Nawakumbusha watanzania kuwa ni wabunge wa CCM ndio waliopitisha sheria zote katili na kandamiza kama zile za makato ya Bodi ya Mikopo, Sheria ya kuunganisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Sheria ya kikokotoo kipya kilichozua malalamiko makubwa kutoka kwa umma.
Nilisema jana katika mada yangu hapa JF kuwa wapinzani na wadau wengine tuna wajibu wa kuukumbusha umma wa watanzania juu ya athari za wabunge wa CCM wawapo Bungeni ili kesho wasianze tena kulia kwa watayoyafanya Bungeni.
Watanzania wakumbushwe: Mbunge wa CCM hata akiwa Doctor,Professor,Msanii maarufu,Mchungaji maarufu,n.k, awapo Bungeni huwa hana msaada kwa wananchi zaidi ya kupitisha tu miswaada ya inayoletwa na serikali na zaidi kutetea serikali Bungeni.
Pia,watanzania wajue tu Bunge likitawaliwa na wana-CCM,basi wasishangae Katiba ikabadilishwa na muda wa Uraisi ukaongezwa kama walivyoanza kupiga kampeni katika Bunge lililopita.
Media kwa sasa naona zitajikita zaidi kupamba wabunge wa CCM bila kuwakumbusha perfomance yao; hivyo, na wapinzani mkilalala na watanzania wakasahau yaliyopita,tutakuja kujuta huko mbele.