Ina maana Maxence Melo hana usingizi?

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,830
4,727
Wadau tangu kubadilishwa kwa mwonekano wa JF sijawahi kushuhudia mwanzilishi wa JF Maxence Melo akiwa offline iwe asubuhi, mchana, jioni na hata usiku wa manane.

Kipindi naandika hii post moderators wote walikuwa wamelala lakini yeye yupo online, swali langu ni hili. Je, bwana Maxence Melo hana usingizi? Haoni kuwa anadhoofisha Afya yake kwa kukesha online?

Namaliza kwa kumpongeza kwa kututengenezea hii kitu lakini aangalie namna ya kufanya ili apate muda wa kupumzika.
 
Wengine tukiingia humu ni kusoma nyuzi mbalimbali,Ku comment na kuanzisha nyuzi,kumbe kuna watu mnaangalia mpaka moderators wanalala sangap???vipi Invisible analala sangapi???!!
 
We na Maxence mna tofauti gani?
Maana ni coincidence tu kwamba akiwa online na wewe unakuwa online akiwa offline na wewe uko offline.

Kwanza hilo swali unatakiwa uulizwe wewe (Huna usingizi hadi kushindana kukesha online na moderator ambaye yeye yupo kazini?)
 
Sijuti,

Wewe utakuwa jipu tu, unawapekua mods ili kama wamelala upost. Sasa hivi hakuna kulala.

Hilo donge na wivu vitakupoteza. Usiwatafute watu usiku, iko siku yatakukuta.
 
duh! inawezekana halali kweli maana ukifuatilia hii thread utagundua kitu kwenye post alizo like.
4 hours ago
3 hours ago
an hour ago
 
Wadau tangu kubadilishwa kwa mwonekano wa JF sijawahi kushuhudia mwanzilishi wa JF Maxence Melo akiwa offline iwe asubuhi, mchana, jioni na hata usiku wa manane.

Kipindi naandika hii post moderators wote walikuwa wamelala lakini yeye yupo online, swali langu ni hili. Je, bwana Maxence Melo hana usingizi? Haoni kuwa anadhoofisha Afya yake kwa kukesha online?

Namaliza kwa kumpongeza kwa kututengenezea hii kitu lakini aangalie namna ya kufanya ili apate muda wa kupumzika.
Sio kwamba huwa halog out? unaweza kuwa on line lakini ukawa umelala hasa wale wanao tumia Apps.
 
Back
Top Bottom