Umuhimu wa mpangilio wa namba na herufi katika makasha ya mizigo

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,560
9,791
Wadau nikiwa napitia katika mitandao ya kijamii, nimeona na kujifunza sehemu fulani maana iliyopo nyuma ya muundo wa herufi na namba tofauti zinazosomeka katika makasha makubwa ya kusafirishia mizigo hasa bandarini, ambayo kwa umaarufu hufahamika kama makontena, yaani "containers". Nitangulize samahani kama mada hii iliwahi kuletwa hapo awali na mdau mwingine hapa jukwaani bila ya mimi kung'amua, lakini kwa upande wangu nimeona ni "worth to share"

Makasha ya mizigo katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi huonekana kila moja likiwa na muundo fulani wa namba na herufi zenye mpangilio fulani unaofanana.

Makasha haya ambayo yana urefu wa futi 20 ama 40, kila moja lina mtindo unaofanana wa kusomeka kwa namba ama herufi zake. Kwa kifupi muundo huo ni kipekee ili kulitambua kasha husika ili liweze kutofautishwa na jingine, kwa kifupi tinaweza kuliita ndilo jina la ubatizo wa kasha lipate kuweza kusajiliwa.

Mpangilio huo hutoa tafsiri muhimu sana kuhusu aina ya mzigo uliobebwa ndani yake, umiliki wa kasha, na hata aina ya chombo ama njia inayopaswa kulisafirisha ama kulipakuwa lifikapo bandarini, ama usafiri utakaotumika kubeba mzigo uposafirishwa kwenda kwa mnunuzi.

Muundo wa namba na herufi hizo hutoa tafsiri zifuatazo;

1. Herufi kubwa 3 za kwanza hutambulika kamq "Owner Prefix Code" hizi hutoa tafsiri kuhusu mmiliki wa kasha

2. Herufi kubwa ya nne ambayo husomeka kwa U, J ama Z hutoa tafsiri kuhusu chombo ama njia ya kulisafirisha kasha.

‘U’ huashiria mzigo wa kawaida upo ndani ya kasha
"J" ufahamika kama "detachable" yaani mzigo ni mkubwa na hauwezi kuingia ndani ya kasha
"Z" ni uchukuzi wa mizigo aina ya matela na "chassis" tu.

Herufi zote nne katika masuala ya usafirishaji na uchukuzi kwa pamoja hutambulika kama "alpha prefix"

3. Mpangilio wa namba 6 hutambulika kama namba za usajili wa kasha, na hizi hutolewa na mmiliki wake ili aweze kutofautisha kasha moja na lingine.

4. Namba ya 7 na ya mwisho hutambulika kama "check digit" hii huonekana upande wa kulia kabisa na ikiwa ipo ndani ya sanduku.

5. Namba ya mwisho ikisomeka sambamba na nyingine ndiyo hulifanya kasha moja liweze kuonekana tofauti na mengine katika mifumo tofauti usafirishaji na uchukuzi na ile ya ulipaji wa tozo husika.
Container-Number-1.jpg
 
Back
Top Bottom