Kusainiwa mkataba DP World na bandari haikuwa siri

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, amesema utiaji saini Mikataba Mahsusi ya Uwekezaji na Uendeshaji wa sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam, baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma October 22, 2023, haikuwa ni jambo la siri.

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam, Matinyi amenukuliwa akisema “Nianze na swali la John Marwa kwamba kulikuwa na usiri kwenye shughuli ya kusaini mkataba (Na kwamba kuna waliofika eneo la tukio bila kuambiwa kulikuwa na jambo lipi) , hakukuwa na siri, Watu walipewa mialiko wakiwemo Waandishi ambao walipewa na usafiri kutoka katikati ya Jiji hadi Chamwino na kuwarudisha, walialikwa Viongozi wa Siasa wa CCM na Upinzani, Wazee wametoka Zanzibar wengine, Viongozi wa Dini na Watendaji mbalimbali wa Serikali, halikuwa tukio la siri na TV na Radio zilirusha LIVE matangazo”

“Walikuwepo Waandishi wa mitandao mbalimbali ya kijamii Mimi nilizungumza nao wengine wakanihoji, hotuba ya Mkurugenzi wa TPA ilieleza vitu kwa upana na urefu unaweza kurudi Youtube ukaisikiliza, hakukuwa na kitu cha kuficha, Rais alizungumza, Makamu wa Rais alizungumza na Watu wa DP World walizungumza , hakukuwa na usiri”

“Sina uhakika kama hata kama umekwenda pale haukujua umealikwa kwa kitu gani kwamba utasema kulikuwa na usiri kwasababu umekiona ulichokiona, sidhani kama hiyo inatosha kusema jambo lilikuwa la siri kwasababu limewekwa wazi na kila Mtu ameliona”

Millard Ayo
 
Back
Top Bottom