Inawezekana tuna watu wasio na uwezo katika nafasi wanazozitumikia?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
 
Walikuwa wako Kenya wote ndo maana labda, isitoshe kinachoendelea ni gas lighting tu, raisi hawezi kufariki tena kwa kuumwa halafu makamu wa raisi asijue never ever, makamu wote hujua kila kitu na hata huwa washajitayarisha kuchukua nchi …
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Hao viongozi si kwamba hawajui katiba, huwa wana makandokando yao ya figisu za kutaka kutofuata katiba.

Ukimsikiliza January Makamba alivyoongea hivi karibuni alikuwa anasema watu waliokuwa wanafanya kazi Ofisi ya Makamu ya Rais walitengwa, hata salamu walikuwa hawapewi.

Kwa hiyo haya mambo ya kumshirikisha Waziri Mkuu bila kumshirikisha Makamu wa Rais hayakutokea jwa bahati mbaya au kwa kukosa kujua katiba.

Huo ulikuwa ni mpango makusudi wa kumuondoa Makamu wa Rais katika succession plan.

Ukimsikiliza Mabeyo kuna sehemu kasema mambo kwa summary sana, kafupisha sana, hajatoa story kamili. Hii jistoria inahitaji kitabu kizima kuiandika.

Na kuhusu Magufuli alikuwa na haki ya kufia nyumbani kwake, everyone has a right to die with dignity, na moja kati ya haki hizo ni pale mtu anapogundua kuwa haponi, basi apewe nafasi ya kufa nyumbani akizungukwa na wapendwa wake.
 
Kama unataka kufia kwako si umwambie daktari? Kwa nini umwambie CDF? Yeye na masuala ya matibabu wapi na wapi?
 
Na ndo maana Nimeanza kuamini ile Story ya Yoga ya Dark days aisee
 
Baada ya Rais ni Makamu wa Rais kwenye jambo gani?

Jambo linalohusu usalama wa nchi limekabidhiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, CDF ndie anayetakiwa kuwa wa kwanza kupewa taarifa.

Ndio maana baada ya cheo cha Rais akiitwa Amiri Jeshi Mkuu, cheo kinachofuatia hapo ni CDF, Makamu wa Rais haingii hapo.

Au utuambie, ni kipi cheo cha Makamu wa Rais kijeshi ilituone kama kweli alirukwa makusudi kutopewa taarifa?

Unapokuja na lawama zako kwanza ujue jambo unalolizungumzia ni lipi, lipo chini ya category ipi, ujue mpangilio wa vyeo kwenye category husika, kisha ndio uje na lawama kama zipo, usikurupuke tu na ujuaji wako.
 
Hili jambo wengi wenu mnalichukulia kisiasa, na hapo ndipo mnapokosea.

CDF Mabeyo wakati akiitwa kupewa zile taarifa hakuwa mwanasiasa yule, alienda pale kwa nafasi yake kama mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa taifa.

Aliitwa pale kwasababu jambo la ugonjwa wa Rais ni nyeti linalohusisha zaidi usalama wa nchi, mnataka Makamu wa Rais aingie hapo kwa cheo gani alichonacho kijeshi kilichoainishwa kikatiba?

Mkisha tambua hilo mtaachana na hizo habari zenu za Makamba sijui alinyimwa salamu na vitu gani....
 
Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?
CDF ameeleza vizuri tu kuwa alikuwepo hospital muda wote siku ya kifo na aliitwa baada ya mgonjwa kuzidiwa

By the way unawajua vizuri wanawake walivyo wanapopata taarifa ya msiba!!
 
Baada ya Rais ni Makamu wa Rais kwenye jambo gani?

Jambo linalohusu usalama wa nchi limekabidhiwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, CDF ndie anayetakiwa kuwa wa kwanza kupewa taarifa.

Ndio maana baada ya cheo cha Rais akiitwa Amiri Jeshi Mkuu, cheo kinachofuatia hapo ni CDF, Makamu wa Rais haingii hapo.

Au utuambie, ni kipi cheo cha Makamu wa Rais kijeshi ilituone kama kweli alirukwa makusudi kutopewa taarifa?

Unapokuja na lawama zako kwanza ujue jambo unalolizungumzia ni lipi, lipo chini ya category ipi, ujue mpangilio wa vyeo kwenye category husika, kisha ndio uje na lawama kama zipo, usikurupuke tu na ujuaji wako.
Usalama wa Nchi ndio kipaumbele cha Nchi yeyote ile kwahiyo CDF yupo sahihi na alikuwa sahihi kwenye tukio lote !
 
Kama unataka kufia kwako si umwambie daktari? Kwa nini umwambie CDF? Yeye na masuala ya matibabu wapi na wapi?
Nilikuwa nakujibu suala la kwamba Magufuli alikuwa na haki ya kutaka kufia kwake.

Hilo halina mjadala.

Kuhusu kumwambia CDF, katika mawazo yake aliona kawaambia madaktari hawajakubali sasa amwambie CDF aamrishe kijeshi.

Magufuli alikuwa mtu wa amri. Inawezekana alikosea kumwambia CDF, lakini ikiwa aliwaambia madaktari wakamkatalia huku wakijua huyu anafariki, ama walijua hiyo safari hataimaliza ndiyo maana wakamkatalia.

Au pengine alikuwa na Covid wakaona kumpeleka nyumbani itakuwa vigumu kuepusha maambukizi kwa ndugu.

Vinginevyo, wamemkatalia haki yake ya kufia nyumbani na dignity.
 
Mahojiano aliyofanya CDF Mstaafu Venance Mabeyo yamenifundisha kitu.

Nchi hii tuna shida kubwa sana ya watu kuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi na uongozi ambao hawastahili kuwepo kwenye nafasi hizo kwa kukosa uwezo.

Hivi inakuwaje kwenye nchi tena yenye miaka zaidi ya 60 ya uhuru watu kwenye nafasi za juu kabisa za maamuzi hawajui kuwa kwenye chain of Command baada ya Rais ni Makamu wa Rais?

Hivi inakuwaje Rais anafariki wa kwanza kutarifiwa ni Mkuu wa Majeshi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje na Mkuu wa Majeshi anaingia Kuanza kusema nimfaarifu Waziri Mkuu au Katibu Mkuu Kiongozi na sio Makamu wa Rais?

Inakuwaje tuna viongozi kwenye nafasi za juu kabisa ambao hawajui hata Katiba ya Nchi inasemaje?

How comes wanaotuongoza hawaijui Katiba?

Kituko zaidi ni mtu aliyefika hadi kuwa Rais wa Nchi anaamuru Mkuu wa Majeshi aamuru atolewe hospitali na kupelekwa kijijini kwake?

Hivi alikuwaje Rais na hajui hata mipaka ya madaraka na uongozi?

Kusema kweli tuna tatizo kubwa kwenye hii nchi na hii ni kansa ambayo kusema kweli itatutafuna na kutumaliza kabisa.
Samia hana uwezo wowote ule.

Uhudumu wa ndege ilikuwa ndoto yake nafikiri huko kungemfaa zaidi.
 
Hili jambo wengi wenu mnalichukulia kisiasa, na hapo ndipo mnapokosea.

CDF Mabeyo wakati akiitwa kupewa zile taarifa hakuwa mwanasiasa yule, alienda pale kwa nafasi yake kama mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa taifa.

Aliitwa pale kwasababu jambo la ugonjwa wa Rais ni nyeti linalohusisha zaidi usalama wa nchi, mnataka Makamu wa Rais aingie hapo kwa cheo gani alichonacho kijeshi kilichoainishwa kikatiba?

Mkisha tambua hilo mtaachana na hizo habari zenu za Makamba sijui alinyimwa salamu na vitu gani....
Mkuu,

Here are facts.

1.Hakuna popote nilipomtaja CDF Mabeyo.

2.CDF Mabeyo mwenyewe kasema kuna watu walitaka kupindisha utaratibu.

3. Kwa mujibu wa CDF Mabeyo Makamu wa Rais alirukwa kabisa kwenye updates za kutoka hospitalini, habari alikuwa anapewa Waziri Mkuu Majaliwa. Licha ya kwamba Makamu wa Rais ndiye mrithi wa Rais, ikiwa Rais atafariki, kikatiba.

4. Habari hii ya CDF ina corroborate habari ya Makamba kwamba Ofisi ya Makamu wa Rais ilitengwa.

Sasa unataka kukataa maneno ya CDF kwamba kuna watu walitakankupindisha katiba Makamu wa Rais asiwe Rais?

Unataka kusema January Makamba kasema uongo mbele ya Rais Samia, Makamu wa Rais na watu wa Ofisi yaje hawakutengwa? Mbona haya mambo tuliyasikia tangu Magufuli yupo hai?

Unachobisha ni kipi hasa?
 
Hii habari kwamba kuna watu walitaka kuipindisha katiba imekuwa verified na watu wengi waliokuwa karibu na center of power wakati huo.

Na kila muda unavyopita na watu kujisikia huru kufunguka tutasikia mengi zaidi.
Na nahisi mengi yanakuja kwakuwa kama CDF kaongea tumsubiri Na DG na yeye Ataongea tu siku moja au IGP pia Kiufupi hata wale viongozi wa siasa..
Ukweli huwa una tabia moja unatabia ya kukereketa na Unabeba Hatia..
Kwahyo mtu akiusema huona kashusha hatia..
Tusubiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom