Imeniuma nikishuhudia mjukuu wangu akikata roho

Yes I agree with you, he must make a follow up and take them to the court for medical malpractice.
It is really sad..pole sana... I think if you have the resources within the family, it would be right to sue all those involved for medical malpractice/ negligence ili iwe fundisho kwa jamii na pia kuepusha maisha ya watoto wengine.

Inauma sana

God Rest little Angels soul in peace!
 
mhhh nimebaki na kigugumizi,poleni wafiwa bwana alitoa na bwana ametwaa.
 
Pole sana kwa kufiwa na mjukuu, nadhani kila mtu angekuwa kwenye viatu vyako angefeel the same.
Hata hivyo katika maelezo yako inaonekana umewalaumu sana madaktari na wauguzi, nakubali hii ni haki yako, na hapa naomba nieleweke sina nia ya kutetea wafanyakazi wa afya ambao ni wazembe. Katika huu mkasa wapo ambao nadhani walitimiza majukumu yao na wapo ambao kwa kweli hakutimiza majukumu yao.

Kwanza napata wasiwasi kama mtoto alianza kuumwa ghafla saa moja na akawa serious au aliumwa before lakini akatibiwa nyumbani mpaka alipozidiwa ndipo akapelekwa hospitali (hili hujatuambia). Tunaweza tukawalaumu wahudumu kumbe mtoto alipelekwa akiwa serious sana na matibabu yakwa magumu. Kwa ufahamu wangu, pneumonia ambayo huua haraka sana ni aspiration pneumonia (ile ambayo maji au kimiminika kinaingia kwenye njia ya hewa mpaka kwenye mapafu na kusababisha hii aina ya pneumonia), lakini pneumonia za uambukizo wa vimelea (bacterial, viral, au hata fungal) huanza taratibu (sometimes viral can be acute) na mtoto asipotibiwa tangu anapoanza kuonyesha dalili kama homa, kukohoa nk.,anaweza kupoteza maisha, wasi wasi wangu ni kwamba labda Doris (RIP) alianza kuumwa mapema na labda alitibiwa nyumbani kwanza kabla ya kufikishwa hospitali (kama desturi zetu) na alipozidiwa ndipo akapelekwa hospitali (unaweza kunirekebisha), watoto wadogo wako delicate sana, unapoona dalili yoyote isiyo ya kawaida usimpe syrup tafadhali mkimbize hospitali haraka.

Huyo daktari wa kwanza japo hakusema mtoto anaumwa nini lakini kitendo cha kumpa referral si cha kubezwa, labda aliona mtoto ana ugojwa ambao asingependa ku-reveal mbele yenu kwa kuogopa kuwapa shock, na kwa kuwa yeye hakuweza kuwatibu akaona awape referral, ninachomlaumu mimi ni hiyo consultation charge ya 30,000/-, ilikuwa kubwa mno.

Wale nurses wa levolos nadhani walitimiza majukumu yao, daktari akiandika weka oxygen and give drugs wanafanya, na walifanya, na kwa uhaba wa manesi sio rahasi wakawa wanakaa kwa mgonjwa mmoja full time kama hawana kitu kingine cha kuoffer zaidi ya prescribed management, wakati unakuta nurse yupo mmoja na ward attendant wake wanahudumia wagonjwa kati ya 40 na 70, (sijui load kwa wakati huo ilikuwa kubwa kiasi gani) inakuwa ngumu kuwa na mgonjwa mmoja muda wote, cha msingi walimpatia matibabu (ambayao naamini zilikuwa ni antibiotics na oxygen which is the recomended treatment for severe pneumonia) bahati mbaya hayakumsaidia. Labda wakati mtoto ana-gasp wlitakiwa wawepo wafanye resuscitation ingawa sio 100% successful lakini huwa inaokoa maisha ya baadhi ya wagonjwa. Na saa nyingine hata vitendea kazi havipo, unakuta mgonjwa anatakiwa apate oxygen, hospitali nzima ina oxygen cylinder moja, hapo mfanyakazi hata kama una moyo wa kusaidia mtu unafanyaje? Hospitali haina nyuzi au dawa za usingizi unafanyaje operation? Hapa lazima serikali itimize wajibu wake, vifaa na wafanyakazi jamani hawatoshi, tukiendelea hivi tutapoteza maisha hata pale ambapo hatukustaili kuyapoteza.

Huyo daktari Longdare hakuwa na lugha nzuri sijapenda, Katika mkasa wote kwa mtazamo wangu huyu ndie ambae hakutimiza majukumu yake na anapaswa aadhibiwe.

Poleni sana kwa msiba Mungu awatie nguvu.
 
Pole sana kaka!!!
Hii dunia bwana!!!
RIP Dorris
 
Ndugu yangu Pole saana, nashindwa kuelewa watanzania tunaelekea wapi? lakini kama kuna uwezekano hawa watu watu wanatakiwa wawajibishwe iliwajue watendayo siyo nikinyume na maadili ya kazi yao.
 
Pole jamani inasikitisha sana,Mungu awape nguvu katika hiki kipindi kigumu.
Mambo mengi tumekuwa tukiyaona kama ni mpango wa Mungu iwe hivyo lakini si kweli kabisa,watanzania tunasema tuna upendo na ukarimu lakini si kweli wengi katika sekta ya Afya wamekaa kibiashara zaidi na kutokuwa na utu kama huna mtu unayemfahamu wala pesa basi ndiyo ujue maisha kwako yamekwisha.
Ifike mahali pa kuwawajibisha hawa wahudumu wa Afya ili iwe funzo kwa wengine,maana wameona ni haki ya mtu kufa tu kwa uzembe ,kama aliona hiyo fani haimfai ni bora wangeenda kuchimba madini Mererani huko ndiyo wakafanye ukatili kweny emiamba na si miili ya watu
POLENI SANA NA MUNGU AMPE NGUVU MKWEO NA DOREEN APUMZIKE KWA AMANI
 
Pole sana,angalia uwezekano wakushtaki Medical board wastuke kidogo kwamba watu wote sio mabwege.Mimi nliwahi kukomaa nao ikaonekana tiba aliopewa mtoto haikuwa sahihi na hatua za nidhamu kuchukuliwa.
 
Kwanza pole sanaaaa.

Pili, nenda tu kafungue mashitaka rasmi na wakichunguzwa itaonekana uzembe uliofanyika na itakuwa fundisho kwa wote. Juzi Dr amemchoma sindano jamaa yetu akafa hapohapo, sindano wala haina sababu, basi tu. Bahati yao sikuwepo na waliokuwepo waliona - kazi ya Mungu haina makosa (kama wanavyosema wao). Please dont let this pass... Anza na huyo Longdare, hao watu wana miiko yao na taratibu zao, washitaki.

Asante sana, najipanga ili nifanye hivyo. Some one must be responsible
 
Pole sana ndugu yangu, umenikumbusha nilivoshuhudia bi mkubwa wangu akizidiwa usiku wa manane na hospitali ya AICC Arusha na manesi wakamchoma dawa ya usingizi ili asiwapigie kelele badala ya kutafuta chanzo cha mgonjwa kupiga kelele, kumbe ilikuwa malaria chronic, hakupatiwa vipimo vyovyote hapo AICC, kutokana na dawa ile waliyomchoma, alipoteza fahamu, kukaa kwenye koma wiki mbili na kufariki hospitali ya KCMC. Madaktari KCMC walidai alikuwa na malaria kali sana na shinikizo la damu. Inaniuma hadi leo na nimetokea kuichukia sana ile hospitali. Tuwe makini na hospitali za Arusha.

Yote mwachie Mungu na Time heals the pains, pole pole sana, najua unavyojisikia.

May out little angel Dorice RIP.

Asante sana, AICC ndio hapafai kabisa ILA niko tayari kuuza shamba kupambana nao
 
Wala usijali mkuu hata haya maelezo uliyotoa yanatosha sana hamna noma mkuu...tupo pamoja na hili swala linashughulikiwa wala usijali....zaidi sasa hivi endeleza maombezi kama kawaida....

Again pole sana....

Asante sana Papizo, nitashukuru sana mkubwa
 
978.gif
Pole sana na familia yote. Thread imenitoa machozi.
May our little angel Dorris rest in peace.[/QUOTE]

Thanks mpendwa, my lovely Dorris is no more
 
Pole sana Blue Balaa na MUNGU muweza yote awape moyo wa uvumilivu.
Tatizo ulilokumbana nalo ni tatizo linalotukumba wengi si Arusha tu bali Tanzania nzima. imefika wakati watoa huduma wanaitoa kwa mazoea badala ya kutumia taaluma zao. hili ni tatizo la system nzima katika serikali na idara zake. lakini inapofikia hata hospitali binafsi nazo zinaingia kwenye mkumbo huo huo basi maisha yetu yapo hatarini sana.
Ndiyo maana mimi sishangai na sintashangaa kuona watu kwa maelfu wakikimbilia Loliondo kwa Babu ili kupata tiba isiyo na masharti na inayotolewa kwa moyo wa huruma na wenye kujenga matumaini mapya kwa wagonjwa.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DORRIS MAHALI PEMA PEPONI, AMINA.

You are very right, life as usual ndio inatuketea matatizo yote. Thanks
 
Pole sana Mkuu. Huu ni uzembe mkubwa ambao umekithiri sehemu zote za huduma za wananchi. Ni wengi sana wamefariki kutokana na uzembe wa madaktari na manesi lakini hatua zozote hazichukuliwi, ndio maana wao wanaona ni kawaida tu na kutukana watu. Tabia hii imeanzia ngazi za juu za serikali hadi kusambaa katika ngazi zote. Hii ni cancer ambayo itaangamiza taifa hatua zisipochukuliwa mapema.

Asante ndugu na ni kweli wengi wanakufa ambao hawana access na forum kama hizi. So bad
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom