Kakati
Senior Member
- Apr 11, 2009
- 167
- 47
Naiangalia Tanzania ya mwaka 2073 miaka 50 kutoka leo. Najitenga na ubinafsi nifikiri bila kuzugwazugwa. Nauangalia mfumo wa Muungano wa Tanzania. Najikumbusha mazingira ya kuanzishwa kwake wakati sultani amefurushwa na hatihati za kutinga kwake tena.
Nafikiria wapendavyo wapemba na waunguja kutopoteza utaifa wao wa Zanzibar. Nayajua mapungufu ya mfumo wa unioni yetu unaokinzana na nadharia ya hisabati ya seti, ungano na muungano.
Nawaona wajukuu wetu wakitushangaa kwa nini tumetengeneza dude lisilowezekana. Nawaona wakipiga viboko makaburi yetu.
Natamani tufanye maamuzi magumu lakini ya maana. Tuunganishe kabisa Tanganyika na Zanzibar. Iwe nchi moja, serikali moja.
Mmakonde aweze kumiliki ardhi pemba au unguja kama mpemba anavyomiliki ardhi kigogo au ujiji. Kusiwe na kusigana.
Hoja yangu haijakamilika. Naikamilisha kwa kusema wakati mzuri wa kutimiza hili ni awamu ya sita. Kwa nini?
Kwanza, katika awamu ya hii ya sita hata tukijitahidi vipi, tutaweza tu kukamilisha miradi ya ujenzi ya awamu ya tano, kwa hiyo majengo, mabarabara, reli nk vyote vipya havitatupa sifa mpya. Pili tunaweza tukajenga nchi kuwa moja ikawa ni legacy bora sawa na hiyo miundo mbinu.
Na muhimu zaidi imani yangu ni kuwa jemedari wetu japo kuwa jambo hili laweza kuwa gumu kwake binafsi, kwa baadhi ya wazanzibari au hata watanganyika kutopenda muungano kamili lakini ndiye mwenye nafasi nzuri ya kulifanya kwa kuwa anatoka Zanzibar na ni mwanamke.
Hata kama ni mfupa mgumu, tafuna mama.