Uchaguzi 2020 Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii ya T 2020 JPM?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,741
107,875
Nimekuwa nikiona magari mengi tofauti yana namba za usajili T2020 JPM, nauliza je hii ni namba halali kwa magari haya?

Nimeona magari zaidi ya 10 yana namba hii. Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii?

Mfano limesababisha ajali nikienda polisi nikiwatajia namba hii watajua ni ipi kati ya hizo nyingi zinazotumia namba hii?

Cc: Mkuu wa usalama barabarani.
 
Kama hizi?
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
Kila siku tunapiga kelele kuhusu Serikali hii na CCM yake wanafanya mambo ya kipuuzi yaliyo kinyume cha Sheria lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Imagine hayo magari yangekuwa yameandikwa Lissu au Rungwe unadhani yangeruhusiwa kupita Barabarani?
 
Back
Top Bottom