Imetokea...ingekuwa wewe mdada ungefanyaje?

sweetdada

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
517
169
Natanguliza salamu kwa wote wapendwa..

kuna kisa kimetokea kimenifanya niamshwe usiku wa manane na kuniharibia usingizi.
nahitaji maoni yenu wadada, ingetokea kwako ungefanyaje?

kisa chenyewe kinaenda namna hii:

Kaka kampigia simu mpenzi wake mida ya sa moja jana usiku, wameongea kisha akamuuliza uko wapi?binti akajibu, niko mwenge nimekuja salon..
kaka:hee!kwani nyumbani hakuna salon?
binti:zipo ila huku ndo nimepazoea,sa hivi ndo naondoka nikapande bus,kaka:aa we bwana kwani huoni shida lakini mi sikuelewi,
binti:nipeleke basi home honey
kaka: aa na hizi foleni mi siwezi ila ningekupeleka

Basi mdada akapanda basi akafika home salama imefika saa tatu mkaka hata kumpigia kuuliza kama alifika salama..mdada akaamua kumpigia...kuanzia saa tatu simu iko engaged yani anaongea na simu mpaka saa nne na madakika ndo akapatikana..

dada akakasirika na kuanza kufoka alikuwa anaongea na nani more than an hour kama si mwanamke, "hata hujali kama nimefika we kwenye simu tuuu blablablabla" kibao mdada zikamtoka kumshutumu mwenzake anaongea na mwanamke kwenye simu,

mkaka akajitetea alikuwa amelala hata hakutumia simu yani hajui ni kwa nini simu ilikuwa engaged na kuendelea kuwa labda mitambo au blackberry inasumbu...lol

sasa bi dada akanipigia simu usiku analalamika afanyeje mwanaume ana mwanamke mwingine wanaongea lisaa kwenye simu...

kwa kuwa mi sio mzuri kwenye maushauri ya mapenzi, mana mie mwenyewe yashanishinda,nikamwambia asubiri nitamjibu ..

sasa nalileta swali kwenu wadada wa MMU..ingekuwa wewe ungereact vipi??
 
Kumbe ni wadada tu ndio wanatakiwa watoe mawazo? Najiweka pembeni.....
 
Huyo mdada ana miaka mingapi? wivu wa kitoto huo kwani ye hawezi pigiwa simu hata na shost wake akaongea muda mrefu? mwambie aache utoto
 
kuna watu bwana yaani hata kwenda toilet lazima aombe ushauri....kupeleka hela banka lazimaaombe ushauri...amefika kitua cha basi na analiona daladala liko pale na liko tupu lakini bado ataomba ushauri..'''unaonaje nipande hii?!!! yaani huu huwa nashangaa sana humu ndani.....mleta mada yaani na wewe baada ya kuambiwa hivyo kwa akili ya haraka tu na wewe ukafikir yule bwana kuonage na simu kwa lisaa lizima basi hapo ni mwanamke mwingine?!!!!
 
nimejaribu kumwelewesha lakini mwenzangu anasisitiza haiwezekani aongee na mwanaume mwenzake for that long
nikaona nisiendelee kupoteza usingizi nikamwambia nitakujibu
ndo kisa cha kuuliza may be kuna mwenye mtazamo kama wake
 
Usimruhusu tena akupotezee usingizi wako kwa sababu ya habari za simu. Hizi simu akiziendekeza atishia kupata ugonjwa wa moyo.
 
nimejaribu kumwelewesha lakini mwenzangu anasisitiza haiwezekani aongee na mwanaume mwenzake for that long
nikaona nisiendelee kupoteza usingizi nikamwambia nitakujibu
ndo kisa cha kuuliza may be kuna mwenye mtazamo kama wake

Kama ingekuwa kuongea na simu muda mrefu ni kosa nalo basi ningekua naachika kila iendayo leo
 
Mwambie ni kweli, ana mpenzi, hivyo aondoke, afungashe akatafute mwingine
 
Mwambie ni kweli, ana mpenzi, hivyo aondoke, afungashe akatafute mwingine

hahahhaha mbavu zangu..atakufa kabisa..
tatizo la shosti wangu huyu anatamani hata angekuwa anambeba huyo BF mgongoni
ni makelelee tuu all the time.mpaka mwanaume keshamwambia kuwa umezidi kutoniamini ila haachi
 
Wadada wengine bwana...mwambie bado mdogo sana kwa mapenzi...asubiri akue kue kidogo ila hata wivu wake uwe wa kiutu uzima!
 
bdada ashazoea nja anapenda za heii beby....beb umefika?umekula.....umejamba??
kwan kuanza yeye kumwambia chalii angu mi ndo nimetimba kwa home apa ...inakua kwere?au mpk uanzwe?

na km kuongea na cm asi poa tu angemwuliza taratibu lakinj siyo kisa cha kununa mpk manyonya yanakunyonyoka mdomon...!!!1

ahh mapenz utoto haya ......lakin kwa upande mwngne iz ni swaga za kiume za ..ULIKUA UNAONGEA NANAN DK 10 NZIMA?
....mapeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeenz mapeeeeeeeeeeeeeeeenz......naenda kwa supu mie njaa io!!!!!1
 
kuna wakati mwingine mitandao ya simu inakuwa na shida
Mweleze aacha wivu na kelele nyingi aonge naye waelewane
 
Ngoja nitoe 2 ushauri japokua mi si bi dada.mwambie aache ushamba jana tigo ilikua inasumbua tokea around saa 1 hv mpk saa 6 tigo uilikua haingii vocha,haitoki wala cm haitoki Ukipiga unaambiwa "no. bisy" mwenyewe jana nusu uchumba upoteze network hiv hiv!! sema kw kuwa mi ni creator nikampgia kw airtel .....mwambie aulize wa2 walo2mia simu jana ucku watamwambia
 
Ngoja nitoe 2 ushauri japokua mi si bi dada.mwambie aache ushamba jana tigo ilikua inasumbua tokea around saa 1 hv mpk saa 6 tigo uilikua haingii vocha,haitoki wala haiingii unaambia "no. bisy" mwenyewe jana nusu uchumba upoteze network hiv hiv!! sema kw kuwa mi ni creator nikampgia kw airtel .....mwambie aulize wa2 walo2mia simu jana ucku watamwambia

huyo bwana ake anatumia zantel..nayo pia ilikuwa na tatizo?
swali langu la kwanza kumuuliza lilikuwa ni hilo kuwa anatumia mtandano gani?akasema zantel
mie sijui kuhusu huo mtandao so nikashut
 
huyo bwana ake anatumia zantel..nayo pia ilikuwa na tatizo?
swali langu la kwanza kumuuliza lilikuwa ni hilo kuwa anatumia mtandano gani?akasema zantel
mie sijui kuhusu huo mtandao so nikashut

Mabig ....mi mwenyewe mgeni!! labda 2waachie wadada km ulivyosema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom