Imebidi niweke choo cha kuchuchumaa hapa kwangu

Imebidi niweke choo cha kuchuchumaa hapa kwangu

Napoleone

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
10,085
Reaction score
16,064
Wakuu kwa miezi kama 6 hivi nimekua nasumbuliwa na haja kubwa kupelekea starehe ya maliwato kuwa kero hadi nikapata a minor haemorhoid.

Ni kosa langu najua, mfumo wa chakula changu ulibadilika, vyakula vyangu vingi napasha moto yaani fridge langu limejaa mavyakula bibie akija weekend ananipikia misosi ya week nzima mimi nafanya kupasha tuu.

Kipindi niko chuo nilikua napata shida sana vyoo vyetu vilikua vichafu sana hili liende kwa uongozi wa UDSM kule kwenye ma hall especialy hall 5, ni ma vyoo ya kukaa.

Nilianzaga pata tabu sana toka enzi hizo.

Wanasema ukifika 30s jichunge sana na unachokula, lifestyle etc. Nimesadiki hilo na pia kupitia google nmeona maoni mengi yana-suggest kuwa style ya kukaa kwenye vyoo hivi vya kukaa ina mchango mkubwa sana.

Maamuzi, juzi fundi kaja fanya yake hapa kwangu na tokea juzi nimeona mabadiliko makubwa kabisa.

Nashauri vyoo vya kukaa ni sumu, narudia tena ni sumu kwa maendeleo ya anus yako.

Wengi wanakaa kimya tatizo hili ila amini nakwambia wahanga ni wengi mnoo.

Uzi tayar
 
Sababu nyingine hizi hapa
Kutokunywa maji ya kutosha
Kutokula matunda ya kutosha
Kula vyakula vigumu
Kujikamua sana wakati wa kukata gogo
Kabisa mkuu, tena hapo kwenye vyakula daktar aliniuliza, unakula sana nyama. Nikamwambia kwenye mlo wangu nyama lazima iwepo tena ya kukaanga au chomaa, tena natafuna hadi mifupa, akanambia tatzo hilo ndugu.
 
Kula mboga na matunda kwa wingi upate (nyuzinyuzi) fibers za kutosha acha kusingizia choo,

mzee wangu since mid 20s anatumia choo cha kukaa na sasa yupo kwenye 80 sijawah msikia analalamikia hlo tatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom