Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Je, ni mashirika mangapi ya habari Tanzania yana maono kama ya BBC? Maana BBC baada ya kuona mapinduzi makubwa kwenye mawanda ya upashanaji habari na hatari iliyopo mbeleni ya kukosa wasomaji na wasikilizaji wakaja na uamuzi mzito wa kufunga ofisi zao nyingi za kikanda hali iliyopelekea punguzo kubwa la wafanyakazi
Mashirika mengi ya habari kwasasa yanabadilika na kuwekeza mitandaoni zaidi.. Na hili limewafanya wapunguze gharama za uendeshaji na kufikia watu wengi zaidi!
Kwa Tanganyika yetu zile enzi za kuwahisha magazeti mikoani zinakufa..zile enzi za kujikusanya saa 12 jioni ili kupata habari za dunia zinamalizia kukata roho! Zile enzi za kujikusanya saa mbili usiku ili kupata yaliyojiri siku nzima ni kama hazipo tena! Maendeleo makubwa ya teknolojia yameua hayo yote! Sasa hivi hakuna haja ya kusubiri saa saba mchana, saa 12 jioni ama saa mbili usiku kujua kilichojiri nchini na duniani
Sasa hivi huna haja ya kwenda kununua gazeti kuweza kujua yaliyojiri kitaifa na kimataifa! Kila kitu kiko kiganjani kwako kupitia simu janja.. Kwa kifurushi chako cha elfu moja tuu unaweza kujua yaliyojiri duniani kote ndani ya dakika chache kupitia magazeti mitandaoni, habari picha, habari video na makala mbalimbali.. Tena nyingine unazipata kupitia live coverage!
Maendeleo haya yamevuka vikwazo vingi vya mamlaka zinazo control media nyingi kwenye upashanaji habari.. Kupangiwa cha kuandika, kupangiwa cha kuripoti nknk.. Japo kuna shida kidogo kwenye habari za mitandaoni kwakuwa karibu kila mtu ni mwandishi sometimes kuna upotoshaji, uongo, uzushi na hata kutoa habari zisizohaririwa, sanifiwa na kukosa viwango bora vys uandishi
Kuna baadhi waliofanikiwa kuwa waandishi wa mitandaoni kwa kusanifu kazi zao, kutoa habari za uhakika na za kuaminika, kutoa habari kupitia live coverage hawa wana maisha ya mafanikio makubwa mbeleni
Juzi kanisani kwangu niliona kitu kilichonifikirisha mno! Waumini kuuziwa magazeti ya kanisa baada ya ibada.. Zamani yaliwekwa nje na muuzaji na baada ya ibada watu walinunua kwa hiari yao! Siku hizi kwa mtindo huo hayauziki tena!
Haya magazeti yanatoka maramoja kwa wiki.. Imagine kwa ulimwengu wa leo matukio ya Jumapili hii Kanisani ama nje ya kanisa yaje yaripotiwe Jumapili inayofuata kanisani
Natambua dhima ya taasisi za kidini kujaribu kwenda na wakati, nyingi zina vyombo vya habari lakini kwenye ishu ya magazeti (hasa RC na Lutheran) wanafeli pakubwa.. Magazeti yanauzwa kwa lazima na kuna wakati mengi hubaki na kuingiza hasara kwenye taasisi husika. Ni rai yangu wawe na maono makubwa kwenye hili haraka!
Miradi ya uchapishaji magazeti sio miradi yenye tija tena! Miradi ya taarifa za habari kwenye tv na radio nayo inachechemea.. BBC wameona mbali wamegutuka mapema! Vipi wengine?