Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Hao viongozi si kwamba hawajui katiba, huwa wana makandokando yao ya figisu za kutaka kutofuata katiba.

Ukimsikiliza January Makamba alivyoongea hivi karibuni alikuwa anasema watu waliokuwa wanafanya kazi Ofisi ya Makamu ya Rais walitengwa, hata salamu walikuwa hawapewi.

Kwa hiyo haya mambo ya kumshirikisha Waziri Mkuu bila kumshirikisha Makamu wa Rais hayakutokea jwa bahati mbaya au kwa kukosa kujua katiba.

Huo ulikuwa ni mpango makusudi wa kumuondoa Makamu wa Rais katika succession plan.

Ukimsikiliza Mabeyo kuna sehemu kasema mambo kwa summary sana, kafupisha sana, hajatoa story kamili. Hii jistoria inahitaji kitabu kizima kuiandika.

Na kuhusu Magufuli alikuwa na haki ya kufia nyumbani kwake, everyone has a right to die with dignity, na moja kati ya haki hizo ni pale mtu anapogundua kuwa haponi, basi apewe nafasi ya kufa nyumbani akizungukwa na wapendwa wake.

Kwanza marehemu hawezi kulaumiwa kwa kutaka kupelekwa kwao au hata angetamka chochote muda huo.

Katika hali kama hiyo ya kukielekea kifo, mgonjwa anasemehewa kwa chochote anachoweza kusema.
 
Tulia. 2025 kabla ya uchaguzi ndo utausikia ukweli wenyewe; Mabeyo anawaandaa tu Kisaikolojia. Mtakayoyasikia mtalazimika kumpumzisha mtu. Tulia
Usijifanye unajua sana kutafsiri tafsida au mafumbo. Hotuba ya Mabeyo siyo ya kuifanyia ubashiri. Wote tumesikia wala haina mikunjo au mikwaruzo

Huo utabiri wako wa 2025 ifanyie familia yako tu iondokane na umaskini wako. Rais Samia tunaye hadi 2030
 
Kutumbua ndiyo nini? Ni ujinga tu alioanzisha Magufuli kisha wananchi wajinga wakawa wanaitikia kama chorus.

Kwa mfano alimtumbua Wilson Kabwe akiwa anazindua daraja la Nyerere pale Kigamboni. Kisha Wilson Kabwe akafariki baada ya siku chache. Je wewe Raia mpya ulipata nini kwa kitendo hicho
Kutumbua nimesema kama mfano ila ki maamuzi makamu wa rais hana maamuz yeyote yale kifupi hana nguvu
 
In Tanzania, it's common for people to hold degree papers without actually being literate.
These papers don't necessarily prove their ability to perform tasks, but instead serve as a means of pursuing monetary gain.

Unfortunately, those who hold degrees but don't prioritize money or unethical deals are often seen as foolish or less successful.
 
Mkuu Kiranga Mabeyo hajazungumza kuhusu swala la Waziri mkuu kuwa anapewa updates ya Hali ya afya ya Magufuli, Ila ameelezea baada ya Magufuli Kufariki ni Majaliwa na Bashiru Alli ndio walikuwa wakwanza kabisa kutaalifiwa kwamba Magufuli katutoka kabla ya Rais Samia.
Point taken.

Ila, bado swali liko pale pale kwa nini Rais anayeumwa mahututi anaita Paroko, anaita Kardinali, anaita CDF, anaita IGP, anaita DGIS, lakini anashindwa kumuita VP?
 
Lakini mi navoona Vp kwa bongo ni cheo ila kipo kipo tu hakina nguvu, hata kipindi cha magu kwenye kutumbua kama sio Magu basi ni majaliwa basi hatujawahi kumsikia hangaya akimtumbua hata mjumbe wa nyumba 10.

Hata waziri mkuu alisema rais ni mzima na anachapa kazi, kuna tofauti gani na hizo story za vijiweni? Ww ndio uendelee kuamini hizo taarifa za serekali ambazo nyingi ni za kupika.
Basi mtaani utakutana na taarifa wewe umekufa
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Hivi aliyetaarifiwa kwamba raisi amefariki ni mkuu wa majeshi au mkuu wa majeshi ndo alikuwepo wakati mheshimiwa raisi alipokuwa anakata roho??!!!!

Hebu angalia Aya ya nne ya thread yako na ufuatilie mazungumzo ya CDF vizuri
 
Sasa mtu anakufa, madaktari washaona huyu hatoboi anakufa, unamfanyia itifaki ya usalama wa hali ya juu asiende kufa nyumbani kwake, akibaki hospitali ndiyo utazuia asife?

Itifaki haifanywi kwa sababu ya itifaki tu, inafanywa kwa rationale.

Ukiondoa hizo sababu possible nilizozitaja, rationale ya kumzuia rais anayetaka kwenda kufia nyumbani kwake asiende kufia nyumbani kwake ni ipi?
Huenda madaktari bado walikuwa wana imani angeweza kupona !

Nadhani mara nyingi huwa ni madaktari ndio wenye uwezo wa kujua mgonjwa wao anaweza kupona au hawezi kupona !
Mgonjwa huweza kuzungumza mengi kutokana na maumivu anayoyapata !
Wagonjwa wengi tu huwa wanaomba warudishwe nyumbani lakini huwa hawarudishwi !
 
In Tanzania, it's common for people to hold degree papers without actually being literate.
These papers don't necessarily prove their ability to perform tasks, but instead serve as a means of pursuing monetary gain.

Unfortunately, those who hold degrees but don't prioritize money or unethical deals are often seen as foolish or less successful.
Iko vile bandugu !
Hii ni Bongolala !
Come easy go easy 😅😅🙏🙏
 
Hili jambo wengi wenu mnalichukulia kisiasa, na hapo ndipo mnapokosea.

CDF Mabeyo wakati akiitwa kupewa zile taarifa hakuwa mwanasiasa yule, alienda pale kwa nafasi yake kama mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa taifa.

Aliitwa pale kwasababu jambo la ugonjwa wa Rais ni nyeti linalohusisha zaidi usalama wa nchi, mnataka Makamu wa Rais aingie hapo kwa cheo gani alichonacho kijeshi kilichoainishwa kikatiba?

Mkisha tambua hilo mtaachana na hizo habari zenu za Makamba sijui alinyimwa salamu na vitu gani....
Pia ni mwenyekiti wa vyombo vya ulinzi na usalama
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Naomba kujazia.
1. CS ndo anaratibu ziara za viongozi wakuu. So inawezekana ziara ya VP ilikuwa kumweka out of the loop.
2. CDF hakujulishwa, alishuhudia kama ulimfuatlia vizuri.
3. Kuna watu walitaka kupindisha katiba kwa kuonesha VP akiwa hayupo basi Speaker may assume authority. Waliotakiwa kusimamia kuhakikisha katiba inafuatwa ni CS.
4. Maamuzi ya kuhakikisha katiba inafuatwa ni ya CDF kwani inaonekana kulishakuwa na mta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom