Inaumiza, inatesa na kuniweka katika majonzi mazito mno

Inaumiza, inatesa na kuniweka katika majonzi mazito mno

Hawa watu ndo wasaidia watoto wetu shuleni!! Sijui watajikwamua vipi kutoka hapo walipo aisee!!!! Maana serikali ndo hii ipo bize kutuuza..... niseme pole sana brother,

Nimeangalia iyo slip yako ni majanga aisee, komaa maliza mkopo huo though ni ngumu! Then kopa pesa ya maana ufanye biashara, lakini kazi usiache nakushauri kazi usiache”

Kama unaweza pia jichoshe zaidi fanya biashara, lakini rudi shule omba kusoma soma mpaka upate masters huu ni mpango wa muda mrefu inaweza kukuchukua miaka hata 5 au 7” ukifanikiwa kumaliza utakuwa na expirience ya muda mrefu, omba kazi sehemu nyingine kimya kimya I hope mungu atakusimamia......

Lakini kubali kutumika na kujichosha kwaajili ya future yako mwenyewe na familia yako” kazi ya baba nikuleta maendeleo kwenye familia, wewe jichoshe ili wanao wapate kile kilicho bora wasije angukia hapa ulipo wewe mkuu.
Hiyo mipango yote kwa hela na muda upi?
 
Abadani sitakuja kuwaonea huruma hawa mbweha mpaka watakapokuja kujitambua na kudai teaching allowance ili iweze kupunguza ukali wao wa maisha

Wakati huku viongozi wakiingia mikataba mibovu ya kubinafsisha bandari ya dar Es salaam nakupiga mabilioni ya pesa huku mwalimu wa shule ya Msingi anahangaika miaka kumi kumaliza deni la payport ambalo kimsingi ni nusu mshahara wa mbunge au waziri.

Walimu mishahara yenu ni midogo sana kama ilivyo Kwa sekta nyingine tu ila shida nyie hamna posho hicho tu, wateja wenu hawana pesa lakini polisi anauwezo wa kupiga patrol mpaka alfajiri hakosi laki Tatu ambayo ndo mshahara wako wa mwezi japo kuwa mnamzidi mpaka polisi ila wao wateja zao (watuhumiwa) ni watu wazima wenye kutoa pesa mfukoni akitengeneza mazingira ya rushwa ila sio nyie Kwa wanafunzi

Mimi ushauri wangu kutokana na iyo salary slip acha kazi tu ufanye maisha mengine maana hapo utakuwa unaaibisha fan huwez kuishi Kwa dolar hamsini hata siku moja. Au mbinu nyingine ya kivita fanya fujo uwe mbishi usiyeelewana na mkuu wako uwe mwanaharakati ili wakutengenezee zengwe wakuhamishe ili upate pesa ya uhamisho hiyo pesa ufanyie miradi vinginevyo hutoboi

Hapo mkuu ngoma ngumu hiyo maana dah ahsee nashindwa nikwambiaje ila nyie walimu kunguru ana uafadhari yani Mnaishi maisha yakifukara chini ya mstari wa umasikini. Mpo kama mapakashumbe
Mpwayungu Village sasa leo ndio nimekuelwa una mantik sema ni vile tu huwa hutumii lugha nzuri.
 
Ipo hivyo maana hata akiwa mbishi, kaidi kufata maelekezo na nimtu wa kuhoji sana Kwa mshahara wake ulivyo wa mbuzi TSC hawana kawaida ya kumpa adhabu ya makato ya mshahara asilimia 15 maana mshahara wenyewe hana Sasa watakata nini kwahiyo watu kama hawa hawawez kukumbana na adhabu yoyote ya mshahara zaidi ya uhamisho. Uhamisho kwake ni advantage maana atalipwa tena ana mke na watoto hakosi million tano mpaka Sita
Kwa hiyo unahisi walimu wamekuwa waelewa mpaka kudai hela ya uhamisho au akipewa barua ya uhamisho anahama bila kulipwa?

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu , Anzisha tuition, amasisha vijana ulinzi shirikishi n.k .. huko dunia ya kwanza ni kawaida mtu kuwa na ajira plus side hustle ata tatu kama kipato hakitoshi,huku kwetu sijui katuroga nani!!!
Pambana hakuna kukata tamaa

Sent from my V2027 using JamiiForums mobile app
Huku kwetu watumishi wa umma hasa walimu wamepigwa ganzi na kudanganywa wajione wao ni watu maalumu ndani ya jamii hivyo wanakuwa wasafi muda wote wakati hawana pesa mfukoni.

Watumishi wa umma wa huku hawapo tayari kupiga vibarua ili wapate pesa ya kula.

Mwalimu ana muda mwingi sana kuanzia saa kumi na jmos & jpili yupo free siku nzima lakini hawataki kufanya kazi za ziada ili apate kipato cha ziada, yeye ni bora aende akakope aandikwe dukani kwa mangi au wachu.

Nawakubali sana polisi wa sasa, ni matajiri vijana. Huwezi kupewa bunduki kufanya doria usiku kucha highway halafu unakuwa maskini!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Huku kwetu watumishi wa umma hasa walimu wamepigwa ganzi na kudanganywa wajione wao ni watu maalumu ndani ya jamii hivyo wanakuwa wasafi muda wote wakati hawana pesa mfukoni.

Watumishi wa umma wa huku hawapo tayari kupiga vibarua ili wapate pesa ya kula.

Mwalimu ana muda mwingi sana kuanzia saa kumi na jmos & jpili yupo free siku nzima lakini hawataki kufanya kazi za ziada ili apate kipato cha ziada, yeye ni bora aende akakope aandikwe dukani kwa mangi au wachu.

Nawakubali sana polisi wa sasa, ni matajiri vijana. Huwezi kupewa bunduki kufanya doria usiku kucha highway halafu unakuwa maskini!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Hhhahaha upo sahihi
 
Duu pole sana huu mshahara nililipwa 2004 nikiwa sina hata familia. Anyway kuna vitu vya kujifunza.
Kabla hujakopa angalia taasisi unayokopa ina sifa gani hata kama haujui kupiga mahesabu ya riba wewe mwenyewe. Lakini taasisi kama Bayport zina sifa mbaya sana ya miriba ya ajabu.
Hakikisha unakuwa na kipato cha ziada kwa njia yoyote ile. Fundisha tuition uza vitu shuleni na mtaani pia. Mashuleni kuna fursa nyingi sana ila waalimu hawatakagi kujiongeza
 
Back
Top Bottom