Kuzorota kwa mambo nchini, ni uwezo mdogo wa kuongoza au anatengenezewa mlango wa kutokea 2025?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,718
11,708
Kwakweli inastaajabisha namna tunavyopiga hatua kurudi nyuma kila kukicha, matatizo tuliyonayo leo tulikwisha anza kuyasahau wakati wa awamu ya Magufuli.

1. Umeme umeshindwa kupatiwa ufumbuzi, kila siku ni excuse zisizo na kichwa wala miguu. Na hilo bwawa linalotegemewa kuleta unafuu inasemekana ni mauzauza matupu huko.

2. Huduma za maji ni vichekesho, yaani DAWASA tangu aondoke Eng. Luhemeja pale mambo yamekuwa hovyo kabisa. Kwasasa kuna mtu wa ICT anakaimu ile nafasi, na kwanamna anavyopigwa chenga ni wazi kuwa viatu havimtoshi. Maji yana wiki kadhaa hayatoki, mtaani yamejaa magari ya kuuza maji, hizi ni biashara za watu wenye mafungamano na DAWASA. Tulikwisha uacha upuuzi huu awamu ya nne, lakini umerudi.

3. Fedha za kigeni zinazidi kuadimika, imefika kipindi sasa kuna soko haramu huko mtaani, unapata dola moja kwa 2800. Soon tutashindwa hata kuagiza mafuta.

4. Sukari ndio usiseme, wazalishaji wa sukari ndio wanaopewa vibali vya kuagiza sukari, yaani sukari inakuwa kama madawa ya kulevya, alafu eti Bashe ambaye ni swahiba wa hilo genge lililohodhi biashara ya sukari ndio waziri wa kilimo, vichekesho hivi.

5. Ukienda kwenye ofisi za umma bila rushwa utateseka sana, yaani ule uadilifu hata wa hofu haupo kabisa, watu wanapiga tu. Sio kwamba vyombo vya usalama hawajui, wanajua jinsi hali ilivyo mbaya, lakini hata kule juu hakujanyooka kabisa hivyo hata wao wanaona bora kila mtu aendelee kula tu.

- Serikali imeshikwa na magenge ya wafanyabiashara, hao ndio washauri wakuu wa mheshimiwa. Nayeye anaamini kabisa hao wanaweza kulinda maslahi ya wananchi. Imefika mahali mpaka mmoja wao anaropoka kuwa apewe nyumba za serikali 100 kule mjini kisha yeye akajenge vibanda vya bei nafuu wapi huko sijui. Mwingine amegeuka TRA ndogo pale bandarini, bila kupitia kwake utataabika sana kama unataka kuagiza mzingo nje ya nchi.

Kwa hali hii, ni either Rais Samia hana uwezo wa kuimudu kazi ya kuongoza nchi labda kutokana na kaliba yake ya upole au anahujumiwa ili kumtengenezea mazingira ya kumwondoa 2025.

Sehemu pekee unaweza kusema Rais Samia amefamya vizuri ni kurejesha siasa za amani na uvumilivu, pamoja na kujaribu kuwatendea watu haki, lakini hiyo pekee haitoshi kumfanya mtu awe kiongozi mkuu wa nchi.

CCM amueni moja, kama 2025 mnayo nia ya dhati ya kwenda na Rais Samia basi msaidieni, mwelezeni ukweli na mpeni ushauri bila kupindisha maneno.
 
Kwakweli inastaajabisha namna tunavyopiga hatua kurudi nyuma kila kukicha, matatizo tuliyonayo leo tulikwisha anza kuyasahau wakati wa awamu ya JPM.

1. Umeme umeshindwa kupatiwa ufumbuzi, kila siku ni excuse zisizo na kichwa wala miguu. Na hilo bwawa linalotegemewa kuleta unafuu inasemekana ni mauzauza matupu huko.

2. Huduma za maji ni vichekesho, yaani DAWASA tangu aondoke Eng. Luhemeja pale mambo yamekuwa hovyo kabisa. Kwasasa kuna mtu wa ICT anakaimu ile nafasi, na kwanamna anavyopigwa chenga ni wazi kuwa viatu havimtoshi. Maji yana wiki kadhaa hayatoki, mtaani yamejaa magari ya kuuza maji, hizi ni biashara za watu wenye mafungamano na DAWASA. Tulikwisha uacha upuuzi huu awamu ya nne, lakini umerudi.

3. Fedha za kigeni zinazidi kuadimika, imefika kipindi sasa kuna soko haramu huko mtaani, unapata dola moja kwa 2800. Soon tutashindwa hata kuagiza mafuta.

4. Sukari ndio usiseme, watemgeneza sukari ndio wanaopewa vibali vya kuagiza sukari, yaani sukari inakuwa kama madawa ya kulevya, alafu eti Bashe ambaye ni swahiba wa hilo genge lililohodhi biashara ya sukari ndio waziri wa kilimo, vichekesho hivi.

5. Ukienda kwenye ofisi za umma bila rushwa utateseka sana, yaani ule uadilifu hata wa hofu haupo kabisa, watu wanapiga tu. Sio kwamba vyombo vya usalama hawajui, wanajua jinsi hali ilivyo mbaya, lakini hata kule juu hakuja nyooka kabisa hivyo hata wao wanaona bora kila mtu aendelee kula tu.

- Serikali imeshikwa na magenge ya wafanyabiashara, hao ndio washauri wakuu wa mheshimiwa. Nayeye anaamini kabisa hao wanaweza kulinda maslahi ya wananchi. Imefika mahali mpaka mmoja wao anaropoka kuwa apewe nyumba za serikali 100 kule mjini kisha yeye akajenge vibanda vya bei nafuu wapi huko sijui. Mwingine amegeuka TRA ndogo pale bandarini, bila kupitia kwake utataabika sana kama unataka kuagiza mzingo nje ya nchi.

Kwa hali hii, ni either SSH hana uwezo wa kuimudu kazi ya kuongoza nchi labda kutokana na kaliba yake ya upole au anahujumuwa ili kumtengenezea mazingira ya kumwondoa 2025.

Sehemu pekee unaweza kusema SSH amefamya vizuri ni kurejesha siasa za amani na uvumilivu, pamoja na kujaribu kuwatendea watu haki, lakini hiyo pekee haitoshi kumfanya mtu awe kiongozi mkuu wa nchi.

CCM amueni moja, kama 2025 mnayo nia ya dhati ya kwenda na SSH basi msaidieni, mwelezeni ukweli na mpeni ushauri bila kupindisha maneno.
Amani na haki uvumilivu ni nini kwako?

Ni haki yako kupata maji, umeme? Wangapi wanakufa kwa kukosa hivi vitu, familia, biashara ngapi zinavunjika kwa kukosa umeme, maji?

UKishambuliwa na panyaroad unarudi nyumbani kuna amani hapo?

Unarudi nyumbani huna pesa kuilisha familia yako kutakuwa na amani?
 
Siasa za amani kwa maana kwamba yale mambo ya CDM wakitaka kufanya mkutano basi polisi wanawakamata viongozi na kuwapa kesi za uchochezi. Angalau kwenye hilo amejitahidi.
 
Huenda ndiyo maana Chadema wanaandamana Mwanza.

R.I.P Magufuli
Siku zinavyozidi kwenda tunazidi kumkumbuka. Alitufumbua macho kuwa tukiamua basi inawezekana.

Kwasasa kiongozi akiwa anavurunda tunayo reference ya kujua kuwa huyu ni mzugaji tu hafai kuwa kiongozi.

Pumzika kwa amani mzalendo JPM.
 
Back
Top Bottom