Imeelezwa kuwa Ole Sabaya anaumwa, kesi yaahirishwa hadi tarehe 4/11/2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita leo Jumatano Novemba 3, 2021 imeahirishwa hadi kesho kwa kuwa Sabaya ni mgonjwa.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana shauri la Sabaya lilipanga kuendelea kusikilizwa leo ambapo shahidi wa upande wa Jamhuri ambaye ni Ofisa wa Tehama wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Nnko, alikuwa aendelee kutoa ushahidi.

Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Alhamisi Novemba 4, 2021 kuwa Sabaya ni mgonjwa na wamepokea taarifa hizo leo asubuhi.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda amekubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho Novemba 4.

MWANANCHI
 
So akikutwa na hatia nyundo zingine zinaongezeka

Sent using Jamii Forums mobile app
Hukumu ingine itaambatana na mengi;
-atawekwa hadharani watu wawe wanamsimanga na kumtemea mate,
-itakodiwa brass-band na kuimba/kupiga nyimbo za kumtweza,
-watamalizia kwa kumpiga mawe hadi azimie na kurudishwa big brother house aka ghetto aka mung'anda akaendelee na kifungo chake pamoja na kazi za kufa mtu.
 
dah haya wazee wa dip state.....mambo magumu sana haya..... lets see if its well coordinated, i see somebody is next...
 
Back
Top Bottom