India kuanzisha chuo cha TEHAMA nchini Tanzania

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Serikali ya India inatarajiwa kuanzisha Chuo cha Teknolojia nchini ambacho kitakuwa kinatoa kozi ya masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na kozi nyingine zinazoendana na mrengo huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema hayo Dares Salaam baada ya kukutana na Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan pamoja na timu ya wataalamu kutoka Chuo cha Teknoloiia India.

Mkenda alisema Serikali ya Tanzania itashirikiana na India ili lengo la kuanzisha chuo hicho liweze kutimia kwa wakati na wanafunzi wasajiliwe mwaka mpya wa masomo ifikapo Novemba mwaka huu.

Alisema chuo hicho kipo mbali kiteknolojia ndio maana wamekialika kuja kuona mazingira ya Tanzania katika kutimiza lengo lao la kuanzisha chuo hapa nchini.

"Wanataka kuanza kuchukua wanafunzi Oktoba mwaka huu, ni muda mfupi sana kutokea sasa ila tutafanya kazi usiku na mchana kuona ni nini kinaweza kufanyika tukasonga mbele," alisema.

Mbali na kufikia Dar es Salaam timu hiyo kutoka India imekwenda kutembelea Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela kilichoko jijini Arusha pamoja na

Taasisi ya Teknolojia Dares Salaam (DIT) ili kuona vifaa vya kujifunzia na kufundishia vilivyopo na namna ambavyo wanaweza kufanya kazi kwa pamoja.

"Timu hi tutakutana nayo tena Februari 17 mwaka huu ili kwa pamoja tuangalie rasimu ya makuballiano ili tuone tunakwendaje," alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Pradhan alisema Serikali ya India imejizatiti kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha pamoja na mambo mengine lengo la kuanzisha chuo nchini linafanikiwa.

India.jpeg
 
Serikali ya India inatarajiwa kuanzisha Chuo cha Teknolojia nchini ambacho kitakuwa kinatoa kozi ya masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na kozi nyingine zinazoendana na mrengo huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema hayo Dares Salaam baada ya kukutana na Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan pamoja na timu ya wataalamu kutoka Chuo cha Teknoloiia India.

Mkenda alisema Serikali ya Tanzania itashirikiana na India ili lengo la kuanzisha chuo hicho liweze kutimia kwa wakati na wanafunzi wasajiliwe mwaka mpya wa masomo ifikapo Novemba mwaka huu.

Alisema chuo hicho kipo mbali kiteknolojia ndio maana wamekialika kuja kuona mazingira ya Tanzania katika kutimiza lengo lao la kuanzisha chuo hapa nchini.

"Wanataka kuanza kuchukua wanafunzi Oktoba mwaka huu, ni muda mfupi sana kutokea sasa ila tutafanya kazi usiku na mchana kuona ni nini kinaweza kufanyika tukasonga mbele," alisema.

Mbali na kufikia Dar es Salaam timu hiyo kutoka India imekwenda kutembelea Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela kilichoko jijini Arusha pamoja na

Taasisi ya Teknolojia Dares Salaam (DIT) ili kuona vifaa vya kujifunzia na kufundishia vilivyopo na namna ambavyo wanaweza kufanya kazi kwa pamoja.

"Timu hi tutakutana nayo tena Februari 17 mwaka huu ili kwa pamoja tuangalie rasimu ya makuballiano ili tuone tunakwendaje," alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Pradhan alisema Serikali ya India imejizatiti kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha pamoja na mambo mengine lengo la kuanzisha chuo nchini linafanikiwa.View attachment 2520509
Kile cha st Joseph kimewashinda wataweza hiki

USSR
 
Prof. Mkenda ni miongoni mwa mawaziri wanao fanya kazi nzuri sana haswa kwenye kusimamia Elimu yeti, tunamuomba Mh. Rais katika mabadiliko yake amuache hapo hapo.
 
Serikali ya India inatarajiwa kuanzisha Chuo cha Teknolojia nchini ambacho kitakuwa kinatoa kozi ya masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na kozi nyingine zinazoendana na mrengo huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema hayo Dares Salaam baada ya kukutana na Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan pamoja na timu ya wataalamu kutoka Chuo cha Teknoloiia India.

Mkenda alisema Serikali ya Tanzania itashirikiana na India ili lengo la kuanzisha chuo hicho liweze kutimia kwa wakati na wanafunzi wasajiliwe mwaka mpya wa masomo ifikapo Novemba mwaka huu.

Alisema chuo hicho kipo mbali kiteknolojia ndio maana wamekialika kuja kuona mazingira ya Tanzania katika kutimiza lengo lao la kuanzisha chuo hapa nchini.

"Wanataka kuanza kuchukua wanafunzi Oktoba mwaka huu, ni muda mfupi sana kutokea sasa ila tutafanya kazi usiku na mchana kuona ni nini kinaweza kufanyika tukasonga mbele," alisema.

Mbali na kufikia Dar es Salaam timu hiyo kutoka India imekwenda kutembelea Chuo Kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela kilichoko jijini Arusha pamoja na

Taasisi ya Teknolojia Dares Salaam (DIT) ili kuona vifaa vya kujifunzia na kufundishia vilivyopo na namna ambavyo wanaweza kufanya kazi kwa pamoja.

"Timu hi tutakutana nayo tena Februari 17 mwaka huu ili kwa pamoja tuangalie rasimu ya makuballiano ili tuone tunakwendaje," alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Pradhan alisema Serikali ya India imejizatiti kufanya kazi na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha pamoja na mambo mengine lengo la kuanzisha chuo nchini linafanikiwa.View attachment 2520509
Mmh. Nahisi ni ndoto tu. Sijui.
 
Back
Top Bottom