Inakuaje magazeti haya yanakuwa na kichwa cha habari kinachofanana?

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,783
2,000
Magazeti tofauti, waandishi tofauti kichwa cha habari kinachofanana hadi maneno yalivyoandikwa. Je, mwandishi wa magazeti haya ni mmoja au yanaandika kwa maelekezo kutoka upande fulani?

Mwananchi.jpg

HabariLeo.jpg

Nipashe.jpg

Uhuru.jpg
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,226
2,000
Kila kitu ni mipango, kabla hamjatoa habari yenu lazima muongee na wahariri namna ya kuipa headline habari yenu.

Hela imemwaga hapo kwa wahariri, Nia ni kufifisha habari za Wapinzani ionekane Tanzania kisiasa ni CCM pekee ndio inakubalika.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,364
2,000
Kwa akili yako umeona ni sawa inamaana hujui neno moja tu hubadili maana sentensi.
 

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
577
1,000
Vichwa vya habari huwa vinakaribiana mara nyingi hasa kwenye michezo ambako sidhani kama kuna maelekezo
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,364
2,000
Acha ujinga wewe. Kama hujui kusoma hata picha huoni? Neno kubwa hapo ni MAFURIKO. Wote wamelitumia. JInsi Mafuriko ilivyotumika ni maana iliyofichama siyo maana ya wazi. Tumia angalau akili kidogo. Haiwezi kuwa coincidence

Sent using Jamii Forums mobile app
Mafuriko yamekubeba unaogopa nini kusema kuwa kuwa unaiogopa ccm
 

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,783
2,000
Vichwa vya habari huwa vinakaribiana mara nyingi hasa kwenye michezo ambako sidhani kama kuna maelekezo
Kukaribiana sawa I'll siyo kufanana Kama huko. Labda Kama waandishi waliwasiliana kabla ya kuandika
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,424
2,000
Kila kitu ni mipango, kabla hamjatoa habari yenu lazima muongee na wahariri namna ya kuipa headline habari yenu.

Hela imemwaga hapo kwa wahariri, Nia ni kufifisha habari za Wapinzani ionekane Tanzania kisiasa ni CCM pekee ndio inakubalika.
kama mafuriko ya watu kuchukua fomu yanafanana. Ulitaka vichwa vya habari viwe tofauti? Nani wa kuhonga waandishi kwa Ccm hii inayojitangaza yenyewe.
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,514
2,000
AWAMU HII VYOMBO VYOTE VYA HABARI VINAAMBIWA CHA KUANDIKA. MAGAZETI YOTE YASIYOKUBAKI KUSHIKWA MASIKIO KAMA VILE TANZANIA DAIMA YAMEFUNGIWA. TUPO NDANI YA NCHI YA GIZA NENE INGAWA WATU HAWAJUI NA WANASHANGILIA.

JAMBO LINGINE LINALOFANYA WAGOMBEA WAWE WENGI HASA CCM NI ILE KAULI YA MZEE KWAMBA ASIWEPO MKURUGENZI ATAKAYEMTANGAZA MPINZANI KUWA KASHINDA. WANAJUA WAKISHAPITISHWA NA CCM TU BASI TAYARI NI WABUNGE.
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
3,125
2,000
Acha ujinga wewe. Kama hujui kusoma hata picha huoni? Neno kubwa hapo ni MAFURIKO. Wote wamelitumia. JInsi Mafuriko ilivyotumika ni maana iliyofichama siyo maana ya wazi. Tumia angalau akili kidogo. Haiwezi kuwa coincidence

Hii nchi ipo hapa ilipo sababu ya mapuuz kama huyo jamaa, yan magazeti matano yote yaseme mafuriko ? sio kweli , wapuuz ni weng hapa Tanzania na hayajui kama ni mabogasi
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,098
2,000
Nawakumbusha watanzania kuwa ni wabunge wa CCM ndio waliopitisha sheria zote katili na kandamiza kama zile za makato ya Bodi ya Mikopo, Sheria ya kuunganisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Sheria ya kikokotoo kipya kilichozua malalamiko makubwa kutoka kwa umma.

Nilisema jana katika mada yangu hapa JF kuwa wapinzani na wadau wengine tuna wajibu wa kuukumbusha umma wa watanzania juu ya athari za wabunge wa CCM wawapo Bungeni ili kesho wasianze tena kulia kwa watayoyafanya Bungeni.

Watanzania wakumbushwe: Mbunge wa CCM hata akiwa Doctor,Professor,Msanii maarufu,Mchungaji maarufu,n.k, awapo Bungeni huwa hana msaada kwa wananchi zaidi ya kupitisha tu miswaada ya inayoletwa na serikali na zaidi kutetea serikali Bungeni.

Pia,watanzania wajue tu Bunge likitawaliwa na wana-CCM,basi wasishangae Katiba ikabadilishwa na muda wa Uraisi ukaongezwa kama walivyoanza kupiga kampeni katika Bunge lililopita.

Media kwa sasa naona zitajikita zaidi kupamba wabunge wa CCM bila kuwakumbusha perfomance yao; hivyo, na wapinzani mkilalala na watanzania wakasahau yaliyopita,tutakuja kujuta huko mbele.
 

Haya_Land

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
5,262
2,000
Waache wafanye mafuriko lakin majina yatakayopitishwa tunayo huku ikulu nashangaa watu wanapanga foleni kinondoni kwa Mtulia wakati anayepitishwa anajulikana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom