanapotoka nje wanawadharau na kuwadhalilisha wake zao na inauma sana kujua kuwa mumeo ametembea na mwanamke mwingine.Ndiyo maana wazungu hawavumilii upuuzi huu- ni talaka tu.Siyo kama sisi waswahili ukiombwa msamaha na kubembelezwa unakubali .
 
Mwanaume zamani ilikuwa mtu akitoka nje na kuongeza mwanamke au mke mwingine unaonekana wewe ni rijali na mke mmoja hakutoshi....
Mwanaume zamani ataka kuwa na mke white,black,mnene,mwembamba,mwenye kalio,kimodel n.k
 
Usha qualify kwa kusema ZAMANI.Tuko enzi nyingine.
Kama ni zamani - kuna mambo mengi zamani yalikuwa yanafanyika na kuonekana ya kawaida lakini ukiyafanya siku hizi utafanyaa watu wakushangae!
 
Hii kitu ipo mpaka sasa saizi ndo imefanyiwa modification ndo tunaita nyumba ndogo watu wanajipendelea kihalali wengine kwa kificho.
 
TENA UMESEMA VEMA KABISAAA!
Wanaume nao wajue kuwa wanapotoka nje wanawadharau na kuwadhalilisha wake zao na inauma sana kujua kuwa mumeo ametembea na mwanamke mwingine.Ndiyo maana wazungu hawavumilii upuuzi huu- ni talaka tu.Siyo kama sisi waswahili ukiombwa msamaha na kubembelezwa unakubali .

WoS, wazungu wengi siku hizi wanaruhusu hili la mume na mke kuwa na boyfriend au girlfriend nje ya ndoa na wanadai kwamba limepunguza kwa kiasi kikubwa ugomvi unaosababishwa na wivu. Mradi tu njemba au mama aage nyumbani kwamba anaenda kwa girlfriend/boyfriend wake naweza kurudi au kulala huko huko. Sijui kma hili litakubalika kwenye jamii yetu ya Kitanzania.
 
BAK,
Thanks for the info.Nadhani hapa napo ndipo tunapotofautiana tena na hawa wenzetu.Jamii zetu zimejaa unafiki wa hali ya juu.Hatupendi kuona ukweli na kuukubali.
Utakuta mwanaume amekuchoka, hakutaki lakini hapo hapo anakulilia wivu.Usisemeshwa wala hata kupewa salamu. Kosa! Inakuwaje hii?
 
I am 100% with you on your argument about this. Utamuona njemba hajamgusa mkewe miezi chungu nzima maana yuko busy na nyumba ndogo, lakini Mkewe akiongeleshwa na njemba nyingine basi ni ugomvi wa mama ntazamie. Kweli huu ni unafiki mkeo hujamgusa miezi chungu nzima, humtimizii matamanio yake ya kimwili kama mwanamke na wakati huo huo hutaki njemba nyingine zimchangamkie. MWACHE BASI ILI AANGALIE USTAARABU MWINGINE!!
 
Kuacha haachi ng'oo! Vinginevyo ule msemo wa " ukisema wa nini, wenzio wanasema nitampata lini" ndipo ungefanya kazi.
The bottomline is - kwenye long term relationship mazoea huchukua nafasi ya excitement na hii ni kwa wote wanawake na wanaume.Badala ya mwanaume kuona kana kwamba yeye tu ndiyo kachoka na hivyo anahitaji kubadili, basi amfikirie na mkewe pia kuwa yuko kwenye hali hiyohiyo.Then kwa pamoja wajipange upya kuweka cheche tena na kuwasha moto wa mapenzi yao ili siku ziende.
 
I am 100% with you on your argument about this. Utamuona njemba hajamgusa mkewe miezi chungu nzima maana yuko busy na nyumba ndogo, lakini Mkewe akiongeleshwa na njemba nyingine basi ni ugomvi wa mama ntazamie. Kweli huu ni unafiki mkeo hujamgusa miezi chungu nzima, humtimizii matamanio yake ya kimwili kama mwanamke na wakati huo huo hutaki njemba nyingine zimchangamkie. MWACHE BASI ILI AANGALIE USTAARABU MWINGINE!!

...huenda anampa mkewe mapumziko jamani! :)
 
WoS, wazungu wengi siku hizi wanaruhusu hili la mume na mke kuwa na boyfriend au girlfriend nje ya ndoa na wanadai kwamba limepunguza kwa kiasi kikubwa ugomvi unaosababishwa na wivu. Mradi tu njemba au mama aage nyumbani kwamba anaenda kwa girlfriend/boyfriend wake naweza kurudi au kulala huko huko. Sijui kma hili litakubalika kwenye jamii yetu ya Kitanzania.

kwa vile ninavyo waelewa wabongo hilo linawezekana tena sana inatakiwa kutokea kundi fulani ndani ya jamii na kuwambia hii ndivyoilivyokuwa wakati huo au vyenginevyo ndani ya miaka 5 utaona matokeoi yake (people in TANZANIA there so naive)
 
BAK,
Thanks for the info.Nadhani hapa napo ndipo tunapotofautiana tena na hawa wenzetu.Jamii zetu zimejaa unafiki wa hali ya juu.Hatupendi kuona ukweli na kuukubali.
Utakuta mwanaume amekuchoka, hakutaki lakini hapo hapo anakulilia wivu.Usisemeshwa wala hata kupewa salamu. Kosa! Inakuwaje hii?

...kwa lugha nyepesi tunaita "kukumbwa na mfadhaiko pamoja na msongo wa mawazo"
 
Kumekuwepo na majadiliano ya kutosha sana humu jamvini kuhusu matatizo ya wanawake na waume au wapenzi wao - Kutelekezwa, kuletewa nyumba ndogo,kuachiwa mzigo wa kulea familia, kutumiwa n.k.Pia tumejadili kuhusu kwanini wanaume hawapendi ushirika kwenye mapenzi.

Tunajua kabisa kuwa tamaduni, mila, desturi, dini vyote vinaamrisha wanandoa kuheshimu ndoa zao.Pamoja na hayo ukweli unabakia kuwa wanandoa hutetereka katika kuheshimu viapo vyao.Msisitizo zaidi uko katika kuwataka wanawake wajiheshimu na inashangaza kuwa msisitizo hauko zaidi katika kuwabana wanaume.Kutokana na hili, wanaume nao wamekuwa wakilega zaidi katika kuheshimu ndoa au mahusiano yao.

Matokeo yake ni kuwa watu wamekuwa wakifumbia macho suala zima la kutoka nje ya ndoa.Hakuna mwanamke anakubali kuwa wanawake nao wanatetereka , na hata wanaume nao wanajidanganya kuwa wapenzi wao au hata wake zao hawatoki nje ya ndoa.Ila hapohapo tunasikia ati vipimo vya DNA vimethibisha kuwa idadi kubwa ya watoto waliozaliwa na wazazi waliokuwa na mabishano kuhusu nani baba wa mtoto - wameonekana siyo wa akina baba hao walengwa.

Je, Mwanaume anayetoka nje ya ndoa na mke wa mtu au mpenzi wa mtu mwingine anajisikia vipi pale mkewe akichukuliwa na mwanaume mwingine?
Vichaa wawili wa kike na wakiume wakipita mbele ya hadhara ya watu bila nguo,nidhahiri shahiri kuwa kwa kichaa wa kiume watu hawatajali, bali kwa yule wa kike kila mtu atakuwa ATTENTIVE.

Maana yake ni nini? Ni kwamba kwa asili Mwanamke anaheshimika sana kwenye jamii.

Jamii inatarajia kuwa hatofanya mambo YASIYOFAA.

Kwa kifupi mwanamke kutembea nje ya ndoa ni MARUFUKU.

Kwa mwanaume ni SUNNA(Ni suala la hiari)
 
Hii mada nataka kuchokoza kupata mawazo ya wanaume maana assumption ni kuwa wanawake hawatoki nje ya ndoa ( japo inajulikana kuwa wanatoka)

Hiyo assumption ishakuwa debunked long ago.

lakini hapo hapo inajulikana kuwa wanaume wanatoka tena wakati mwingine na wake za watu au wapenzi wa watu wengine.

Mwanaume anayetoka na wake za watu? Na huyo mke wa mtu anayetoka na wanaume je?

This is what I think though it can not be empirically verified. Men and women are neck and neck when it comes to cheating.
 
Hii mada nataka kuchokoza kupata mawazo ya wanaume maana assumption ni kuwa wanawake hawatoki nje ya ndoa ( japo inajulikana kuwa wanatoka)lakini hapo hapo inajulikana kuwa wanaume wanatoka tena wakati mwingine na wake za watu au wapenzi wa watu wengine.

Wakati niko Jandoni na wenzangu moja wapo ya vitu tulivyoelezwa ni kuwa wake za wenyewe pia hutoka nje ya ndoa, kwa hali hiyo baba mwenye nyumba unaposafiri si vema wakati wa kurudi ukaenda nyumbani moja kwa moja, badala yake kale kazawadi ulikokuja nako unakatanguliza kwa kumtuma mtoto yeyote ili iwe ishara kwamba mwenye mji amesharejea nyumbani na kama mama mwenyenyumba alikuwa na mishemishe basi aweke mambo vizuri. Philosofia hii ukiichambua kwa undani zaidi unaona kuwa kitu muhimu ni anayetendewa kutofahamu kuwa anatendewa na hivyo hujiaminisha kuwa mambo ni shwari. Hili utaliona, mathalan, kwenye wanaume kutafuta mchumba wa kuoa. Nakumbuka wanaume wengi wa vijijini hupenda kutafuta mchumba wa kijiji kingine kwa sababu anaamini kuwa wanawake wa kijiji chake ni wahuni kwa sababu tu anafahamu kuwa fulani anamahusiano na fulani na fulani, lakini kwenye kijiji kingine anakuwa hajui kinachoendelea. Lakini pia hata nyakati za sasa utakuta vijana wa vyuo wanakwenda kutafuta wapenzi kwenye vyuo vingine kwa kuamini kuwa wale wa chuoni kwao ni wahuni kwa sababu kama nilizozitaja hapo juu.

Hali hii ndiyo huleta hitimisho la "........siamini macho yangu......., au sikutarajia kama na wewe uko hivi"; pale mtu anaposhuhudia laiv mwenzi wake akijirusha na mtu mwingine
 
Asante mkuu kwa kutupa busara hizi.
Wahenga walikuwa na busara sana na ndiyo maana huko nyuma ilikuwa nadra kusikia au kuona migogoro na mitafaruku inayotokana na kuhisiana au kufumaniana.

Ila kuna kitu kimoja - watu siku hizi wanachimbana sana.Mke anamchunguza mume na mume anajitahidi sana kumchunguza mkewe.Tena hizi simu za kiganjani ndiyo shetani mkuu anayevunja ndoa za watu. Zipo kesi nyingi tu zinazuka kila leo kisa ni kupekuana kwenye simu kuona sms za watu n.k.Kwa mtaji huu ile philosophy ya usilolijua halitakuumiza inakuwa haipo.
 
Hii philosophy ya usilolijua halitakuumiza ni nzuri na kweli inasaidia kupunguza maumivu but kwanini usilijue la mwenzio (mke au mume)? Km mmeamua kuwa wanandoa inabidi mambo yawekwe hadharani ili watu mfahamiane inavyopasa. Hii itatoa nafasi kwa mtu kuchagua kusuka au kunyoa. Ndio maana wenzetu 'wazungu' hawako wanafiki km mke anaboyfriend mume ataambiwa ili ajichagulie la kufanya km kuendelea au divorce! Kuchimbana ni kawaida cha msingi usifanye mambo ya 'gizani',fanya mchana kweupeee mwenzio ajue nini kinaendelea ili aamue nayeye afanyeje, kwa makubaliano.
 
Ndiyo maana kuna methali kama ..ukimchunguza sana kuku hutamla.Pia binadamu tulivyo kila mmoja ana siri lukuki ambazo kama zingewekwa bayana nadhani pangekuwa hapatoshi kwa inda, madharau, hasira, chuki,visasi,n.k. Binafsi nisingependa kujua kila kitu kinachomhusu mtu wangu.
 
Back
Top Bottom