Mkuu... nilivyoona hii headline nimesikitika sana.Wakati huo ukisoma gazet la habari Leo linasema ""hali ya uchumi Tanzania ni nzuri"""
Inasikitisha sana Mkuu.Binafsi nashindwa kabisa kuwaelewa wanhabari wetu... taharifa hii kwenye Habari leo imeelezwa eti "uchumi wa tanzania upo vizuri" kwenye magazeti mengine imetajwa hivyo kuwa "IMF yaonya mwenendo wa uchumi" sasa sijui tunafeli wapi? tafsiri ya hii lugha inatusumbua au nini hasa tatizo kwa wahariri wetu hawa..?
Hapa nawasubiri wasomi wa uchumi hewa
Wanaweza kuwa wapiga dili ila kama sio wapiga dili tutaona wskisema ukweli maana mpiga dili anaogopa kutumbuliwaWasomi wote wa uchumi wamejificha uvunguni wanaogopa kumwambia ukweli JPM. Nchi inaongozwa kwa woga na hofu kubwa. Mfalme yuko uchi nyeti zinaning'inia lakini wapambe wanamwambia amependeza sana.
We have a long way to go!!!!
Magazeti ya kitanzania wameandika kinafiki na kupunguza makali ili kuifanya hiyo habari isiwe nzito.
Mkuu nimesoma mwananchi jinsi walivyoandika kama vile ni habari fulani iliyopo mbali sana.Mficha MARADHI kifo kitamwumbua!Huu ni umbuni wa kipuuzi. Unaficha kichwa kwenye mchanga ilhali kiwiliwili chote kiko njenje. Kweli utawala huu ni shida.
Uchumi utakuwa kwa kasi kubwa sana, baadae. Hali hii inayoonekana sasa ni kweli, sababu tupo kwenye mabadiliko. Pesa zinatoka kwa wachache kwenda kwa wengi. Yaani, huduma zinapelekwa kwa jamii.
Kuhamia Dodoma ndio kuta push hata mikoani kutakuwa na ungezeko la uchumi. Dodoma ni katikati ya Tanzania na from Dodoma co-ordinations zitawezekana kwenda pande zote hata mpaka Chato na Kilimanjaro, Kenya na Yuganda, Malawi hadi Rwanda na Ulaya, India na Venezuela hadi kwa Trump tutashirikiana nao yaani toka huko Idodomya, Tanzania.
Tusiogope Watanzania, mambo ndio yameanza tu majuzi juzi. MUNGU aliumba Dunia kwa siku saba, hadi sasa matekenolojia yanaendelea kuumbikaga. Sasa na hii Selikali yetu pia itafanyaga uchumi wetu ku progressigi. Tuna gas, tuna madini na makampuni yake, tuna vifaru na wanyama kibao, tuna ardhi tena ya kijani, mvua ndio ameanza kunyeshaga. Mamito ya maji, maziwa hadi Bikitoria, masamake. Utajiri wote huo wajameni.
Angalizo: Tuji control tuwe na population ndogo ndio tunaweza kujimudu. Sasa watu tunaongezeka kwa haraka hapo ndipo tutakosa kujiendesha na uchume utadodora mwana wane. Too muchi is harmufulu.
Angalieni tu musinitukane mie.
Haya Bana. sitashangaa wakija akina fulani hapa kukanusha hali mbaya ya Uchumi Tanzania na hata kuituhumu IMF kuwa ni WACHOCHEZI 🙁
Huyo waziri sijawahi kumuelewa.Hakuna mdororo wa uchumi~Mpango