Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,805
- 43,228
Habari za usiku mabibi na mabwana,
Ni wasaa mwingine tena Kasinde kuzungumza nanyi.
Msema ukweli siku zote mpenzi wa Mungu. Mie tangu nijifahamu kuwa ni mschana bin kigori niliyekamilika idara zote, nilikuwa na marafiki wengi wa kiume na kati yao kuna waliokuwa wapenzi. Shida kubwa ya Kasie nilikuwa siwapi nafasi wanaume, muda wote naambatana nao na kugombana nao.
Ugomvi wangu kwao ulikuwa ni tabia ya wanaume kupiga kiwi cha macho pale anapopita mschana aidha awe mrembo au hata wa kawaida tuu ila ananukia uturi wa kuamsha hamasa, basi mwanaume bila kujali mie nipo pale atamtizama yule dada hadi atakoishia tena kwa kushangaa saa ingine hadi kuachama midomo.
Hii kitu ilikuwa inaniudhi inanipa hasira na kunipa wivu.... kwanini amwangalie yule inamaana mimi sio mzuri? Simvutii? Sasa kama anaangalia wengine mi nafanya nini hapa si aniache awafate hao...? Nilikuwa nachukia mno.... (hii ndo ilikuwa dalili kuwa Kasie ni mbinafsi ). Nakumbuka kuna jamaa mmoja ndo ilikuwa mtoko wetu wa 2 tangu tufahamiane na ndo ilikuwa tunawekana sawa ili tufahamiane zaidi. Heee...!!! Katikati ya maongezi si akapita mdada mrembo kiukweli, asipigwe na butwaa nini.....! Nikamstua mara 2 hasikii. Nilinyanyua pochi yangu nikasepa na ndo ikawa mwisho wetu.
Kiukweli nilikuwa sijawaelewa kuwa ile ni kusuuza macho tuu japo saa ingine hupelekea kuosha rungu.
Tangu mwaka jana nikaanza kufanya majaribio ya kuwa nikiwa kwenye migahawa au barabarani nikiona mdada anayevutia au mrembo namtizama kwa umakini. Nilichogundua... kiwi cha macho kitamu na wanaume wanafaidi.
NAMALIZIA NILIPOISHIA JANA.......
Siku hizi nimekuwa addicted na kuangalia wadada, yaani nikipishana na mdada lazima nigeuke kumuangalia nyuma. Au nikiwa kwenye gari najikuta naangalia wadada hasa unakuta wamevaa dera halafu huku nyuma ni maashalaah looh basi ntasindikiza ile dodoma singida na nikimpita namuangalia kwenye side mirror hadi anapotea. Hii ya kwenye foleni imeshanitokea sana yaani inakuwa tumesimama foleni halafu kuna mdada nakuwa namuangala kwa mshangao kuja kustuka napigiwa honi na gari la nyuma kumbe magari yalisharuhusiwa siku nyingi mie nimezubaishwa na kumuangalia mdada.
Nilichokigundua, wakati unaweka umakini kuangalia maungo ya mwanamke ila akiwa amevaa nguo, akili huwa inapumzika na inaburudika au inafurahi. Nimejikuta nimewaelewa sana wanaume na hata ningekuwa kwenye ndoa mwanaume wangu wala asingepata tabu ya mie kukasirika tena kwa yeye kuduwaa kumuangalia mwanamke.
Wengine unakuta hana tako ila ana kashepu ka uchokozi ambako ukimuangalia na nguo aliyoivaa daah unajikuta unazubaa flani hivii huku akili inaburudika hahahahhaaa.
Uzuri wake muda mwingi nakuwa nimevaa miwani tinted na kwenye gari vioo ni tinted hivyo huwa hawanioni sana ninavyopiga kiwi cha macho.
Ila wanaume muda wote huo wanafaidi ila hawawaambiagi wanawake wao ukweli na kujikuta wananuiwa au kusababisha ugomvi, ila mie nimeshawaelewa sanaa hahahahaa.
Kasie.