Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Discussion in 'JF Doctor' started by BLUE BALAA, Mar 9, 2011.

 1. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  JAMANI NIPELEKE WAPI HAYA MALALAMIKO?
  Naandika hii post nikiwa na uchungu mkubwa sana kwani ndionimetokea West Kilimanjaro kumzika mjukuu wangu aliekuwa na umri wa miezi sita. Hakika huyu malaika hakustahili kutoweka mapema hivi ila ni kwasababu tu ya uzembe wa manesi na madaktari.
  Mnamo saa saba na robo hivi usiku nilishuhudia malaika huyu (Dorris) akikata roho hodini katika hospitali ya Levolosi Arusha ambako ndio ward ya watoto wa Mt Meru ilipo. Dorris alifikishwa hospitalini hapo mnamo saa 5 kamili usiku na alipopimwa aligundulika kuwa anaumwa na Pnewmonia which also triggered her sugar mpaka kufikia 19. Alichomwa sindano, akawekewa oxygen na wauguzi wakaendelea na shughuli zao. Dorris alijatahidi sana kutetea uhai wake kwa takribani masaa mawili tukiwa mimi na mama yake (mkwe wangu) tunamkodolea macho kwani hatukuwa na la kufanya. Basi ilipotimia saa saba na robo mjukuu wangu alivuta pumpzi yake ya mwisho akiwa mikononi mwa mama yake namimi nikiwa pembeni. Hakukuwa na Nurse wala Daktari.
  THE WHOLE SCENARIO:
  1. Dorris alianza kuugua nyumbani mnamo majira ya saa 1 usiku na kupelekwa private hospital maeneo ya kaloleni (Arusha) inayoitwa Eben Hospital. Daktari aliyekuwepo zamu alimpima na akasema hana ugonjwa wowote. Lakini cha kushangaza akampa vichupa vitatu vya dawa alivyowatoza shs 30,000 halafu akamwambia mama yake Dorris ampeleke mtoto kwa Dr Mohamed Hospital iliyopo tank la maji. Kama hana ugonjwa kwanini ampe dawa na kum refer kwenda hospitali nyingine?
  2. Mama Dorris na mototo walifika kwa Dr Mohamed majira ya saa nne usiku hivi. Walivyofika hospitalini hapo, wauguzi hawakujali kuwapokea wala kuwasikiliza isipokuwa walimwambia mama Dorris ampeleke mototo Mt Meru Hospital kwasababu wao wana wangonjwa wengi sana. Mama Dorris aliondoka na mototo wake kuelekea Mt Meru Hospital.
  3. Walifika Mt Meru Hospital mnamo saa nne na nusu na kupokelewa na Dr Longdare ambaye ndio alikuwa Daktari wa zamu. Dr Longdare hakuwapatia huduma yoyote zidi ya kumwambia mama Dorris kwamba idara ya watoto imehamishiwa Levolosi hivyo ammpeleke mototo huko. Mama Dorris ndo akanipigia simu na tukakutana Levolosi. N.B. Baba yake Dorris ni mototo wangu anaefanya kazi mbuga za wanyama hivyo siku hiyo alikuwa mbugani.

  MALALAMIKO
  1. Kwanini Daktari wa Eben akasema Dorris hana matatizo yoyote na kisha kum refer kwenye hospitali nyingine huku akiwa amemcharge shs 30,000?
  2. Kwanini Dr Longdare wa Mt Meru hospital haku treat issue ya Dorris kama emergency na ampe matibabu pale pale Mt Meru badala ya kupoteza muda na motto kukimbia kwenye idara ya watoto?
  3. Kwanini ma nurse wa Levolosi hawakuendelea na jitahada za kuokoa maisha ya Dorris ila walichofanya ni ushahidi tu wakumchoma sindano na kumuwekea oxygen na kisha kwenda kukaa zao ofisi. Nilitegemea mgonjwa mahututi kama huyu angefariki manasi wakiwa wanhangaika huku na kule lakini kwa Dorris ni kinyume kwani kafariki akiwa mikononi mwa mama yake na mimi peke yangu nikiwa pembeni.
  4. Baada ya mototo kufariki nikaomba kama naweza pewa mwili ili niupeleke mortuary. Waliniambia kuna gari ya hospitali ndio itakao upeleka mwili wa mototo. Nilisubiri kuanzia saa saba ile mpaka saa 10 za usiku gari haikutokea ndio mwishowe wakaamua kuniruhusu niuchukue mwili wa mjukuu wangu.
  5. Tukiwa Levolosi baada ya mototo kufariki mama Dorris alipatwa na uchungu sana na ilimpelekea kuzirai mara tatu. Cha ajabu mama Dorris alipozirai alikuwa anahudumiwa na wagonjwa wenzake na siyo ma Nurse.

  SAFARI YA MT MERU HOSPITAL/MORTUARY
  1. Tulifika mortuary saa kumi na nusu, tuligonga mpaka saa kumi na moja kasorobo lakini hapakufungukiwa. Wakati huo mkwe wangu mama Dorris yuko kwenye gari amezimia tena.
  2. Ilibidi nitoke kuelekea main building ya Mt Meru na nilipofika mapokezi nikamkuta Dr Longdare akiwa amekaa so relaxed pale reception ni kikombe chake cha chai. Nikamwambia nina shida mbili kama ifuatavyo.
  Ø Nina motto amefariki hivyo nataka kumpeleka mortuary, hii alinipa maelekezo na nikasaidiwa
  Ø Pili mama wa marehemu yuko kwenye amezimia hivyo ninaomba apatiwe matibabu. Dr Longdare huku akiwa pale pale mapokezi na kikombe chake cha chai akasema “aaaaaaaaaaaaaaaa huyu mpeleke tu nyumabi bwana”. Nikamwambia hapana amesha zimia mara tatu akasema “ aaaaaaaaaaaaa kwani kuzimia ni nini bwana? Kweli at that stage I had to lose temper and I asked him what the hell he was doing there. Cha kushangaza aka charge na kuniambia “You must be mother ****er” – imagine loudly. Infact I didn’t know what he meant. Basi baada ya kucharge sana akaniambia mchukue mgonjwa wako mpeleke kule (waliko manesi)
  3. Mama Dorris alikuwa amezimia hivyo nilikuwa nahitaji msaada, nilipoenda kwenye chumba cha ma Nurse kuwaomba msaada wakanielekeza sehemu ilipo wheelchair ili nikamlete mgonjwa. Muda wote huo mkwe wangu alikuwa kwenye gari. Nikaendesha wheelchair mwenyewe nikaenda kwenye gari na kuanza kumbeba mama Dorris. Mungu saidia kukatokea watu walioleta wagonjwa wao hivyo walinisaidia kumteremsha mama Dorris na kumpeleka ndani. Note for all that time Dr Longdare was in the same place enjoying his cup of tea.
  4. Wakati nampeleka mama Dorris ndani napishana na Nurse mwingine. Nikijua angenisaidia ila aliishia kunikejeli na kusema “Hivi ni nini tena? Nyie hamkwenda Loliondo? Sikumjibu nikaendelea kumsukuma mama Dorris kwenye wheelchair
  5. Finally Dr Longdare akaja, akampima mama Dorris na kumuwekea drip mbili mpaka saa moja asubuhi? Je kama hakuwa mgonjwa kwanini alimuwekea drip? Yeye alisema nimpeleke nyumbani?

  Bye: Blue Balaa.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu. Malaika wetu yuko peponi amepumzika. Poleni sana.

  [​IMG]
   
 3. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Thanks Bubu.
   
 4. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  It is really sad..pole sana... i think if you have the resources within the family, it would be right to sue all those involved for medical malpractice/ negligence ili iwe fundisho kwa jamii na pia kuepusha maisha ya watoto wengine.

  Inauma sana

  God Rest little Angels soul in peace!
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  [​IMG]Rest in Peace our Angel Dorris![​IMG]
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Imeniuma halafu nimekereka kwa jinsi ulivyokuwa treated, Pole sana ndugu na zaidi hongera kwa uvumilivu uliokuwa nao...
  Yaani huyo Malaika amefariki kwa uzembe wa hao Mafedhuli na bado wakawa wanakukejali??????????????

  God Bless Tanzania.

  Inauma kwa kweli..
   
 7. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani pole sana
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  rest in peace Doris. Its so sad. Kwanza blue.. Huyo dr longdare ni mwafrica ama mzungu?
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni mswahili aisee, Longdare huwa ni wamasai wa maeneo ya Shangarai hapa Arusha.
   
 10. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Thanks alot,
   
 11. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asaante sana ndugu yangu
   
 12. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana BLue Balaa, Mungu amlaze malaika wake mahali pema peponi.


  Nimepatwa na uchungu sana kwani nimekumbuka mtoto wangu alipokuwa na mwaka mmoja na nusu alipatwa na pnemonia pia.


  Mungu hawape nguvu na i hope kuna uwezekano wa kuwajibisha hawa wauguzi wetu kwani wamezidi kudharau wagonjwa sana.
   
 13. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Pole sana tena sana kwa matatizo hayo uliyopata na mwenyezi mungu amrehemu mtoto

  Pia kama itakuwa possible naomba nitumie kwenye Private messeg details kamili za huyo doctor, na pia naomba nitumie na majina ya hao ma nurse kama unawajua...Na kama utakuwa unaingia humu ndani mara kwa mara basi nitakupa feedback zaidi....maana walivyofanya sio vizuri kabisa na ni uzembe mkubwa wamefanya....Na je ulivyoenda uliandikishwa kwenye kitabu??Weka more details zaidi.....
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  du, basi nimechoka .. Kwa sababu wazungu ndio mara nyingi huwaga na madharau lakini kama ni mswahili kama sisis basi Mungu si athuman..huyo mmasai naweza kusema kuwa kwa vile kakaa hapo hospitalin mda mrefu basi anachukulia mambo yote easy , hajali kuwa kapewa mustakabali wa kuokoa maisha ya watu. Kama yeye ni dr, basi asisahau kuwa Mungu ndie kamsaidia hadi kawa pale na na anything can happen to him also but simuombei mabaya kabisa ila nawaomba wengine wenye hulka kama hii wabadilike na tuwe na utu.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  mkuu nitapingana na hatua yoyote unayotaka kuwachukulia hawa watu zaidi tu ya kwenda kuwashauri.kwa sababu i hope wapo wachache pale so mkiwafukuza huduma haitakuwepo tena , but kawa madokta wapo wengi ,ok hamna shida
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Inauma sana. Nilishasema Watanzania tunajifanya tuna upendo lakini hatuna ubinadamu kabisa. Hasa huko makazini. Pole sana mkuu. RIP Doris.
   
 17. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu umesoma mwanzo mwisho hiyo habari aliyoandika huyu mama??I mean umesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho???Je ungekuwa ndio wewe imekutokea ungesema kwamba wapo kidogo??inauma sana mkuu so lazima tuangalie na matatizo ya raia pia....
   
 18. Wed

  Wed JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60

  Hii story imeniuma sana. Pole sana Mkuu. Wewe pamoja na familia yako yote mko pamoja nami katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha mjukuu Doris. ......May her soul rest in peace - Amen
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Mwisho wa taarifa yako nimejikuta natoa machozi kwa sababu kuu mbili,

  1. Nimemuhurumia malaika ambaye roho yake imetoweka kwa sababu tu ya uzembe wa watoa huduma.
  2. Hii imenikumbusha kifo cha Mama yangu mzazi ambacho lilitokea pale muhimbili mwaka 2000 kwa uzembe wa ma nurse kwa mtindo huo huo. Pamoja na kununua dawa kama alivyoshauri daktari, manesi hawakuwa tayari kumuwekea dripu na kumpa hizo dawa kama walivyoelekezwa na daktari. Hii ilinifanya niwaambie ndugu zangu kwamba endapo nitakuwa mgonjwa ghafula na ikabidi nipelekwe hospital, basi kuliko kunipeleka kwenye hospitali yoyote ya serikali hapa Dar, basi ni bora waniache nifie ndani!!!!

  Pole sana mkuu wa kumpoteza mjukuu wako kwa uzembe wa watoa huduma.

  Tiba
   
 20. L

  LAT JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  God loves us but loves Dorris more than us ..... almighty god rest her soul in eternal piece
   
Loading...